SAKATA LA ESCROW: Ole Naiko ajitetea Hakujua kama amewekewa Mamillioni

Hela zimeingia February 2014 kwenye account yake. Vyombo vya habari vimeripoti NOvember 2014 jina lake, yaani miezi tisa baadaye. Utasemaje hukujua miezi yote hiyo?

Inashangaza sana! Kama ni kweli anaweza kukaa miezi tisa bila kufuatilia mwenendo wa akaunti yake ina maana ni mzembe kiasi ambacho hakustahili hata kushika wadhifa aliokuwa nao TIC!
 
Ni sahihi kuna watu hawana tyme na baadhi ya akaunti hadi zinakuwa dormant
 
wewe mzee Naiko acha kutudanganya,Regemalila alijuaje Una account mkombozi bank, na kwa nini akuwekee wewe sio Mimi wala yule.?
kwa nafasibyako uliyokuwa nayo by that time, Kama mkurugenzi wa uwekezaji..uliongwa bana.tafuta utetezi mwingine wewe fisadi..
barrick gold walikuonga mpaka wakakupa chairman wa board of directors kwan atujui..
 
unaeza kuta alitoa ndani ya masaa 24 tangu kuwa transffered!
afu bado nasema hakuona hadi aliposikia kwenye vyombo ya habari,
sasa huyu ndo alikuwa director wa uwekezaji nchini na utetezi ambao upo sawa na akili ya Lusinde, sijui hawa viongozi wanajuaga wananchi ni wajinga kiasi gani!

km alitoa mwizi mi nlikuta kias flani kwenye account yangu niliuliza sikutoa mpaka umepita mwezi na bado nkaulizia kumbe ile pesa nilikua naekea na benki yenyewe maana account yangu ni junior
 
Mtu akuwekee mamillioni ya $ kwenye account usijue wala huulizi ? Hawa watu kweli wameshatufanya sisi wajinga
 
Watu wanafanya utani sasa. Hata kutafuta majibu ya maana wanashindwa. Fedha imewekwa Mwezi Machi hadi leo hajui, je hiyo account kazi yake nini, ilifunguliwa lini? Kwa maelezo ya wengine ni kuwa watu wote waliopewa fedha na Ruge ni kuwa kabla ya kufanya hivyo walielekezwa ili kupata fedha hizo walitakiwa kufungua account Mkombozi benki bila hivyo hawapati hizo fedha. Mbali na hivyo kama hakujua walipata wapi account namba yake na kuweka fedha? Akae afikirie anjiandae na majibu mazuri. Siyo suala la kulalamika kuchafuliwa, amejichafua mwenyewe. Kama alichosema ni kweli hizi fedha hazina mwenyewe.
 
Fedha ziliwekwa february,yeye anasema ameisikia bungeni kwa mara ya kwanza!!Inamaana haja angalia acc. Yake toka mwezi wa pili?
 
Katika distribution ya pesa zilizotoka kwa rugemalira hakuna kitu kama hicho ilikua ni 40,80,160, n.k. Halafu Escrow Account ilitumika zikiwa BOT baada ya kutolewa BOT ziliwekwa kwenye account nyingine na huko jina la Escrow halikutumika tena. Hayo unayosema ni vichekesho kama vichekesho vingine.
Ni kweli unaweza kusema ni vichekesho lakini hiyo ndicho kilichotokea na ni ngumu kuamini hata mie ilikuwa ngumu mpaka alivyonionesha bank statement ndio nikaamini
 
Haiwezekani mtu asijue kinachoendelea katika bank account yake for 9 months.Haiwezekani mtu ukute mil 40.4 kwenye account yake without his concern.
This is a complete conspiracy its time for Tanzanian's to wake up,to stand on their own to fight for their country's freedom.Its a shame to see our Leaders whom we've entrusted power to are corrupt.I recall a poem from Kundi Faraja which have the following:
``..I plead the stomachs
of the priviledged few
greater than the rift valley
they can not be satisfied
with a normal share..''Also he proceeds saying:
``..I plead the thirst of the minority greater than that of Sahara no rain can quench it
I reckon the minority more sensitive to egoism than to nation building nothing that is not theirs is of any interest
Their response to egoism is faster than the camera film to light but as slow as tropism to nation building..''
Its an high time for we Tanzanian's to stand up for our country which is rich in resources but has a great number of poor people.Its time to wake up
 
Nimeshangazwa na kauli ya aliyekuwa mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji kusema kwamba Hana taarifa kuwa akaunti yake iliyopo Mkombozi bank imewekwa fedha milioni 40 bila yeye kuwa na habari. Maswali ninayojiuliza hivi inawezekanaje mtu akuingizie fedha bila kukutaarifu kwa kipindi cha miezi karibu 8 na ukaikuta na wewe bila kuuliza hizi fedha Ni za nini mpaka usikie kwenye vyombo vya habari? Huyu mzee kwa mtazamo wangu angenyamaza asiseme chochote hii kauli yake imenisikitisha Sana na sasa ninapata mashaka kuwa fedha zilizotolewa Ni rushwa.
 
Wengine wanatumia watoto maskini kama ngao zao, wakati hao watoto maskini hiyo fedha na wao wanaiona kwenye magazeti. You can't have it both ways. You are either dirty or clean. If you are dirty, even if you use the best perfume, the stink will not go.
 
Swali dogo tu alifungua account lini na kwa madhumuni gani? Lini alikuta hela ya ruge kwenye account yake? Au mpaka alivyoona jina kwenye gazeti ndio akaenda kuhakikisha?
 
No free launch kutakuwa na fadhila analipa. Account yangu mbona ameisahau
 
Back
Top Bottom