Sakata la Polepole Mengi yamesemwa kwa Ubaya na Uzuri

Mkandara

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2006
Posts
15,813
Reaction score
9,063
Asalaam Aleikum - Amani iwe juu yenu.

Kwa muda nimejaribu sana kujizuia kuandika lolote juu ya MKASA wa Kiongozi balozi mstaafu Humphrey Polepole. Mengi yamesemwa kwa Ubaya na Uzuri ili mradi kuridhisha nafsi na malengo ya wasemaji. Lakini UKWELI wa yote unabakia kuwa fumbo la Mbayuwayu.

Mimi nina maswala machache ya Kiutu uzima yanayonitia wasiwasi juu ya Taifa langu, hivyo naomba zaidi Hekima na Busara itumike kwani tunakoelekea sii shwari hata kidogo iwe siku ya Uchaguzi ama baada ya Uchaguzi huu.

Hoja ya kwanza ni pale napowasikia baadhi ya watu Wanasema Polepole kajiteka maana hayupo nchini yuko nje ya nchi hivyo hii ni sinema tu. Yawezekana kweli lakini swali linakuja hivi.

Kama Polepole alikuwa nje ya nchi kwa nini wale wasojulikana walivamia nyumba ya dada yake Wakamteka, wakampiga wakitaka awambie Polepole kajificha wapi? Kulikuwa na umuhimu wowote wa kuvamia nyumba ya dada yake ikiwa wanajua Polepole hayupo nchini? Laa sivyo basi dadake na Polepole wote waliongopa kuvamiwa haikutokea.

Hoja nyingine ni kwamba ikiwa Polepole ni mkosa kumsema vibaya rais wa nchi. Je, kwa kufanya hivyo tulivyomsikia ni 1. kosa la jinai? ama ni 2. Uthubutu wa muumbuzi katika Uzalendo kwa nchi yake (Whistleblower).

Tafakari yangu - katika hali inayoendelea sasa hivi - Je, ni nani haswa anayetakiwa kusema mabaya ya rais ama kiongozi kama itatokea mbeleni tumepata rais fisadi, dikteta, muuaji, na dhalimu? Nani baina yetu sote atakaye thubutu kumfunga Paka kengele? Kesho yetu sote imekaaje...

Ya mwisho kabisa ni kwa wale wanaosema Polepole alihudumu ndani ya Serikali ya Magufuli ambayo ilifanya utekaji na mauaji mengi kwa nini aje leo kuikosoa Serikali hii? Kwa nini asiseme haya wakati ule akiwa madarakani.

Ukweli ni kwamba Polepole alikuwa
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi sio Serikali, na baadae alihudumu kama Mbunge wa kuteuliwa na rais. Na hoja zake zilijikita zaidi kwenye Uongozi wa Chama chake na kukataa Uteuzi wa Mama Samia kuendelea kugombea Urais kwa sababu alizotaja yeye. Haya yote ni maswala ya ndani ya Chama cha Mapinduzi sio Serikali ya JMT, ni bahati mbaya tu kwamba Mwenyekiti wa CCM ndiye rais wa nchi.

Binafsi, nachukulia tuhumu hizo kwa uzito mkubwa sana na nilitegemea kati ya Rostam, rais Mstaafu Jakaya Kikwete, na wengineo walojumuishwa katika kundi hili akiliita WAHUNI kufungua mashtaka mahakamani dhidi ya Humphrey Polepole! Au laa sivyo maswala haya yangemalizwa ndani ya vikao vya Chama - HAIKUTOKEA. - Najiuliza kwa nini?

Siamini katika Uzushi na tungo za kuharibu twasira na hadhi za viongozi wetu lakini pia siamini katika Utekaji na mateso wanayopitia baadhi wananchi kwa sababu wametoa tuhuma nzito dhidi ya Viongozi wa nchi.

Kwa hoja na maandishi haya, nimetumia Uhuru wangu wa fikra kutoa dukuduku langu juu ya hofu ilotanda nchini kuelekea Uchaguzi Mkuu hiyo tarehe 29 October. Siwezi kuweka shaka juu ya matukio na siwezi kaa kimya kwa sababu ya woga!

Tukipoteza HAKI zetu Kikatiba, basi hatutakuwa na Tanzania wanayodai ni hii hii moja. Hiyo Tanzania moja ina upande mmoja tu wa HAKI kwa wote - HAKUNA ALOKUWA JUU YA SHERIA.
 
