Sakata la kuvamia viongozi: Ndesamburo anusurika

Ochu

JF-Expert Member
May 13, 2008
975
47
Ndesamburo nusura avamiwe mkutanoni
Mussa Juma, Moshi

MBUNGE wa Jimbo la Moshi mjini, Philemon Ndesamburo juzi nusura avamiwe baada ya walinzi wa Chadema kumuwahi mwanamke mmoja aliyekuwa akimfuata huku akiwa ameshikilia kalamu ambayo alidhaniwa kuwa angeitumia kumjeruhi mbunge huyo.

Tukio hilo lilitokea kwenye uwanja wa eneo la Majengo wakati wa moja ya mikutano ya hadhara inayoendeshwa na chama hicho kote nchini ikiwa imepewa jina la Operesheni Sangara.

Mama huyo alionekana akielekea eneo alilokuwa Ndesamburo wakati wa tukio la kukusanya fedha za kufanikisha mikutano ya Operesheni Sangara, fedha zilizokuwa zikikusanywa na Ndesamburo, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Dk Willibrod Slaa, ambaye ni katibu mkuu, waliokuwa chini ya jukwaa.

Msichana huyo, ambaye jina lake halikuweza kufahamika mapema, alikamatwa na walinzi wa Chadema hatua chache kabla ya kumfikia Ndesamburo na akapokonywa kalama hiyo.

Kukamatwa kwake kuliamsha hisia kwa mamia ya watu waliokuwa kwenye mkutano huo, baadhi yao wakitaka kumshambulia kabla ya kutolewa tangazo kuwa mwanamke huyo hakuwa na akili timamu.

"Mwacheni huyu... hata kama katumwa hana akili timamu," alisema mmoja wa walinzi wa Chadema ambao walikuwa wamemkamata mwanamke huyo.

Haikueleweka kama mwanamke huyo alipelekwa kwenye vyombo vya dola kwa hatua zaidi.

Awali kwenye mkutano huo, Ndesamburo aliilalamikia Halmashauri ya Moshi na madiwani kwa kukwamisha mpango wake wa kuwatengea eneo la soko jipya wananchi wa wilaya hiyo.

Ndesamburo alisema baada ya halmashauri hiyo kuwahamisha wafanyabiashara katika soko la Kiborironi, aliamua kununua eneo kwa ajili ya wafanyabiashara hao, lakini akasema halmashauri na madiwani wamekataa eneo hilo litumike kama soko.

"Nimefikisha malalamiko yangu mpaka kwa Rais (Jakaya) Kikwete na yeye akasema anakubaliana na mimi, lakini uamuzi ni wa meya na madiwani ambao wamegoma," alisema Ndesamburo.

Hata hivyo, alisema bado ataendelea na harakati na kumtaka Rais Kikwete kuishinikiza manispaa ya Moshi kukubali eneo alilonunua liwe soko kwa ajili ya manufaa ya wakazi wa Moshi.

Akizungumzia suala hilo kwa njia ya simu jana, mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Benadetta Kinabo alisema halmashauri iliamua kuwahamisha wafanyabiashara katika eneo la Kiborironi kwa kuwa soko hilo lilikuwa barabarani.

Hata hivyo, alisema halmashauri hiyo, inaendelea na mipango ya kuboresha soko jipya la Memorial kwa kuboresha miundo mbinu.


new trend ya watanzania
 
Back
Top Bottom