Sakata la Lovness Tarimo limejaa ukakasi

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,669
698,657
Wakati mijadala ikielekea mwishoni kuhusiana na kijana Lovness Tarimo na jinsia yake ambaye kwa mwonekano tuu huwezi kumuweka kwenye jinsia ya like bali ya kiume.

Na hata kama ni mwanamke basi ana silika nyingi za kiume kuliko za kike... Lovness ni mwalimu wa mazoezi gym na ana misuli ya kutosha sana.

Sakata lake lilizidi kuchukua sura mpya mitandaoni baada ya kuwahakikishia watu kupitia mahojiano mbalimbali kwamba yeye ni mwanamke na ana mchumba na hivi karibuni anatarajia kuolewa.

Tukiachana na maswali ya maandishi wetu ya kumuuliza kwamba ni lini aliondolewa ubikira wake na kama anaingia kwenye siku zake kama wanawake wengine, juzi akajitokeza mwanadada aliyedai ni mke halali wa Lovness walikuwa wanaishi Wote Canada na wana mtoto.

Mwanadada anadai mme wake Lovness aliondoka Canada wiki mbili zilizopita na kurudi Tanzania na nipo kupitia mitandaoni akasoma habari hizo za aibu za mumewe kujitangaza ni mwanamke

Mdada huyo akiongea kwa uchungu na majonzi huku akijizuia sana asilie kutokana na habari za mumewe huyo aliahidi kufanya lolote ili apate pesa za kumtibia mumewe kwakuwa anaamini kuna kitu Kibaha kimempata mpaka kufikia kufanya aliyofanya

Kitu kilichokuja kumpa mshtuko karibia azirai ni pale mwandishi aliyekuwa anaongea naye kumwambia mchumba wa kiume wa Lovness ni mzungu

Sasa hebu tujiongeze kidogo tusijekuwa tunalishwa matango pori na Hizi bongo muvi zisizoisha

Ni nani alimuibua Lovness Tarimo?
Ni nani aliyehakiki jinsia yake?
Ni nani aliyejaribu kuhoji background yake?

Je huyo mchumba mpya wa Lovness kuna mwandishi alihangaika kumtafuta na kumhoji?

Kwa mwanamama anayedai Lovness ni mumewe wa ndoa na walikuwa wanaishi wote Canada, je kuna ithibati zozote kazitoa hasa nyaraka kuthibitisha madai yake?

Kwa mwandishi aliyemhoji huyo mwanamama imekuwaje ndio huyohuyo alimhoji Lovness!? Je ni coicedence ama?

Hii habari ina ukakasi mwingi, lakini poa kwa wazazi kama ikithibitika Lovness ni mwanaume je ni sahihi kumpa mtoto wa kiume jina ambalo limekaa kike?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

View: https://www.instagram.com/reel/Czy_oDeM6ks/?igshid=MzRlODBiNWFlZA==
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…