mwangalingimungu
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 1,300
- 732
Hukumu haijasema Kessy kavunja mkataba Simba, wala haikusema kwamba Yanga imemsajili wakati ana mkataba na Simba. Ilichosema ni kwamba Yanga imepeleka jina la Kessy CAF wakati bado ni mchezaji wa Simba. Ni kosa la utovu wa nidhamu, si la usajili haramu. Asingeweza kusajiliwa kwa ajili ya Ligi kwa kuwa Dirisha Dogo lilishafungwa kitambo. Na bila ya kusajiliwa Ligi ya Ndani asingeweza kusajiliwa Ligi ya CAF. Kilichofanywa ni kuwasilishwa jina lake CAF ili liwahi mfunda (deadline) wa kutumia majina huku usajili ukiendelea. Fundisho hapa siyo kwa wachezaji tu bali hata kwa viongozi wanaoendesha timu kwa hadaa, chuki, tamaa na mazowea.Simba bado wanaweza kuendelea na kumdai Kessy.Kwani mkataba unasema akivunja mkataba sio Yanga kama timu bali Kessy kama mchezaji. Aliyevunja masharti ya mkataba ni Kessy. Na habari za ndani ni kwamba Simba itaendelea kukomaa naye ili iwe fundisho kwa wachezaji wasioheshimu mikataba.