GE2025 Sakata la Mpina kugombea Urais kupitia ACT Wazalendo latua mezani kwa msajili, watakiwa kutoa maelezo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Sakata la kupingwa kwa mtiania wa urais wa ACT Wazalendo, Luhaga Mpina limefika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, huku chama hicho kikitakiwa kutoa maelezo kwa ofisi hiyo kesho Jumatano Agosti 20, 2025.

Mzizi wa hilo, ni barua iliyoandikwa na Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam, Monalisa Ndala akipinga kupitishwa kwa Mpina kuwa mgombea urais, kwa kile alichosema ni kinyume na kifungu cha 16(1)4)I cha kanuni za kudumu za uendeshaji chama toleo la mwaka 2015.

Kwa mujibu wa kanuni hiyo, mwanachama anayewania nafasi ya urais kupitia chama hicho, anapaswa kuwa mwanachama wa zaidi ya siku saba.
Alipotafutwa kuzungumzia hilo, Naibu Katibu wa Mawasiliano, Uenezi na Mahusiano kwa Umma wa ACT Wazalendo, Shangwe Ayo amesema hayuko tayari kulizungumzia hilo.

Awali, alitafutwa katibu mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu, simu yake iliita bila majimbu. Vivyo hivyo kwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara, Issihaka Mchinjita.

Mpina alijiunga na chama hicho Agosti 5 na Agosti 6, 2025 akapitishwa na mkutano mkuu uliofanyika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam kuwa mtiania wa urais wa chama hicho.

Tayari Mpina amekabidhiwa fomu ya kuomba kuteuliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na anaendelea kutafuta wadhamini wasiopungua 200 kila mkoa katika mikoa 10 ikiwemo miwili ya Zanzibar.

Chanzo, Mwananchi
Ccm vopi ? Tuanzie hapa kwa msajili kwanza , vinginevyo ipo siku atakufa mdomo wazi asema Bwana
 
Wenye hizo kanuni watuambie, siku saba zinahesabika kuanzia lini na ukomo wake ni lini. Kisheria Mpina hadi kufikia leo hajateuliwa kuwa mgombea wa Urais bali bado yupo kwenye process za kutafuta uteuzi. Kiutaratibu japo mimi kanuni sijazisoma, Uteuzi wa Urais unaanza mara baada ya Tume ya Uchaguzi kuwatangaza. Na ndio maana hata mtumishi wa umma utumishi wake unakoma mara baada ya kutangazwa na tume kama ni mgombea.
Hoja hii naiona kama inamsukumo wa kutoka ng'ambo ile ya pili
 
Sakata la kupingwa kwa mtiania wa urais wa ACT Wazalendo, Luhaga Mpina limefika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, huku chama hicho kikitakiwa kutoa maelezo kwa ofisi hiyo kesho Jumatano Agosti 20, 2025.

Mzizi wa hilo, ni barua iliyoandikwa na Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam, Monalisa Ndala akipinga kupitishwa kwa Mpina kuwa mgombea urais, kwa kile alichosema ni kinyume na kifungu cha 16(1)4)I cha kanuni za kudumu za uendeshaji chama toleo la mwaka 2015.

Kwa mujibu wa kanuni hiyo, mwanachama anayewania nafasi ya urais kupitia chama hicho, anapaswa kuwa mwanachama wa zaidi ya siku saba.
Alipotafutwa kuzungumzia hilo, Naibu Katibu wa Mawasiliano, Uenezi na Mahusiano kwa Umma wa ACT Wazalendo, Shangwe Ayo amesema hayuko tayari kulizungumzia hilo.

Awali, alitafutwa katibu mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu, simu yake iliita bila majimbu. Vivyo hivyo kwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara, Issihaka Mchinjita.

Mpina alijiunga na chama hicho Agosti 5 na Agosti 6, 2025 akapitishwa na mkutano mkuu uliofanyika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam kuwa mtiania wa urais wa chama hicho.

Tayari Mpina amekabidhiwa fomu ya kuomba kuteuliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na anaendelea kutafuta wadhamini wasiopungua 200 kila mkoa katika mikoa 10 ikiwemo miwili ya Zanzibar.

Chanzo, Mwananchi
Kaka kajichanganya sana! Alafu ujue nguvu ya mpina sio kubwa sana, hivyo naona amejiaminisha hewa kuwa mpinzani wa sa100, mie Bado namwona kama zile katuni alizosema polepole juzi😁😁
 
Sawa, km kanuni zimekiukwa washughulikiwe
Sakata la kupingwa kwa mtiania wa urais wa ACT Wazalendo, Luhaga Mpina limefika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, huku chama hicho kikitakiwa kutoa maelezo kwa ofisi hiyo kesho Jumatano Agosti 20, 2025.

Mzizi wa hilo, ni barua iliyoandikwa na Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam, Monalisa Ndala akipinga kupitishwa kwa Mpina kuwa mgombea urais, kwa kile alichosema ni kinyume na kifungu cha 16(1)4)I cha kanuni za kudumu za uendeshaji chama toleo la mwaka 2015.

Kwa mujibu wa kanuni hiyo, mwanachama anayewania nafasi ya urais kupitia chama hicho, anapaswa kuwa mwanachama wa zaidi ya siku saba.
Alipotafutwa kuzungumzia hilo, Naibu Katibu wa Mawasiliano, Uenezi na Mahusiano kwa Umma wa ACT Wazalendo, Shangwe Ayo amesema hayuko tayari kulizungumzia hilo.

Awali, alitafutwa katibu mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu, simu yake iliita bila majimbu. Vivyo hivyo kwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara, Issihaka Mchinjita.

Mpina alijiunga na chama hicho Agosti 5 na Agosti 6, 2025 akapitishwa na mkutano mkuu uliofanyika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam kuwa mtiania wa urais wa chama hicho.

Tayari Mpina amekabidhiwa fomu ya kuomba kuteuliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na anaendelea kutafuta wadhamini wasiopungua 200 kila mkoa katika mikoa 10 ikiwemo miwili ya Zanzibar.

Chanzo, Mwananchi
Km kanuni zimekiukwa washughulikiwe kwa mujibu wa katiba yao wenyewe.
 
Back
Top Bottom