[h=2]Kigogo wa RITA aliyetoa cheti cha kuzaliwa cha Sitti Mtemvu matatani[/h]
Kigogo wa RITA aliyetoa cheti kwa mtoto wa mbunge Abbas Mtevu ameanzwa kuchunguzwa kama kweli alifuata taratibu za utoaji wa cheti.
Vikao vilikuwa vikiendelea RITA manispaa ya Temeke kujua kama kweli cheti ni original au cha kupika, ingawa taarifa za ukweli ni kwamba cheti hicho ni original.
Inaonyesha Sitti Mtemvu anamiliki vyeti viwili
1. Kabla ya rita kuanzishwa . Ambacho alizaliwa 1989
2. Kipya kinachooonesha ana miaka 18.
Haki itendeke isiwe ugomvi wa wakurugenzi wa Rhino agency ; wanamtupia msala binti Mtemvu.
Ila kweli aisee, nahisi baada ya wazimbabwe sasa tutapangiwa waarabu khaa, mwisho wa mbio za paka sakafuni nauona!!!
Halafu nifah ujue tunachakachua uzi wa watu, huku siyo michezoni ujue!
Akiitwa kujieleza ili ahukumiwe kutokana na kosa lake, atakimbilia mahakamani kuweka zuio la kutojadiliwa na kamati yoyote, hivi ndivyo Tanzania inavyotumia mahakama kama kichaka cha wahalifu.
Hivi ule uchunguzi wa kama huyo binti alifanya udanganyifu kwenye nyaraka zake uliishia wapi? Ilitangazwa kuwa RITA ingefanya uchunguzi juu ya hizo tuhuma
Lakini baada ya hapo sikusikia tena kuhusu hilo jambo hususan baada ya huyo binti kuachia taji lake.Au ndo yaleyale mambo ya 'upepo' na ulishapita huo na watu (Watanzania) kama ilivyo ada yetu tushasahau kabisa.