Sakata la Lissu "Handle with care"

Mwenyewe umesema huku kwetu hakuna kufuata sheria ni kuoneana tu, likely na Lissu anatafutiwa sababu ya kufungwa.
 
Mwenyewe umesema huku kwetu hakuna kufuata sheria ni kuoneana tu, likely na Lissu anatafutiwa sababu ya kufungwa.
Na akiendelea hivi basi ujue anako elekea ni magereza. Hovi weee unafikiri Lissu akifungwa nini kitatokea? Nchi itachafuka au wazungu watakata misaada? Ukweli ni kuwa maisha yataendelea huku uraiani kama kawaida na atasahulika haraka sana.
 
Hakuna sharia hapa yeye anataka maendeleo.
Sasa hiyo mikutano na maandamano inazuiaje maendeleo? Walioweka sheria na taratibu hawakujua kuwa kuna maendeleo? Na mbona yeye rais anafanya mikutano na kuingiza wanachama katika CCM?
 
Kuna kitu kinaitwa Presidential Decree.
Hakuna kitu kama hicho kunapokuwapo na katiba na uchaguzi wa kidemokrasia. Hicho huwapo pale nchi inapopinduiwa ikiwa katika kipindi cha mpito. Hicho iliwahi kuwepo hapa baada ya muungano wakati katiba ikiandaliwa. Baada ya hapo raisi akiapa kufuata katiba na akienda kinyume cha hapo hafai kuwa rais hata baba wa taifa alishawahi kusema sifa ya kwanza ya rais ni kufuata katiba aliyoapa kuongoza nchi. Alisema kinyume cha hapo ni uhuni. Rejea wakati ule wa Mwingi kwenye sakata la IOC na vugu vugu la kurudishwa kwa Tanganyika. Katiba ndio sheria mama mkuu na hakuna presidential decree Tanzania kwa sasa labda uniambie mabavu au hicho wanachomshtakia Lissu kinachohusiana na mambo ya uchwara! Ndio maana wapinzani wanatumia katiba na sheria zinazotambua shughuli zao lakini rais anasema tu mimi sijaribiwi mara oh mimi ndiye rais kana kwamba kuna mtu kasema yeye sio rais. Sasa kwa maelekezo ya rais vyama visivyokuwa na wabunge na madiwani lakini vina usajili wa kudumu visifanye mkutano? Na chama nini? Si watu? Sasa utaendeshaje chama bila kukutana na wanachama na kutafuta wanachama wapya? Si hata madhehebu ya dini yanafanya hivyo hivyo ndio maana unaona mihadhara na mikutano ya kidini ya hadhara na kupitia vyombo vya habari. Yote hiyo ni kuhubiri imani yao na kupata waumini au wafuasi wapya ili kukua na kujiimarisha vinginevyo basi baada ya watu kuokoka kungekuwa hakuna haja ya kuendelea na mahubiri au basi watu wangesali mara moja au mbili kwa mwaka. Ukweli ni kuwa katika mahali ambapo JPM anaiharibu CV yake yeye mwenyewe ni hapa kwenye kupiga marufuku mkutano na maandamano ya vyama vya siasa wakati yeye na CCM yake wakifanya na vile kuwapangia pa kufanya hii inabomoa umoja wa kitaifa. Vyama vimesajiliwa kitaifa na vinapaswa kufanya kazi hivyo yeye anasema wafanye tu kule walikochaguliwa. Analeta utengano badala ya utangamano! Mr. President, please rethink!
 
Serikali inacheza mziki wa Lissu
Kwa jinsi ilivyo badala ya kucheza itachezewa sana kwakuwa yenyewe haina sheria za kuhalalisha hayo inayoyafanya wakati mwenzao ana sheria na kanuni zinazoruhusu mikutano na maandamano kikatiba na sheria ya vyama vya siasa
 
Reactions: BAK
Wapuuzi wenzako walishashituka kuwa walifanya kosa kumuondoa Gadaf bado wewe tu. yaelekea kwako Libya ya sasa ni Bora kuliko ile ya gadaf! kweli kwenye dunia hii kuna mataahira mengi sana.
Libya ya Iraq au kuwait mkuu.
 
Alifungwa Shekhe Ponda Issa Ponda waliojifanya want mihemko naye wakafyata mikia hapo hamna kitu anaweza kufungwa na wasifanye lolote
 
Dikteta anajiamini kupita kawaida, anadhani watanzania tunamuona malaika kumbe tunamuona kichekesho
Yaani nimeahidi mbele ya Mungu sitaki tens kusikiliza hotuba zake wala kuangalia TV kwa kipindi chote atalacho kaa madarakani kwani nafsi yangu imekereka kupita Maelezo.Hivi anadhani Nchi hii Ni take kama familia yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…