Sakata la TZ kuomba eneo baharini. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la TZ kuomba eneo baharini.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jaguar, Jan 25, 2012.

 1. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Baada ya waziri wa makazi,ardhi na nyumba prof.Anna Tibaijuka kuwasilisha ombi la Tanzania kuongezewa eneo la mita kadhaa za mraba baharini,SMZ imekuja juu.Serikali ya mapinduzi ya zanzibar imedai kwamba haikushirikishwa katika mpango huo.Pia SMZ imesema kwamba katika hali halisi,wao Zanzibar ndo wenye haki ya kwenda kuomba kuongezewa eneo baharini tena bila hata kuingiliwa na serikali ya jamhuri ya muungano ya Tanzania.SMZ imesema bara hawana haki yoyote katika suala hili na wamepotoka kwa kuchukua uamuzi huu.
   
 2. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Unafanya marudio au mapitio ya habari????
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo hadi upande wa mtwara wao ndo wenye haki ya kuomba.

  Ila mada ilishajadiliwa
   
 4. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280

  Tags؛‎ wabara hawana haki ya kuomba, bali wazanzibari(japo hawajaona umuhimu wa kuomba).

  Hii naifananisha ni lile sakata la MOU baina ya kundi moja la taasisi za kidini na kisha kundi lingine likadai limeonnewa kutopewa MOU japo halikuomba na lilikuwa halijaona umuhimu wake.
   
 5. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Unaelewa maana ya SMZ au unakurupuka tu kuandika? Hivi Jussa ndo amekuwa SMZ? Usipotoshe watu kwa kitu usichokijua. Kwa taarifa yako SMZ imeshirikishwa kuanzia mwanzo hadi mwisho. Fanya utafiti kabla ya kuja na jambo.
   
 6. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #6
  Jan 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,119
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  watakuwa tayari wameshapata mtu wa kumuuzia,
  tz ni kuishi kiujanja ujanja tu.
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  Zanzibar, what is wrong with their leadership? Kwanini maneno maneno kwenye kila kitu? A sign of weakness??
   
 8. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,238
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  wazanzibar bwana!!! kila kitu wanataka wasikike kila kitu,,, utakuta ni wazee wale wasio na kazi ambao kazi yao kubwa kukaa kwenye vijiwe vya kahawa kutwa nzima...hao hao wanajazana ujinga mwisho wasiku wanazua maneno yasiyo na kichwa wala miguu
   
Loading...