Gambamala
JF-Expert Member
- May 13, 2014
- 1,045
- 766
Sakata la ESCROW limewakumbusha Watanzania walio wengi sakata la Richmond ambalo ndilo lililomtoa Lowasa madarakani. Watanzania taratibu walianza kusahau ufisadi wa Richmond na kuanza kumuunga mkono Lowasa, lakini baada ya kutokea Sakata la ESCROW sasa Watanzania wamekumbuka kuwa ndani ya CCM uwezi kupata kiongozi mwadirifu, hakika Watanzania wakisikia sakata la ESCROW wanaanza kumchukia Lowasa kwa kuwa na yeye alitolewa madrakani kwa sakata kama hili, kwa kuwa nalo linahusisha TANESCO, kweli hii inakumbushia machungu ya RICHMOND. Ukitazama kwa undani ESCROW ni mtoto wa Richmond. Richmond kidogo imilikishwe kwa IPTL, lakini Richmond ikazaa Symbion, Sasa ESROW ni account ya IPTL.