Sakata la mchezaji Hassan Kessy, Simba wako sahihi

njeeseka

JF-Expert Member
Oct 19, 2012
1,371
976
MAAMUZI YA KAMATI YA TFF KUHUSU HASSAN KESSY
Ifuatayo ni taarifa ya Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji

Baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote kwa njia ya mahojiano, na vielelezo Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji imebaini mambo yafuatayo ambayo yanapaswa kuchukuliwa hatua za haraka:

1. Mchezaji Hassan Hamis Ramadhan au Hassan Kessy alikuwa na Mkataba na Klabu ya Simba uliokuwa unaishia tarehe 15/06/2016.

2. Young Africans SC walikiri mbele ya Kamati kupeleka jina la Mchezaji Hassan Ramadhani Kessy huko Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) tarehe 10/06/2016 huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na klabu ya Simba.

3. TFF kupitia Sekretarieti yake ilikuwa na nafasi ya kuweza kuielekeza Young Africans SC hatua stahiki za kuchukua ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Klabu ya Simba kama taratibu zinavyoelekeza. Kama hatua hii ingechukuliwa kwa wakati mwafaka mgogoro huu usingekuwa na sura ya sasa na pengine usingekuwepo.

4. Simba SC walileta machapisho yanayotokana na Mtandao/blog wa mtu waliomtaja kuwa ni Bin Zubeiry ukimwonyesha Mchezaji yuko na viongozi wa Young Africans.

5. Young Africans SC ilionesha Mkataba iliosainiwa na Hassan Hamis Kessy tarehe 20/6/2016 na hivyo hakukuwa na sababu ya msingi ya kufanya mambo yaliyoainishwa kwenye kipengele cha 2 and cha 4 kabla ya kumalizika kwa mkataba kati mchezaji Haasan Kessy na Klabu ya Simba.

6. Bila kuathiri hadhi ya Uanachama wengine wa TFF, Klabu ya Simba ni brand kubwa kama ilivyo Klabu ya Young Africans, umakini mkubwa upaswa kutumika katika kushughulikia brand hizi ili kuepuka madhara yasiyokuwa ya lazima.

HATUA:

Kitendo cha Klabu ya Young Africans kupeleka jina la mchezaji wa klabu nyingine CAF huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na mwanachama mwingine wa TFF ni kosa kubwa kwa mujibu wa kanuni za ligi kifungu 69[5] ambalo linapaswa kupewa adhabu itakayopelekea wanachama wote kuheshimu nafasi ya TFF kwenye suala la usajili na sio kuanza kwenda CAF au kwingineko ili kulinda integrity ya soka la Tanzania.

Klabu ya Young Africans inatozwa faini ya Sh 3,000,000 (Sh milioni tatu) kwa mujibu wa kanuni na fidia kwa klabu ya Simba ya Sh 50,000,000 (Shilingi milioni hamsini).

Ofisa wa TTF aliyehusika ama kwa kushirikiana na Uongozi wa Klabu ya Young Africans au kwa kutochukua hatua stahiki kwa wakati apelekwe kwenye mamlaka yake ya nidhamu, yaani, Katibu Mkuu wa TFF ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dcidi yake.
 
Adhabu ndogo sana Simba watumie haya maamuzi kufungua kesi ya madai. Vipi kuhusu mechi alizocheza Kessy itakuwaje?
 
Simba isikubali hela ndogo sana hii, hela zenyewe za mkwepa kodi, asilimia kadhaa ya fedha anazofanyia jeuri ni za magumashi.
 
Sasa tukisema kuna watu wako TFF kwa maslahi ya Yanga huwa mnabisha nini? Upelekwaji wa jina CAF kafu Yanga walipitia TFF na wakapata baraka.Hili ni jipu kwelikweli.
 
SIMBA WAMESHAONEWA SANA NA KUNYANYASWA TENA KWA MIAKA MINGI. KWA HILI VIONGOZI WASIKUBALI HIYO FIDIA KABISA KWA SABABU HAILINGANI KABISA NA KOSA LILILOFANYIKA. NA ZAIDI WAKATE RUFAA CAF/FIFA KUPINGA HIYO ADHABU NDOGO IKIWEZEKANA YANGA WANYANGA'NYWE POINTI ZOTE KWA MECHI ALIZOCHEZA KESSY ILI LIWE FUNDISHO KWA BAADHI YA VIONGOZI WA TFF NA KLABU YANGA.
 
