Sakata la Sukari: Wassira afuta vibali feki

Uchaguzi

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
914
Reaction score
171
Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika ametoa agizo la kufuta vibali feki vya kuingiza sukari Nchini, akitoa agizo hilo mbele ya Wadau wote wa Sukari Tanzania, Wassira amepiga marufuku kwa wadau hao wasijaribu kuendeleza tabia ya kuficha sukari ili kuiongezea bei inapokosekana sokoni.

Agizo hilo limepokelewa na Wadau wote na Timu ya ukaguzi na Ufuatiliaji inaanza mara moja kufuatilia utekelezaji.

Waziri Wassira amesema Serikali imeamua kwa dhati kukomesha mazoea,Rushwa na Mianya ya Magendo,Ukwepaji kodi na Vibali feki.

Haya Wadau kazi ni kwenu,Wizara imekuwa ya Moto hii.

image.jpgimage.jpgimage.jpgimage.jpg
Picha: Mhe. Stephen Wassira akiwa na Naibu Waziri Godfrey Zambi, Viongozi wa Wizara ya Kilimo pamoja na Wadau wa Sukari Tanzania.
 
Tunataka utekelezaji maana tatizo la Sukari limekuwa la kudumu, Watanzania wamechoka, Wassira fanya kazi
 
Tatizo Tz kila kitu siasa hapo kesho utakuta kg1 2500
 
Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika ametoa agizo la kufuta vibali feki vya kuingiza sukari Nchini, akitoa agizo hilo mbele ya Wadau wote wa Sukari Tanzania, Wassira amepiga marufuku kwa wadau hao wasijaribu kuendeleza tabia ya kuficha sukari ili kuiongezea bei inapokosekana sokoni.
Agizo hilo limepokelewa na Wadau wote na Timu ya ukaguzi na Ufuatiliaji inaanza mara moja kufuatilia utekelezaji.

Ina maana wizara huwa inatoa vibali feki na wanaviruhusu kutumika kuingiza sukari?
 
Kwanini wasikamate hao wenye vibali feki?
Kwanini wasiwape ruhusa watengenezaji wa sukari wao ndio wawe wanaleta sukari badala ya watu na makampuni binafsi?
 
Uchaguzi

Ooh kumbe waziri aliyekuwepo alikuwa amatoa vibali feki?kweli serikali ya ccm ni ya ukoo wa panya.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: 999
Uchaguzi

Kwa huyo Wasira kuzuia hivyo vibali feki atakuwa amamuimgilia pm ambaye ni rais mtarajiwa hivyo basi watamzania tutegemee ngonjera mpya.
 
Last edited by a moderator:
Hongera Wassira wewe Watanzania wengi wanakuamini, wanakuhitaji uwe Rais wao mwaka huu Sifa kubwa ni Uaminifu na Uadilifu wako, Uzalendo na Mtetezi wa Wanyonge wa daraja la Chini kwasababu unafanana nao. Mungu akubariki.
 
vibali feki unavifutaje wakati hukuvisajili?

Waziri alitakiwa kuamuru kukamatwa na kufunguliwa mashitaka kwa wale wote wanaomiliki vibali feki na wale walioruhusu vibali hivyo kutumika. Lakini hili la "kufuta" vibali feki naona siasa kila sehemu. Enzi za Edward Sokoine (hayati), zitabaki kua ni historia.
 
kumbe vibali feki vinatambulika? nchi hii bana...wananchi wanataka action kama mwakyembe sio blahblah kama lukuvi et al
 
Uchaguzi

Kwa kwa kuanzia sioni sababu kwanini sukari inunuliwe kwa kibali, hivi sasa nchi zote duniani zinaendesha biashara kiushindani kila mmoja aagize bidhaa matokeo yake bei ya bidhaa inaaanguka yenyewe wananchi wananufaika, kitu muhimu cha kutizama kodi halali inachajiwa na bidhaa nzuri zinaletwa nchini siyo kukataza wafanya biashara wasiagize mpaka kwa vibali vinavyotoka serikalini kimagendo.

Mambo ya kulinda viwanda vyetu nchini vimepitwa na wakati viwanda vyetu vinatakiwa vishindane bei na sukari inayoagizwa. Hatukuvilinda viwanda vilipokua mali ya umma na tukaamua kiviuza karibu vyote sasa kwanini tunataka kuvilinda, wananchi tunataka sukari nzuri ya bei nafuu hatujali inatoka wapi au kaleta nani.

Haya mambo ya vibali ndiyo yanatuletea mambo ya rushwa hapa nchini.
 
Wewe ni kipofu na umekurupuka kuchangia suala hapa sio kulinda vieanda
 
Wewe ni kipofu na umekurupuka kuchangia suala hapa sio kulinda viwanda vya ndani ni kufuata utaratibu wa kibiashara. Kwa taarifa yako wakilipa kodi Sukari ya nje itakuwa ghali kuliko ya hapa nchini. Ni siongwe mengi imrnichefua kwa kudandia vitu usivyovijua.
 
Wewe ndio hujamuelewa Farid. Njia rahisi na ya uwazi zaidi ya kulinda viwanda vya ndani bila upendeleo au rushwa ni kuweka kodi kwa sukari inayoingizwa nchini na kuisimamia hiyo kodi. Vibali vya sukari ni biashara karibia ya "unga". Vibali vya uingizaji sukari vilimuondoa Iddi Simba wakati huo waziri wa viwanda na biashara. Na kwa hili wanataka kumchomoa Pinda. So kama Wasira amekiri kulikuwa na vibali "Feki" atueleze ni nani alivitoa. Na vibali hivyo havingeweza kutumika bila Pinda kuvibariki. Hapa tena Pinda anataka kuchomoka kama alivyochomoka ESCROW
 
Unawezaje kufuta vibali Feki???....
 
Mh hapo shida sana tena nchi hii imekwisha ooza kila idara ya serikari vibari feki kweli jamani wakamatwe wote walio hujum uchimi wa nchi yetu masikini ila uchaguzi waja jaman tufanye kweli.
 
Nilitegemea kauli ya kupandisha kizimbani wenye vibali feki na waliotoa vibali feki. Toka lini serikali ikatangaza kufuta vibali feki?
Ova
 
Back
Top Bottom