Hapa Hoja isiwe Polepole, au yoyote wa jana au mwingine wa kesho..., Hoja iwe ni kwanini Uharamia huu na Upuuzi unaendelea kutokea bila kutafutiwa au kuonyesha juhudi za kuzuia: Iwe watekaji au hata wanaojiteka kuweza kufikishwa kwenye utaratibu tuliojiwekea kama jamii iliyostaarabika ? Kila shutuma iweze kufuatiliwa ili mwisho wa siku kama ni kweli watu wafikishwe kwa Pilato na kama wamesingiziwa waweze kusafishika - Tunaelekea kwenye Failed State
 
Nimesema kuna watu wanachezea amani tena ni wenye madaraka Polepole kama ana kosa apelekwe kwenye vyombo vya kisheria kama ni Mahakama basi sio kama walishindwa Kumaliza kwenye vikao vya ndani CCM kwa sasa CCM hamna God father wote wamegeuka kasuku ili jambo lingeisha kichama simple CCM maadali wamekufa Mkapa angekuepo mambo yasingefika huku mzani hauna balance umelalia upande
 
Asalaam Aleikum - Amani iwe juu yenu.

Kwa muda nimejaribu sana kujizuia kuandika lolote juu ya MKASA wa Kiongozi balozi mstaafu Humphrey Polepole. Mengi yamesemwa kwa Ubaya na Uzuri ili mradi kuridhisha nafsi na malengo ya wasemaji. Lakini UKWELI wa yote unabakia kuwa fumbo la Mbayuwayu.

Mimi nina maswala machache ya Kiutu uzima yanayonitia wasiwasi juu ya Taifa langu, hivyo naomba zaidi Hekima na Busara itumike kwani tunakoelekea sii shwari hata kidogo iwe siku ya Uchaguzi ama baada ya Uchaguzi huu.

Hoja ya kwanza ni pale napowasikia baadhi ya watu Wanasema Polepole kajiteka maana hayupo nchini yuko nje ya nchi hivyo hii ni sinema tu. Yawezekana kweli lakini swali linakuja hivi.

Kama Polepole alikuwa nje ya nchi kwa nini wale wasojulikana walivamia nyumba ya dada yake Wakamteka, wakampiga wakitaka awambie Polepole kajificha wapi? Kulikuwa na umuhimu wowote wa kuvamia nyumba ya dada yake ikiwa wanajua Polepole hayupo nchini? Laa sivyo basi dadake na Polepole wote waliongopa kuvamiwa haikutokea.

Hoja nyingine ni kwamba ikiwa Polepole ni mkosa kumsema vibaya rais wa nchi. Je, kwa kufanya hivyo tulivyomsikia ni 1. kosa la jinai? ama ni 2. Uthubutu wa muumbuzi katika Uzalendo kwa nchi yake (Whistleblower).

Tafakari yangu - katika hali inayoendelea sasa hivi - Je, ni nani haswa anayetakiwa kusema mabaya ya rais ama kiongozi kama itatokea mbeleni tumepata rais fisadi, dikteta, muuaji, na dhalimu? Nani baina yetu sote atakaye thubutu kumfunga Paka kengele? Kesho yetu sote imekaaje...

Ya mwisho kabisa ni kwa wale wanaosema Polepole alihudumu ndani ya Serikali ya Magufuli ambayo ilifanya utekaji na mauaji mengi kwa nini aje leo kuikosoa Serikali hii? Kwa nini asiseme haya wakati ule akiwa madarakani.

Ukweli ni kwamba Polepole alikuwa
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi sio Serikali, na baadae alihudumu kama Mbunge wa kuteuliwa na rais. Na hoja zake zilijikita zaidi kwenye Uongozi wa Chama chake na kukataa Uteuzi wa Mama Samia kuendelea kugombea Urais kwa sababu alizotaja yeye. Haya yote ni maswala ya ndani ya Chama cha Mapinduzi sio Serikali ya JMT, ni bahati mbaya tu kwamba Mwenyekiti wa CCM ndiye rais wa nchi.

Binafsi, nachukulia tuhumu hizo kwa uzito mkubwa sana na nilitegemea kati ya Rostam, rais Mstaafu Jakaya Kikwete, na wengineo walojumuishwa katika kundi hili akiliita WAHUNI kufungua mashtaka mahakamani dhidi ya Humphrey Polepole! Au laa sivyo maswala haya yangemalizwa ndani ya vikao vya Chama - HAIKUTOKEA. - Najiuliza kwa nini?

