Sakata la fedha za CUF na tathmini ya uzito wa habari hii katika magazeti ya leo

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,671
149,843
Baada ya CUF jana kutoa tuhuma nzito ni namna gani fedha za chama hicho zilivyochotwa,leo hii nimefanya tathimini fupi kuona ni jinsi gani Wahariri wetu walivyoripoti juu ya habari hii(wameipa uzito kiasi gani).

Nadiriku kusema kile nilichokisema jana kuhusu namna gani habari hii itakavyoripotiwa katika magazeti ya leo, ndio hicho kilichotokea.

kwa mfano gazeti moja limeandiki hivi(heading):

"CUF YA LIPUMBA YAPEWA RUZUKU-UK 4"

Maoni yangu kuhusu ni namna gani habari inaweza kuripotiwa na magazeti ya leo unaweza kuyasoma kupitia link hii hapa chini.

Leo hii na kesho angalieni uzalendo wa vyombo vya habari

Mimi leo sitaki kuwa msemaji ila naomba kila aliepitia magazeti ya leo atupe tathimini yake hasa ukizingatia tuko katika awamu inayojinadi kupambana na rushwa,wizi na ufisadi
 
Wewe ni nani mpaka uwapangie waandishi cha kuandika?
Mmiliki mwenyewe wa gazeti haruhusiwi kuwapangia waandishi cha kuandika.
Kila mtu akitaka kiandikwe anachokitaka unafikiri hivyo vyombo vya habari vitakuwaje? mnalalamikia udikteta wa Magufuli na ninyi mnaufanya huo huo.
 
Kwako wewe habari za ruzuku ya CUF ni kitu cha muhimu Wengine habari za uchumi wa Tanzania na ushauri wa IMF ndicho cha muhimu.
 
Wewe ni nani mpaka uwapangie wahariri cha kuandika?
Mmiliki mwenyewe wa gazeti haruhusiwi kuwapangia wanadishi cha kuandika.
Kila mtu akitaka kiandikwe anachokitaka unafikiri hivyo vyombo vya habari vitakuwaje? mnalalamikia udikteta wa Magufuli na ninyi mnaufanya Huo huo.
Kitakachosaidia watanzania kujua kwa undani ni nini kinaendeles katika nchi hii ni mitandao ya kijamii tu na si hivi vyombo rasimi vya habari.

Hela itoke hazina iingizwe kwenye account ya chama isiyo rasimi na kisha itolewe na kuingizwa kwenye account ya mtu binafsi ni tuhuma nzito sana lakini ukiangali jinsi ilivyoripotiwa huwezi kuamini.

Habari imeripotiwa kama ni issue ndogo sana katika baadhi ya magazeti huku mengine wala hayaandiki chochote.

Katika magazeti mengi niliyoyaona,habari hii ni habari kuu katika gazeti la Mtanzania pekee(Tanzania Daima na Jamuhuri bado sijayaona ila nitayatafuta).

Kuna baadhi ya heading ukisoma kwa mtu asiejua ni nini kimetokea anaweza kuona ni kama habari ya kawaida tu na hakuna jambo zito lililotokea.

Vita ya rushwa,wizi na ufisadi nchii hii ni ya kinafiki sana na inapewa uzito pale mh.sana anapokuwa amesema jambo au kuchukua hatua fulani.
 
Wahariri wanatafuta ukuu wa wilaya baba ,haujui kuwa ukikandya sana ccm ukuu wa wilaya itakupita kushoto au unafikiri hawatamani mashangingi
 
Huyu anahaki ya kuchambua ila amekisea ilitakiwa na yeye atoa comment ya anavyo ona yeye!
 
Wewe ni nani mpaka uwapangie waandishi cha kuandika?
Mmiliki mwenyewe wa gazeti haruhusiwi kuwapangia waandishi cha kuandika.
Kila mtu akitaka kiandikwe anachokitaka unafikiri hivyo vyombo vya habari vitakuwaje? mnalalamikia udikteta wa Magufuli na ninyi mnaufanya huo huo.
Acha uoga wewe
 
Mshangao Ni Pale Chadema Wanaposhupalia Mgogoro Wa Cuf Kuliko Wana Cuf Wenyewe, Wamekazana Mapovu Hadi Mishipa Ya Shingo Imewatoka.
 
Tuwashange nyinyi mnaotetea wizi huku mkijidai hii ni awamu ya kupiga vita rushwa na ufisadi.
 
Hayo yanawahusu wao,mie sina la kusema.zingekuwa zetu si zingenunua panadol hospital?anayejua wanavyozitumia achangie tu.
 
Baada ya CUF jana kutoa tuhuma nzito ni namna gani fedha za chama hicho zilivyochotwa,leo hii nimefanya tathimini fupi kuona ni jinsi gani Wahariri wetu walivyoripoti juu ya habari hii(wameipa uzito kiasi gani).

Nadiriku kusema kile nilichokisema jana kuhusu namna gani habari hii itakavyoripotiwa katika magazeti ya leo, ndio hicho kilichotokea.

kwa mfano gazeti moja limeandiki hivi(heading):

"CUF YA LIPUMBA YAPEWA RUZUKU-UK 4"

Maoni yangu kuhusu ni namna gani habari inaweza kuripotiwa na magazeti ya leo unaweza kuyasoma kupitia link hii hapa chini.

Leo hii na kesho angalieni uzalendo wa vyombo vya habari

Mimi leo sitaki kuwa msemaji ila naomba kila aliepitia magazeti ya leo atupe tathimini yake hasa ukizingatia tuko katika awamu inayojinadi kupambana na rushwa,wizi na ufisadi
Tatizo lako unataka wahariri wafikiri kama unavyofikiri wewe.Ruzuku amekabidhiwa Lipumba ambaye ni mwenyekiti halali wa cuf tatizo lipo wapi?Humjui Magdalena sakaya ni nani?kwa nini bavicha mnaumizwa sana na mambo ya cuf?
 
Ukiona ma-CCM yanatetea jambo uje wana maslahi nalo.
 
Kama Serikali ya JPM itakaa kimya au itafinyanga ishu hii, tutakuwa tumerudi miaka 50 nyuma katika Vita ya Kupambana Na ufisadi, rushwa, ubadhirifu wa mali ya umma.
Huu Ni zaidi ya wizi.....kuna dalili za ugaidi. Hii pesa kwa mamilioni imeingia mikononi mwa watu hawazidi watatu au wanne.
Swali la kujiuliza; Wamezihifadhi wapi hadi sasa Hivi!?. Haiwezi kuwa imepelekwa msituni kufadhiri makundi yenye nia ovu dhidi ya viongozi wanaopingana nao!?
CUF ya Li-Pumba wanakiri kuzichukuwa pesa zile lakini hawaelezi wamezipeleka wapi!!
Leo Rais yuko Simiyu, tunategemea atoe Kauli (hata kama Ni Tata) juu ya suala hili kama alivyotangaza kumtumbua Mramba akiwa kanisani.
Vinginevyo, nitatangaza kupoteza imani Na Serikali hii
 
Bado una imani na hawa watu mkuu?CCM ni ile ile hata iongozwe na malaika.
 
Back
Top Bottom