Sakata la MCC: Wamarekani waonesha dalili ya kulegeza KAMBA

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,504
MCC imeitaka Tanzania kukaa chini na kuangalia ni hatua gani za kuridhisha inaweza kuchukua ambazo zitapelekea MMC Board iweze kurejesha fedha za msaada zilizozuiliwa.

Msemaji wa Shirika hilo bibie Renee Kelly amesema kama hatua hizo za serikali ya Tanzania itakazochukua zitakuwa za kuridhisha basi watarejesha pesa hizo bila tatizo.

“The Government of Tanzania needs to determine how it will rectify the specific issues of concern,”
“It is up to MCC’s Board to determine if any such actions taken by the Government of Tanzania are sufficient to warrant re-instatement.”

Msemaji huyo alipohojiwa kama suala la Zanzibar kurudia uchaguzi ndilo litakalosababisha pesa hizo kurudishwa Mwanamama huyo alikataa kusemea swala hilo, ila akasisitiza kuwa sio kazi ya MCC kuamua nini cha kurekebisha, ila ni kazi ya serikali ya Tanzania kuamua nini cha kurekebisha.

"MCC does not provide checklists,” akimaanisha MCC haikuamulii nini cha kurekebisha.

Naona kuna kitu kilikuwa kinatafutwa zaidi ya hili suala la uchaguzi wa Zanzibar, Ishu ya Zanzibar inaanza kupotezewa mdogo mdogo, sasa naanza kumuelewa Waziri aliposema watanzania msiwe na wasiwasi hakitaharibika kitu, hawa jamaa tutaelewana nao tu mbele ya safari na pesa wataachia.

Source:http://www.nation.co.ke/news/africa...mption/-/1066/3143796/-/117wu69z/-/index.htmlhttp://www.thecitizen.co.tz/News/Ac...told/-/1840340/3144236/-/rsb7l3z/-/index.html
 
Kulegeza Kamba wapi hapo unaona? Kamba ilipokazwa wapi na ilipolegezwa wapi? Tofauti iko wapi kimsingi mpaka uone Kamba imelegezwa?

Tatizo nililoliona ni kwamba, tangu mwanzo, MCC hawakuwa na nia ya kukataa kutoa misaada, despite ya matatizo ya Zanzibar. Tatizo lilikuwa serikali ya Tanzania haikujali hata kujieleza kwamba haya matatizo yapo na tunayafanyia kazi.

Sasa mtu akisema kwamba serikali ya Tanzania ikijieleza misaada inaweza kurudishwa anakuwaje kalegeza kamba wakati hilo halijabadilika na lilikuwa hivyo hivyo tangu mwanzo?
 
Kulegeza Kamba wapi hapo unaona? Kamba ilipokazwa wapi na ilipolegezwa wapi? Tofauti iko wapi kimsingi mpaka uone Kamba imelegezwa?

Tatizo nililoliona ni kwamba, tangu mwanzo, MCC hawakuwa na nia ya kukataa kutoa misaada, despite ya matatizo ya Zanzibar. Tatizo lilikuwa serikali ya Tanzania haikujali hata kujieleza kwamba haya matatizo yapo na tunayafanyia kazi.

Sasa mtu akisema kwamba serikali ya Tanzania ikijieleza misaada inaweza kurudishwa anakuwaje kalegeza Kamba wakati hilo halijabadilika na lilikuwa hivyo hivyo tangu mwanzo?
Oficial statement ya MCC mwanzo ili-base katika suala la Uchaguzi wa Zanzibar kama ishu kuu ya kuyimwa hizo hela, cha ajabu sasa MCC haitaki hata kuizungumzia hii ishu, inachotakiwa ni serikali ya Tanzania kuchukua hatua za kuridhisha tu.

Na msemaji kadai MCC kasema MCC haiichagulii Tanzania ishu za kurekebisha, maana yake iamue yenyewe cha kurekebisha provided kwamba hatua hizo zitaridhisha.

Unataka uambiwe nini tena ujue kuwa ishu ya Zanzibar wameamua kuipiga pini??
 
