Sakata la ruzuku ya CUF: Kambaya na Mtatiro ndani ya Star tv

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,068
151,315
Mtatiro atashiriki kwa njia ya simu baada ya kushindwa kufika studio kutoka na kuumwa Malaria.

MADA:SINTOFAHAMU RUZUKU NDANI YA CUF

Kambaya:Katiba ya CUF inamruhusu Naibu Katibu Mkuu(Magdalena Sakaya) kushughulikia maswala ya fedha iwapo Katibu Mkuu atashindwa kutekeleza majukumu yake hayo kwasababu yoyote ile.

Kambaya:Mtariro aliwahi kuingiziwa na chama shilingi milioni mia moja na nane katika akaunti yake binafsi kwa ajili ya uchaguzi wa Igunga(mwaka 2011)

Kambaya:CHADEMA wanataka kuiongoza CUF

Kambaya:Walipanga Mtatiro asifike studio za star tv

Kambaya:Social Media zinatawaliwa/ziko -controled na CHADEMA

Kambaya:Maoni ya watazamaji kuhusu kipindi ni ya maoni ya mashabiki/wanachama wa CHADEMA

Kambaya:Mtatiro nafasi zake ni za uteuzi tu na sio za kuchaguliwa.

Mtatiro:Kwa utaratibu,Katibu Mkuu(Maalim Seif) ndio alipaswa kukaimaisha madaraka hayo( kwa Sakaya kitu ambacho hakikufanyika)

Mtatiro:
Shilingi milioni 108 ziliingizwa katika akaunti yangu kwasababu akaunti ya chama Igunga ilikuwa dormant.Uamuzi ulifanya na vikao halali vya chama na ndipo nikatakiwa kufungua akaunti NMB ili fedha zitumwe kupitia akaunti hiyo kwa ajili ya shughuli za uchaguzi.

Mtatiro:
Wataalamu wa mambo ya benki waalikwe ili waeleze kama utaratibu wote uliotumika kutoa fedha kutoka kwenye ya chama ulikuwa sahihi.

Wamejadili mambo mengi mengine wadau wengine watayaongeza.

Nukuu zangu zinaweza sahihi sana katika kutumia maneno yale yale waliyoyasema ila kwa kifupi ujumbe wao ndio ulikuwa huo
 
Kaka, kama nilivyowajuza nina Malaria +5 na hadi majira ya saa 4.30 usiku huu najisikia weak. Sitahudhuria kipindi hiki muhimu na upande wa chama chetu ungeliweza kumtuma Mhe. Mbarala au Mhe. Hashim Mziray (Wakili) lakini wako nje ya DSM.
Mnisamehe sana.
Mtatiro J.
 
Mtatiro atashiriki kwa njia ya simu baada ya kushundwa kufika studio kutoka na kuumwa Malaria.

MADA:SINTOFAHAMU RUZUKU NDANI YA CUF

Fuatilia mjadala unaendelea star tv.
Ila ingekuwa ndiyo Kambaya anaumwa MALARIA.....ungesikia michango ya NYUMBU HUMU........ila kwasababu ni MTATIRO yeye ni sawa kuumwa MALARIA na kukachaa kukutana ana kwa ana na KAMBAYA......
 
Ila ingekuwa ndiyo Kambaya anaumwa MALARIA.....ungesikia michango ya NYUMBU HUMU........ila kwasababu ni MTATIRO yeye ni sawa kuumwa MALARIA na kukachaa kukutana ana kwa ana na KAMBAYA......
Kambaya yuko vizuri na Mtatiro need to be very careful if he wants his opinion to be heard. Tumeshaona tayari Kambaya kesha take over nafasi ya mtangazaji kwa kumlazimisha kumleta Mtatiro. Mtariro kuwa kwenye simu kuna mnyima nafasi ya kushiriki kikamilifu, Huwezi kutumia simu na panelists labda kama ni commentator. Star TV tayari imeonekana ina position ya kuwabeba CUF Mtatiro. Tazama aina ya maswali ya mtangazaji wa mwanza. Mtatiro need to focus on the questions, not to create his own questions, anapoteza point, swali alilouzwa na Kambaya ni je, Kamati iliyompa uongozi iko ki katiba? simple, hayo mambo ya Lowassa hayana uhusiano haya. Mtatiro abaki kwenye hoja, muda unakwenda na simu inaweza kukatika kabla hajaongea chochote, kwa sasa kama nafasi ikirudishwa kwa Kumbaya, atamamlizwa, abaki kwenye ofisi ya mwenyekiti na sio mwenyekiti. nawakilisha
 
Mtatiro atashiriki kwa njia ya simu baada ya kushundwa kufika studio kutoka na kuumwa Malaria.

MADA:SINTOFAHAMU RUZUKU NDANI YA CUF

Fuatilia mjadala unaendelea star tv.
Mkuu namsikiliza huyu dogo Kambaya....inaelekea kuna katuzo anataka kupewa na CCM dizain ya kina Hapi na Polepole

Hana hoja ya maana.

Ni mfano tu wa msaliti LIPUMBA.
 
Huyu Nyanda nilimuheshimu sana

Lakini kuanzia leo nimemuona mpuuzi mkubwa

Ameshindwa kumhoji kambaya.....kashindwa kabisa


Kambaya aropoka tuuu....anatukana atakavyo


Star tv hovyo kabisa.
 
Back
Top Bottom