Adhabu ndogo sana Simba watumie haya maamuzi kufungua kesi ya madai. Vipi kuhusu mechi alizocheza Kessy itakuwaje?
Usajiri wa Yanga vpl uko sawa kwani alikuwa amemaliza mkataba ndiyo maana kipengelebkilichowabana ni kupeleka jina cuf tarehe 10.6.2016 wakati mkataba wa Kessy na Simba ulikuwa unaisha tarehe 15.6.2016.
 
Hamsini tu. Mkude naye tutamsainisha kwa mfumo huo huo. Mkipiga sana kelele mtakuja kulipwa million 50 nyingine.
Wapiga dili wa mikia tayari wameishajua mgawo wao6katika hizo 50.
Mkuu, angalau hapa haki imeonekanabkutendeka tofauti na swala la Mbuyu, Yondani, Ramadhani sing'ano orodha inaendelea...halafu kumbuka ilikuwa imebaki siku nne mkataba uishe halafu tulikuwa tumemfungia ingawa kimkataba hata kama ilikuwa imebaki sekunde...
 
SIMBA WAMESHAONEWA SANA NA KUNYANYASWA TENA KWA MIAKA MINGI. KWA HILI VIONGOZI WASIKUBALI HIYO FIDIA KABISA KWA SABABU HAILINGANI KABISA NA KOSA LILILOFANYIKA. NA ZAIDI WAKATE RUFAA CAF/FIFA KUPINGA HIYO ADHABU NDOGO IKIWEZEKANA YANGA WANYANGA'NYWE POINTI ZOTE KWA MECHI ALIZOCHEZA KESSY ILI LIWE FUNDISHO KWA BAADHI YA VIONGOZI WA TFF NA KLABU YANGA.
Hahaha kessy alikuwa kabakisha siku 5 mkataba uishe ....lilipofunguliwa dirisha bado alikuwa na mkataba? Naona mnataka yanga inyanganywe point vipi mmechoka kupumuliwa nyuma?
 
Hivi takukuru wameishia wapi na Aveva?
Kwani wao hawapendi pesa..!? Anyway Aveva alihojiwa kuwa zilepesa zilizokuwa zinatumw Hongkong zilikuwa za nini ? Akawaambia ni za ununuzi Wa Nyasi za uwanja na nyasi ziko Bandari hutaki nenda kazione...kosa kwanini ziingie kwenye account binafsi, jibu kufanya transaction kutoka account binafsi ni rahisi kuliko ya taasisi kwa hiyo Simba kama wanamashaka ni kujiridhisha he nyasi zipo, je zina thamani husika....
 
Hamsini tu. Mkude naye tutamsainisha kwa mfumo huo huo. Mkipiga sana kelele mtakuja kulipwa million 50 nyingine.
Wapiga dili wa mikia tayari wameishajua mgawo wao6katika hizo 50.
Cha mijinga huliwa na mjanja. Mlijitia wajuaji. Mngeandika barua tu ya kuomba kuidhinishiwa. Siku 5 za mkataba zimezaa milioni 50.Mhindi sidhani kama atakubali kulipa kirahisi.Lazima vichwa vita roll kwa ujinga huu.
 
SIMBA WAMESHAONEWA SANA NA KUNYANYASWA TENA KWA MIAKA MINGI. KWA HILI VIONGOZI WASIKUBALI HIYO FIDIA KABISA KWA SABABU HAILINGANI KABISA NA KOSA LILILOFANYIKA. NA ZAIDI WAKATE RUFAA CAF/FIFA KUPINGA HIYO ADHABU NDOGO IKIWEZEKANA YANGA WANYANGA'NYWE POINTI ZOTE KWA MECHI ALIZOCHEZA KESSY ILI LIWE FUNDISHO KWA BAADHI YA VIONGOZI WA TFF NA KLABU YANGA.
hahahaha we mbumbumbu siku yanga akipokwa point sababu ya kessy naomba uongozi wa jf unipige ban ya miezi12
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom