Sakata la Madini: Maftah Nachuma ampinga Tundu Lissu

Waweke Wazi Hiyo Mikataba Ili Tujuwe Nani Anaonge Ukweli. Kama Hawatafanya Hivyo Watakuwa Wanatafuta Kiki Coz Kila Mtu Anaongea Lake.
 
MBUNGE MAKINI WA MTWARA MJINI MAFTAH NACHUMA (Cuf) AMPINGA TUNDU LISSU WA (Chadema)
Imeandikwa na Maftah Nachuma (MB)
Mikataba yoote ya kimataifa huongozwa na wajibu wa aina mbili. Wajibu ulioandikwa(express obligation) na wajibu ambao haukuandikwa(implied obligation).
Wajibu ulioandikwa ni masharti yote ya mkataba yaliyo katika maandishi ambayo wahusika husoma na kuridhia, wakati wajibu usioandikwa ni masharti ya mkataba ambayo hayakuandikwa katika mkataba lakini yapo kwa asili au yapo kwakuwa tayari yalishasemwa na sheria na hivyo si lazima kuyaandika ktk mkataba.
Mathalan, mfanyakazi wako wa duka hawezi kukuibia halafu akasema kwenye mkataba wangu wa ajira hakuna sharti la uaminifu. Laa hasha uaminifu ni sharti la asili "implied obligation" kwa hiyo liandikwe au lisiandikwe bado lipo tu.
Kwenye mikataba ya kimataifa kama ile ya kwetu na makampuni ya madini masharti yafuatayo ni ya asili na hayahitaji kuwa yameandikwa ili kuyatekeleza :
1. Wajibu wa kuanika taarifa zote muhimu kuhusu shughuli inayotekelezwa katika mkataba( Implied covenant to disclose all necessary information over the subject matter).
2. Wajibu wa kutekeleza na kutenda kwa nia njema(Implied covenant to act in good faith and fair dealing).
3. Wajibu wa kila mhusika katika mkataba kuwa mkweli . Hili huwa ni katazo la udanganyifu(Fraud).
Haya yawe yameandikwa kwenye mkataba au hayakuandikwa yakikiukwa tafsiri yake ni kukiuka masharti ya mkataba.
Matendo kama kulaghai kuhusu uzito wa madini yanayochukuliwa, kulaghai kuwa unachukua dhahabu huku ukijua unachukua zaidi ya dhahabu, kulaghai kuhusu bei , kutotoa taarifa sahihi za kipi unapata na kipi hupati,nk ni kukiuka wajibu na masharti ya mkataba jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Na ikiwa wamekiuka mkataba kwa misingi hiyo basi Tanzania inaweza kufanya yafuatayo;
1. Kuendelea na mkataba lakini kwa sharti la kurudisha kile chote kilichopotea kwa mda wote( specific performance).
2. Kutoendelea na mkataba na kudai fidia, hasara tuliyopata,pamoja na riba zake kwa kipindi chote(
breach of contract).
Ndugu zangu, wajibu wa kutekeleza na kutenda kwa nia njema (implied covenant to act in good faith and fair dealing), kuwa mwaminifu na kutoa taarifa sahihi katika utekelezaji mikataba ni matakwa ya lazima duniani kote.
Sheria ya biashara ya Amerika Uniform Commercial Code vifungu vya 1 - 12 habari hii imeelezwa kwa upana.
Sheria ya biashara ya Ufaransa na Ujerumani The German Civil Code(BGB) na Civil Code of France zimeeleza vitu hivi.
Pia mahakama kuu ya Uingereza katika kesi ya Yam Seng PTE vs International Trade Co. Ltd (2013) EWHC 111 ( QB) iliamua kuwa masuala ya uaminifu na kutoa taarifa sahihi katika kutekeleza mikataba ni wajibu ambao upo hata Kama haukuandikwa kwenye mkataba.
Halikadhalika sheria yetu ya Mikataba, Sura ya 345 vifungu vya 18 na 13 vimeyafanya masuala ya udanganyifu na kutoa taarifa zisizo sahihi kama mambo ambayo ni makosa na yanayobatilisha mkataba.
Kamati ya Profesa Mruma imebaini upotevu wa Bilioni 829.4 x Miezi 12 kwa miaka 18 = Trilioni 829.4. Hizi ni pesa nyingi mno. Tunayo kesi nzuri ya madai na uhakika wa kurejesha fedha tulizopoteza. Ni vema mda huu pamoja na mambo mengine, nguvu nyingi ikatumika kuona ni namna gani tunapata hii fedha. Makosa yapo na yametendwa na hilo halina Shaka. Iko wapi haja kukhofu, hakika haipo.
Yumkini haitakuwa rahisi kutokana na aina ya mabepari ambao tunashughulika nao. Ni mabepari hatari wenye mtandao mkubwa wa kisiasa na nchi wafadhili pamoja na taasisi kubwa kama IMF, WB, UN nk.
Hata hivyo tumeshasema hii ni vita na vita sharti ipiganwe ili waliosiginwa wawe huru. Tunaweza kuumia kwa mda ila mwisho wa maumivu hayo itakuwa ni neema kubwa na ya milele.
Ni wakati sasa watanzania wote bila kujali Itikadi za vyama au Dini kuungana pamoja kupigania haki yetu.
Prof Ibrahimu Lipumba alionya jambo hili miaka kumi wakati wa utawala wa awamu ya tatu lakini serikali haikuchukua hatua za msingi.
Mungu ibariki Tanzania na mbariki rais kwa pamoja tushinde vita hii.
MAFTAH NACHUMA Mbunge Mtwara mjini.

MUNGU akubariki na wewe kwa kuzidi kuchangia Kwenye hii vita ya udhurumaji. Kuna watu wanautumia upinzani vibaya. Upinzani sio kwa jambo kama hili, hili jambo linataka Watanzania wote tuungane bila ya kujali tofauti zetu kwani hii ni vita ya kuokowa maisha yetu na vizazi vyetu.
 
Hii habari yote neno kwa neno...mbona ina jina la Bashir Yakub hata kwenye blogs na mleta mada umeandika jina la huyo Mbunge? Lipi ni lipi haswa?

Mbunge aliandika wapi haya, watu waone ni kweli?
 
Makofi tafadhali! Tanzania moja watu wamoja na lugha ni moja. Mungu ibariki Tanzania na watu wake. Pamoja tutashinda, na penye ukweli uongo hujitrnga.
Mbunge wa Mtwara nakuunga mkono.You are absolutely right.Akina Lisu kisiasa hawana ajenda.Sasa wameamua kula na kumeza matapishi yao.Wamenunuliwa.Lakini hawatafika mbali.
 
Wewe mbona sijaona palipompinga Lissu? Au mihemko!!!!!! Kumbuka lkn Lissu aliwekwa ndani sababu ni kutetea maslahi ya Nchi kwenye huohuo mgodi.... Lissu ni habari nyingine.. Alianza mapambano ya ukombozi miaka mingi sana
 
Badala yakupambana na mikataba mibovu naona sasa tunajadili lissu kana kwamba yeye ndio alikuwa waziri wa nishati na madini au mwanasheria Mkuu wa Serikali.
 
Huu ni umburula uliobeba viwango vya kiuwendawazimu, kwanini huyu Maftah asiikosoe ccm juu ya sera zake mbovu za mikataba ya madini kuliko kuanza kujadili maoni ya kiutaalam toka kwa mwanasheria nguli. Mtu yeyote makini atampuuza Maftah na hii C&P toka kwa Lipumba.
Mwanasheria nguli au mwanasheria mbishi??, Lissu sasa sio mtalaamu tena basi anaendeshwa na mihemko ya kisiasa
 
MBUNGE MAKINI WA MTWARA MJINI MAFTAH NACHUMA (Cuf) AMPINGA TUNDU LISSU WA (Chadema)
Imeandikwa na Maftah Nachuma (MB)
Mikataba yoote ya kimataifa huongozwa na wajibu wa aina mbili. Wajibu ulioandikwa(express obligation) na wajibu ambao haukuandikwa(implied obligation).
Wajibu ulioandikwa ni masharti yote ya mkataba yaliyo katika maandishi ambayo wahusika husoma na kuridhia, wakati wajibu usioandikwa ni masharti ya mkataba ambayo hayakuandikwa katika mkataba lakini yapo kwa asili au yapo kwakuwa tayari yalishasemwa na sheria na hivyo si lazima kuyaandika ktk mkataba.
Mathalan, mfanyakazi wako wa duka hawezi kukuibia halafu akasema kwenye mkataba wangu wa ajira hakuna sharti la uaminifu. Laa hasha uaminifu ni sharti la asili "implied obligation" kwa hiyo liandikwe au lisiandikwe bado lipo tu.
Kwenye mikataba ya kimataifa kama ile ya kwetu na makampuni ya madini masharti yafuatayo ni ya asili na hayahitaji kuwa yameandikwa ili kuyatekeleza :
1. Wajibu wa kuanika taarifa zote muhimu kuhusu shughuli inayotekelezwa katika mkataba( Implied covenant to disclose all necessary information over the subject matter).
2. Wajibu wa kutekeleza na kutenda kwa nia njema(Implied covenant to act in good faith and fair dealing).
3. Wajibu wa kila mhusika katika mkataba kuwa mkweli . Hili huwa ni katazo la udanganyifu(Fraud).
Haya yawe yameandikwa kwenye mkataba au hayakuandikwa yakikiukwa tafsiri yake ni kukiuka masharti ya mkataba.
Matendo kama kulaghai kuhusu uzito wa madini yanayochukuliwa, kulaghai kuwa unachukua dhahabu huku ukijua unachukua zaidi ya dhahabu, kulaghai kuhusu bei , kutotoa taarifa sahihi za kipi unapata na kipi hupati,nk ni kukiuka wajibu na masharti ya mkataba jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Na ikiwa wamekiuka mkataba kwa misingi hiyo basi Tanzania inaweza kufanya yafuatayo;
1. Kuendelea na mkataba lakini kwa sharti la kurudisha kile chote kilichopotea kwa mda wote( specific performance).
2. Kutoendelea na mkataba na kudai fidia, hasara tuliyopata,pamoja na riba zake kwa kipindi chote(
breach of contract).
Ndugu zangu, wajibu wa kutekeleza na kutenda kwa nia njema (implied covenant to act in good faith and fair dealing), kuwa mwaminifu na kutoa taarifa sahihi katika utekelezaji mikataba ni matakwa ya lazima duniani kote.
Sheria ya biashara ya Amerika Uniform Commercial Code vifungu vya 1 - 12 habari hii imeelezwa kwa upana.
Sheria ya biashara ya Ufaransa na Ujerumani The German Civil Code(BGB) na Civil Code of France zimeeleza vitu hivi.
Pia mahakama kuu ya Uingereza katika kesi ya Yam Seng PTE vs International Trade Co. Ltd (2013) EWHC 111 ( QB) iliamua kuwa masuala ya uaminifu na kutoa taarifa sahihi katika kutekeleza mikataba ni wajibu ambao upo hata Kama haukuandikwa kwenye mkataba.
Halikadhalika sheria yetu ya Mikataba, Sura ya 345 vifungu vya 18 na 13 vimeyafanya masuala ya udanganyifu na kutoa taarifa zisizo sahihi kama mambo ambayo ni makosa na yanayobatilisha mkataba.
Kamati ya Profesa Mruma imebaini upotevu wa Bilioni 829.4 x Miezi 12 kwa miaka 18 = Trilioni 829.4. Hizi ni pesa nyingi mno. Tunayo kesi nzuri ya madai na uhakika wa kurejesha fedha tulizopoteza. Ni vema mda huu pamoja na mambo mengine, nguvu nyingi ikatumika kuona ni namna gani tunapata hii fedha. Makosa yapo na yametendwa na hilo halina Shaka. Iko wapi haja kukhofu, hakika haipo.
Yumkini haitakuwa rahisi kutokana na aina ya mabepari ambao tunashughulika nao. Ni mabepari hatari wenye mtandao mkubwa wa kisiasa na nchi wafadhili pamoja na taasisi kubwa kama IMF, WB, UN nk.
Hata hivyo tumeshasema hii ni vita na vita sharti ipiganwe ili waliosiginwa wawe huru. Tunaweza kuumia kwa mda ila mwisho wa maumivu hayo itakuwa ni neema kubwa na ya milele.
Ni wakati sasa watanzania wote bila kujali Itikadi za vyama au Dini kuungana pamoja kupigania haki yetu.
Prof Ibrahimu Lipumba alionya jambo hili miaka kumi wakati wa utawala wa awamu ya tatu lakini serikali haikuchukua hatua za msingi.
Mungu ibariki Tanzania na mbariki rais kwa pamoja tushinde vita hii.
MAFTAH NACHUMA Mbunge Mtwara mjini.

AMEKURUPUKA TU HUYU.
 
Napendekeza serikali imujumuishe mbunge wa Mtwara kwenye jopo la kuitetea kwenye kesi iliyofunguliwa na ACACIA. Unajua sakata la mchanga limeinua ma-bush lawyers kibao.
 
Huu ni umburula uliobeba viwango vya kiuwendawazimu, kwanini huyu Maftah asiikosoe ccm juu ya sera zake mbovu za mikataba ya madini kuliko kuanza kujadili maoni ya kiutaalam toka kwa mwanasheria nguli. Mtu yeyote makini atampuuza Maftah na hii C&P toka kwa Lipumba.
Mmoja wapo mimi nimeshapuuzia.
 
Back
Top Bottom