Sakata la Lissu "Handle with care"

Kisingizio cha siku zote huwa ni kuepusha uvunjifu wa amani
 
Kitu gani kinakufanya udhani CCM na serikali hawana mikakati ya kumaliza mbinu zenu dhaifu.
 
Jambo kubwa linalohitajika hapa ni ''Busara''. Kuhimili mikiki mikiki ya kukosolewa na kukosoana, hata kama Serikali inaendeshwa na malaika lazima iwe na ngozi ngumu kuhimili kukosolewa.
Magufuli alianza vizuri ila kadri siku zinavyokwenda anarudi kwenye square one.
 
Kitu gani kinakufanya udhani CCM na serikali hawana mikakati ya kumaliza mbinu zenu dhaifu.
Kama kila upande utakuwa na mikakati ya kumaliza upande mwingine unatabiri nini kitatokea.
 
Watawala wanachoshindwa kukifahamu ni kwamba kuna watu ambao wamejitoa kafara kwa alili ya kuwatetea wananchi na wako tayari kwa lolote,wako tayari hata kukatwa kichwa ilimradi wahakikishe adhima yao inatimia.

Watu wenyewe ni kama hawa wa aina ya Lissu ambao huwezi ukawanyamazisha kwa kuwakamata na kuwafunga gerezani na hata kama utatumia mabavu yako kwa kuwafunga bado wataendelea kupiga kerere hukohuko gerezani.

Na usipotumia akili jinsi ya kudili na watu wa aina hii utaishia kuwapaisha bure kwa kuwa ulishindwa namna ya kuchukuliana nao,kama siyo kuwapaisha utajikuta unawakata vichwa.

Ukifiri kuwa ndiiyo njia ya kumaliza tatizo kumbe ndiyo unazalisha tatizo lingine,kwa kuwa unapomkata Lissu kichwa ndiyo wanazaliwa akina Lissu wengine maelfu na maelu na huku jela inakusubiri kwa kuwa hakuna atakayekubaliana na wewe umkate mwenzako kichwa eti kwa kuwa mmetofautiana naye kimtazomo.

Na kwa kuwa wewe ni mbabe unayemiliki vyombo vya dola basi unahaki ya kujifanyia chochote unachotaka na huku watu wakikuchekea na kukupigia makofi pwaa,pwaa kama mazuzu vile.

Makaburu wa Afrika ya kusini waliwaua wapinzani wao na kumfunga Mandela wakiamini kuwa hiyo ndo njia sahihi ya kuwanyamazisha wapinzani wao haki ya kudai haki yao.

Mwisho wake waliishia kubana makalio yao na kupiga saluti mamilioni na mamilioni kwa mtu waliye mnyanyasa na kumdhihaki huku wakiimba tata Madiba Nelson Mandela.
 
Kama kila upande utakuwa na mikakati ya kumaliza upande mwingine unatabiri nini kitatokea.
Ushindi kwa mwenye mkakati bora na rekodi zetu zinaonesha CHADEMA na UKAWA hawajawahi kushinda.
 
Afungiwe tu huyu Jamaa ,mnafiki sana.

Tokea amsafishe Lowasa watanzania wenye akili hawana imani nae tena
 

Una akili sana
 
Ushindi kwa mwenye mkakati bora na rekodi zetu zinaonesha CHADEMA na UKAWA hawajawahi kushinda.
Wewe ushindi unaupima kwa kigezo gani kuingia ikulu?

Mimi nasema hapana kigezo cha ushindi ni utekelezaji wa sera bora whether ni za upinzani au chama tawala. Na kama utaupima kwa kigezo cha data tangu 1992 basi CCM wanazidi kupungukiwa na upinzani kuongeza katika nyanja zote utazofikiri.
 
Iramba mashariki? Duuuu Kaka unajua ukikimbia sana unaweza kupitiliza mpaka kwenu aisee.
 
Fafanua ni damu gani zinazomwaga kila mwaka chini ya utawala wa Magufuli.
Wewe jifunze kusoma na kuelewa dhima ya hoja ndani ya sentensi au aya. Ni wapi ametajwa Magufuli katika hiyo aya? Acha kuvuruga hoja za watu na kuleta uchonganishi wa kitoto. Jibu hoja na kama huna isome na kuipisha. Siyo kupretend kila hoja una cha kuongezea au kuipinga.
 
Magufuli alianza vizuri ila kadri siku zinavyokwenda anarudi kwenye square one.
Sijui karogwa na nani mwanzo hata mi nilifikiria kumpa kura yangu 2020 ila sasa mmh, nishaghairi
 
Mkuu umeona mbali sana ila waache kwanza wenyewe hawajashtumia ishu bado. Wanaenda kama makondoo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…