Unajuaje kwamba suala la uchaguzi wa Zanzibar serikali ya Tanzania ingelijadili vizuri na MCC kusingekuwa na kuondolewa kwa misaada?

Kama MCC ilichotaka ni maelewano tu na serikali ya Tanzania tangu mwanzo, serikali ya Tanzania ikashindwa kujadili suala, na sasa MCC inasisitiza kwamba bado ipo tayari kujadiliana na serikali ya Tanzania ili misaada irudishwe, kamba imelegezwa wapi hapo?

Watu kama walitaka majadiliano tangu mwanzo, na wanasisitiza kujadiliana mpaka sasa, ilipolegezwa hasa kamba ni wapi hapo?
 
Tangu awali MCC ilionesha kuna kitu inatafuta, pesa zilizokuwa zitolewe kabla ya October zilizuiliwa kwa kisingizio cha "mpaka uchaguzi upite", uchaguzi ulipoisha ikaja ishu ya "mpaka Zanzibar wamalize uchaguzi" uchaguzi wa Zanzibar wakaja na ishu ya "uchaguzi wa Zanzibar haukuwa huru na shirikishi", sa hizi tena wanakuja na ishu kuwa tukae chini tuamue nini cha kui-convice MCC itoe hela.
Hakukuwa na maelewano yoyote ambayo MCC ilikua inatafuta kuhusu suala la Zanzibar, ila kuna "kitu" zaidi ya hayo maelewano.
 
Sawa, kuna kitu wanatafuta.

Unajuaje kwamba kitu hicho si acknowledgement tu kwamba kuna matatizo ya Zanzibar na serikali ina commit kuyatatua hivi na vile?

Na kama hivyo ndivyo, kamba ilipolegezwa ni wapi?

Ikiwa serikali ya Tanzania imekataa kutoa hiyo acknowledgement na commitment tangu mwanzo, na all along MCC ilichotaka ni hiyo acknowledgement na commitment tu, ambayo haikutolewa mwanzo na haijatolewa mpaka sasa, kamba ilipolegezwa ni wapi?
 
Tangu awali MCC ilionesha kuna kitu inatafuta, pesa zilizokuwa zitolewe kabla ya October zilizuiliwa kwa kisingizio cha "mpaka uchaguzi upite", uchaguzi ulipoisha ikaja ishu ya "mpaka Zanzibar wamalize uchaguzi" uchaguzi wa Zanzibar wakaja na ishu ya "uchaguzi wa Zanzibar haukuwa huru na shirikishi", sa hizi tena wanakuja na ishu kuwa tukae chini tuamue nini cha kui-convice MCC itoe hela.
Hakukuwa na maelewano yoyote ambayo MCC ilikua inatafuta kuhusu suala la Zanzibar, ila kuna "kitu" zaidi ya hayo maelewano.
Wanataka serekali iendelee na mikataba ya Symbion kampuni ya America
 
Magufuli endelea kukaza tu baada ya muda hao ma-MCC watakuelewa tu
Kwa nini unataka MCC wamuelewe?

Kwa nini ni muhimu MCC wamuelewe?

Watamuelewaje ikiwa wanachotaka ni majadiliano naye na yeye hata kuongea nao hataki?
 
Bunge lijalo litunge sheria ya kukataa misaada....

Misaada inatudumaza... Tujitegemee kwa kidogo tulichonacho.
Kwa Tanzania bado Sana kujitegemea!kikubwa kinachotakiwa kufanyika ni pesa zote za misaada zitumike ipasavyo kwa asilimia 100% zisiishie mkononi kwa wajanja....ambao kutwa ni kuvaa tai na kuendesha v8 kwa fedha hizo....
 
Kwa nini unataka MCC wamuelewe?

Kwa nini ni muhimu MCC wamuelewe?

Watamuelewaje ikiwa wanachotaka ni majadiliano naye na yeye hata kuongea nao hataki?
Watamuelewa pale atakapokataa moja kwa moja kupokea msaada wao na bado nchi ikaendelea kusonga mbele na kusimama
 
Kwa nini hajafanya hivyo sasa hivi?

Unafahamu hesabu za kuendesha nchi?
 
Back
Top Bottom