Siamini katika Uzushi na tungo za kuharibu twasira na hadhi za viongozi wetu lakini pia siamini katika Utekaji na mateso wanayopitia baadhi wananchi kwa sababu wametoa tuhuma nzito dhidi ya Viongozi wa nchi.

Kwa hoja na maandishi haya, nimetumia Uhuru wangu wa fikra kutoa dukuduku langu juu ya hofu ilotanda nchini kuelekea Uchaguzi Mkuu hiyo tarehe 29 October. Siwezi kuweka shaka juu ya matukio na siwezi kaa kimya kwa sababu ya woga!

Tukipoteza HAKI zetu Kikatiba, basi hatutakuwa na Tanzania wanayodai ni hii hii moja. Hiyo Tanzania moja ina upande mmoja tu wa HAKI kwa wote - HAKUNA ALOKUWA JUU YA SHERIA.

Ninakazia:

Humphrey Polepole ni Nyerere na Mandela wa zama zetu aliyetwaliwa kutoka kwetu na wasiolitakia mema Taifa hili!
 
Wakati HP yuko Malawi alikuwa akirudi Tz mara kwa mara, Siku ya uapisho/uhamisho wa kwenda Cuba, Mh. Rais alimwambia mbele ya umma kuwa Polepole naambiwa unarudi rudi…

Kusema serikali haikufahamu kuwa HP ameingia nchini ni jambo la uongo, Kati ya watu wachache waliokuwa wanaangaliwa (surveillance) Since 2021 HP ni mmoja wapo ukiacha wale jamaa wa upinzani.

Zaidi ya kampeni yake ya kataa wahuni, nadhani hawakutarajia kama mambo yangefika huko….

WaTz “wengi” hatuna ugomvi mkubwa na serikali yetu zaidi ya kukataa wahuni, Wawarudishe mateka wote kama wanao au kama wana miili yao ili familia zao zipate closure , Is this even too much to ask?
 
..haki ya waliomizwa na kuuwawa na serikali ya Ccm haiwezi kupatikana kupitia serikali za Ccm.

..utawala usiotokana na Ccm ndio utakaowezesha HAKI kupatikana. Na kuna watu wameumizwa katika awamu mbalimbali za uongozi, watu wao wanalia kimyakimya.
 
Wakati HP yuko Malawi alikuwa akirudi Tz mara kwa mara, Siku ya uapisho/uhamisho wa kwenda Cuba, Mh. Rais alimwambia mbele ya umma kuwa Polepole naambiwa unarudi rudi…

Kusema serikali haikufahamu kuwa HP ameingia nchini ni jambo la uongo, Kati ya watu wachache waliokuwa wanaangaliwa (surveillance) Since 2021 HP ni mmoja wapo ukiacha wale jamaa wa upinzani.

Zaidi ya kampeni yake ya kataa wahuni, nadhani hawakutarajia kama mambo yangefika huko….

WaTz “wengi” hatuna ugomvi mkubwa na serikali yetu zaidi ya kukataa wahuni, Wawarudishe mateka wote kama wanao au kama wana miili yao ili familia zao zipate closure , Is this even too much to ask?

Unategemea hatimaye lugha laini ya busara wanaweza kuielewa? Kwamba labda wakiombwa mno hatimaye watasikia na busara kuwarejea?

"Alikosea sana JPM kudhani hatimaye ange ridhiana na wahuni." -- HP.
 
Ili kujenga hoja inanilazimu kumtumia Polepole kwa sababu kwanza niseme ukweli sioni kosa lake Kisheria.

Zaidi ya yote hayo, tuhuma zote alosema Polepole zimeshindwa kujibiwa na Serikali moja baada ya nyingine badala yake wanasaka watu.

Kwani wale wasemaji wa Serikali na Chama kazi yao nini haswa? Tukiendelea na mfumo huu wa kutokanyana - kesho yetu ni Panya gani atamfunga Paka kengele?

Polepole alichofanya ni sawa kamuona Mwanamke alikuwa katika "Abusive marriage" japokuwa mume tajiri lakini ajue ni jambazi.

Kamsihi aachane na ndoa hiyo wala yeye kama ndugu yake haibariki, laa ataiharibu familia kwa tamaa ya fedha na pengine hata yeye kufikishwa mahakamani ikiwa mume atakamatwa. Badala yake mume sijui nani kamtumia majambazi! bado mwanamama haelewi!
 
Shukrani mkuu.
Umetimiza wajibu wako kwa kusema ukweli na kushauri.
 
Hapa Hoja isiwe Polepole, au yoyote wa jana au mwingine wa kesho..., Hoja iwe ni kwanini Uharamia huu na Upuuzi unaendelea kutokea bila kutafutiwa au kuonyesha juhudi za kuzuia: Iwe watekaji au hata wanaojiteka kuweza kufikishwa kwenye utaratibu tuliojiwekea kama jamii iliyostaarabika ? Kila shutuma iweze kufuatiliwa ili mwisho wa siku kama ni kweli watu wafikishwe kwa Pilato na kama wamesingiziwa waweze kusafishika - Tunaelekea kwenye Failed State
Hapo uliposema Polepole hakua kiongozi wa serikali kuna utata,, 1:serikali inatekeleza maagizo ya chama na isipotekeleza chama kina wajibu wa kuisimamia serikali. 2: Viongozi wa serikali sehemu kubwa ndio hao waliopo kwenye chama.
 
Hapana mkuu, Kulingana na Katiba Chama kilichoshinda Uchaguzi Mkuu ndicho huunda Serikali hata kama tunaona inatokana na Wanachama lkn kumbuka rais anaweza mteua kiongozi asokuwa mwanachama wa CCM.

Tunaposema Serikali sio viongozi tu ni pamoja na hao Wanajeshi, Polisi, Wakuu wa taasisi zote za Umma, Wizara, Wakurugenzi na hata Watumishi wa Umma wote ni Sehemu ya Serikali (Executive)

Huwezi sema Mzee Mng'ula, Warioba, Butiku na wengineo wasokubaliana na Mchakato huu nao ni sehemu ya Serikali sijui kwa sababu zamani walikuwa viongozi wa Chama.

Mwisho, wanaotakiwa kuisimamia Serikali ni BUNGE (Kifungu cha 63(2) cha Katiba sio Chama tawala. Chama hakina mamlaka ya kuisimamia Serikali, mfumo huo ni ukiukaji uloanzishwa kinyemela na CCM.
 
Asalaam Aleikum - Amani iwe juu yenu.

Kwa muda nimejaribu sana kujizuia kuandika lolote juu ya MKASA wa Kiongozi balozi mstaafu Humphrey Polepole. Mengi yamesemwa kwa Ubaya na Uzuri ili mradi kuridhisha nafsi na malengo ya wasemaji. Lakini UKWELI wa yote unabakia kuwa fumbo la Mbayuwayu.

Mimi nina maswala machache ya Kiutu uzima yanayonitia wasiwasi juu ya Taifa langu, hivyo naomba zaidi Hekima na Busara itumike kwani tunakoelekea sii shwari hata kidogo iwe siku ya Uchaguzi ama baada ya Uchaguzi huu.

Hoja ya kwanza ni pale napowasikia baadhi ya watu Wanasema Polepole kajiteka maana hayupo nchini yuko nje ya nchi hivyo hii ni sinema tu. Yawezekana kweli lakini swali linakuja hivi.

Kama Polepole alikuwa nje ya nchi kwa nini wale wasojulikana walivamia nyumba ya dada yake Wakamteka, wakampiga wakitaka awambie Polepole kajificha wapi? Kulikuwa na umuhimu wowote wa kuvamia nyumba ya dada yake ikiwa wanajua Polepole hayupo nchini? Laa sivyo basi dadake na Polepole wote waliongopa kuvamiwa haikutokea.

Hoja nyingine ni kwamba ikiwa Polepole ni mkosa kumsema vibaya rais wa nchi. Je, kwa kufanya hivyo tulivyomsikia ni 1. kosa la jinai? ama ni 2. Uthubutu wa muumbuzi katika Uzalendo kwa nchi yake (Whistleblower).

Tafakari yangu - katika hali inayoendelea sasa hivi - Je, ni nani haswa anayetakiwa kusema mabaya ya rais ama kiongozi kama itatokea mbeleni tumepata rais fisadi, dikteta, muuaji, na dhalimu? Nani baina yetu sote atakaye thubutu kumfunga Paka kengele? Kesho yetu sote imekaaje...

Ya mwisho kabisa ni kwa wale wanaosema Polepole alihudumu ndani ya Serikali ya Magufuli ambayo ilifanya utekaji na mauaji mengi kwa nini aje leo kuikosoa Serikali hii? Kwa nini asiseme haya wakati ule akiwa madarakani.

Ukweli ni kwamba Polepole alikuwa
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi sio Serikali, na baadae alihudumu kama Mbunge wa kuteuliwa na rais. Na hoja zake zilijikita zaidi kwenye Uongozi wa Chama chake na kukataa Uteuzi wa Mama Samia kuendelea kugombea Urais kwa sababu alizotaja yeye. Haya yote ni maswala ya ndani ya Chama cha Mapinduzi sio Serikali ya JMT, ni bahati mbaya tu kwamba Mwenyekiti wa CCM ndiye rais wa nchi.

Binafsi, nachukulia tuhumu hizo kwa uzito mkubwa sana na nilitegemea kati ya Rostam, rais Mstaafu Jakaya Kikwete, na wengineo walojumuishwa katika kundi hili akiliita WAHUNI kufungua mashtaka mahakamani dhidi ya Humphrey Polepole! Au laa sivyo maswala haya yangemalizwa ndani ya vikao vya Chama - HAIKUTOKEA. - Najiuliza kwa nini?

Siamini katika Uzushi na tungo za kuharibu twasira na hadhi za viongozi wetu lakini pia siamini katika Utekaji na mateso wanayopitia baadhi wananchi kwa sababu wametoa tuhuma nzito dhidi ya Viongozi wa nchi.

Kwa hoja na maandishi haya, nimetumia Uhuru wangu wa fikra kutoa dukuduku langu juu ya hofu ilotanda nchini kuelekea Uchaguzi Mkuu hiyo tarehe 29 October. Siwezi kuweka shaka juu ya matukio na siwezi kaa kimya kwa sababu ya woga!

Tukipoteza HAKI zetu Kikatiba, basi hatutakuwa na Tanzania wanayodai ni hii hii moja. Hiyo Tanzania moja ina upande mmoja tu wa HAKI kwa wote - HAKUNA ALOKUWA JUU YA SHERIA.
Ukiambiwa habari mtu katekwa, the default ni kuamini habari ya victim mpaka pale itakapogundulika kuwa si kweli.

This is to err on the side of caution when a human life is concerned.

Watanzania wenzetu wengine wengi wanapenda sana kwenda na conspiracy theories bila ya kuangalia facts wala reasoned sensibilities.

Kuna uzi uliletwa hapa juzi, Ben Saanane alikuwa anasema kuna watu wanamtisha watamuua.

Ben Saanane aliweka mpaka namba za watekaji hao.

Watu wakambeza, wakasema anatafuta kick.

Mwishowe in all likelihood Ben Saanane kauswa.

Hao ndio Watanzania wenzetu wengi tu.

Leo kuna ripoti za watu ambao wanaaminika kuwa Polepole kashauawa.

Wao, hao Watanzania wanaosema habari za conspiracy theories, bado wanahoji kama Polepole ametekwa at all.
 
Mwishowe in all likelihood Ben Saanane kauwa.

Hao ndio Watanzania wenzetu wengi tu.

Leo kuna ripoti za watu ambao wanaaminika kuwa Polepole kashauawa.

Wao, hao Watanzania wanaosema habari za conspiracy theories, bado wanahoji kama Polepole ametekwa at all.
Inasikitisha sana, tena jana nimeona mama moja jirani akisema alipofika sehemu ya tukio alikuta nyumba imezingirwa, mtaa umefungwa wamejaa Polisi akauliza kuna nini?

Polisi wenyewe wanakataa ati wanachojua Polepole yuko nje ya nchi, sasa huyu mama muongo? Zaidi ya haya kwa nini asihojiwe Mama mwenye nyumba? Sii ndio upelelezi unavyotakiwa!
 
Hapo uliposema Polepole hakua kiongozi wa serikali kuna utata,, 1:serikali inatekeleza maagizo ya chama na isipotekeleza chama kina wajibu wa kuisimamia serikali. 2: Viongozi wa serikali sehemu kubwa ndio hao waliopo kwenye chama.
Wapi nimesema hivyo
 
Back
Top Bottom