Sakata la ESCROW: Magufuli mkamate Seth wa IPTL

Mpangawangu

JF-Expert Member
Mar 5, 2014
887
965
Wasomi wataka wabunge wamalizane na kiporo cha SETHI

IPTL/PAP yawazuia wabunge kuliibua upya suala hilo.

Yadaiwa kutumia Mahakama kujikinga dhidi ya maamuzi ya Bunge

Yamtumia Rais Mstaafu Kikwete kujitetea wasifilisiwe

Yamshitaki Zitto Kabwe Mahakama Kuu

Zitto Mwenyewe ajibu mapigo

Waziri Muhongo atakiwa kukaa upande wa Umma sio SETHI

Na Mwandishi Wetu.

JUMUIA ya Wanazuoni Watetezi wa Rasilimali nchini (JUWARA), imewataka wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania linalotarajia kuanza rasmi vikao vyake vya kujadili hotuba ya Rais aliyoitoa wakati wa kulizindua bunge hilo hapo kesho, kumuomba na kumkumbusha Rais DK. John Pombe Magufuli kutoa agizo la kukamatwa mara moja kwa mfanyabiashara Harbinder Sing Sethi ambaye ni mmiliki wa kampuni ya IPTL/PAP inayoendesha mtambo wa kufua umeme wa dharura uliopo tegeta Salasala kama sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge lililopita .

Wanazuoni hao wamesema kuna kila sababu ya wabunge wa bunge hili la 11 kusimama imara ili kutetea rasilimali za taifa letu zinazoonekana kutafunwa na wajanja wachache wanaotumia visingizio dhaifu vya sheria na uwekezaji kwa kumtaka Rais John Magufuli aharakishe utekelezwaji wa maazimio hayo ya Bunge hasa azimio namba moja lililoitaka serikali kumchukulia hatua kali na kumkamata mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Herbinder Sing Seth kwa makosa ya kulisababishia taifa hasara ya zaidi ya bilioni 320 kutokana na wizi uliofanyika katika akaunti ya TEGETA ESCROW.

Pia, jumuia hiyo imesema ina imani kubwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo huku ikimtaka awe mwangalifu na asiwe mtetezi wa IPTL safari hii kwa kuwa maamuzi ya bunge yalikuwa sahihi dhidi ya kampuni hiyo, ambayo imeisababishia hasara kubwa serikali kutokana na vitendo vyake vilivyofanya.

Wakizungumza na JAMVI LA HABARI, Mwenyekiti na Katibu wa Jumuia hiyo, Omary Kisambu na Mahmud Salibaba kila mmoja,w ameonyesha kusikitishwa na kitendo cha serikali kumkumbatia mfanyabiashara huyo, anayelalamikiwa na watanzania wengi kwa kulitia hasara taifa kutokana na vitendo vyake alivyovifanya kwenye sakata nzima la akaunti ya Tegeta Escrow.

"Tunashangaa mpaka sasa mapendekezo na maazimio muhimu ya Bunge kuhusu TEGETA ESCROW hayajatekelezwa na badala yake wameishia kuwatoa kafala kina William Ngeleja na Anna Tibaijuka, hii haitakiwi kuachwa ipite hivi hivi, lazima kama vijana wasomi tusimame kidete kupigania taifa letu na rasilimali zake" alisema Mwenyekiti huyo.

Naye, Katibu wa Elimu na Mawasiliano wa Jumuia hiyo, Mahmud Salibaba amelinukuu azimio namba moja na kushangaa kuona serikali imekubali kutekeleza azimio namba nane wakaliacha azimio namba moja ambalo linahitaji utekelezaji tu.

Mahmud aliongeza kuwa azimio namba moja linasema

"Bwana Harbinder Singh Seth na wengine,Bunge linaazimia kwamba, TAKUKURU, Jeshi la Polisi na Vyombo vingine husika vya Ulinzi na Usalama, vichukue hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, dhidi ya watu wote waliotajwa na Taarifa Maalumu ya Kamati, kuhusika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na Miamala ya Akaunti ya Escrow, na watu wengine watakaogundulika kufuatia uchunguzi mbalimbali unaoendelea kuhusika katika vitendo vya jinai". Aliinukuu.

Katibu huyo, alisema "Hatuna wasiwasi na Prof. muhongo, Tunaamini ana mapenzi mema na utayari wa kulitumikia taifa katika sekta hii, lakini kwenye hili tunamtaka aweke mbele maslahi ya Taifa na kamwe asigeuke kuwa mtetezi wa IPTL wala Sethi".

Wanazuoni hao wameendelea kuonyesha matumaini yao kwa Bunge hili huku wakiamini kwamba kama ilivyo kawaida ya mabunge yaliyotangulia, panapotokea masuala ya kitaifa yenye maslahi mapana kwa nchi basi wabunge wav yama vyote huungana na kuweka tofauti zao pembeni na kulisimamia taifa liokoe rasilimali zake.

IPTL/PAP YAMZUIA ZITTO KABWE KUZUNGUMZIA.

Wakati hayo yakiendelea, kampuni hiyo inayolalamikiwa kuingizia hasara ya mabilioni serikali na kupelekea kuwajibishwa kwa watumishi kadhaa wa umma, imejitokeza na kuwataka wabunge waache kulizungumzia suala hilo kwa kuwa bado lipo mahakamani.

Katika taarifa iliyosambazwa kama tangazo iliyosainiwa na Katibu na Mshauri mkuu wa sheria wa Kampuni hiyo, Joseph Makandege, imemtaka Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto kutokuendelea kulizungumzia suala hilo na kwamba aache mpango wake wa kutaka kulifufua upya suala hilo hasa bungeni kwa kuwa tayari kampuni hiyo imeshamshitaki katika kesi ya madai iliyopo mahakama kuu na kwamba haitakuwa busara kwa mbunge huyo kulizungumzia suala hilo ambalo yeye binafsi ana maslahi nalo.

Kadharika taarifa hiyo inasema kwamba tayari serikali imejibu kupitia hotuba ya Rais mstaafu Jakaya kikwete pindi alipokuwa madarakani kuwa haipo tayari kumkamata Sethi wala kutaifisha mitambo hiyo kwa kuwa itasababisha kuanzishwa kwa mahusiano mabovu na wawekezaji, hivyo Makandege amesisitiza kwamba ni vema mbunge huyo na mbunge mwingine yoyote aachane na mpango wa kuliibua suala hilo bungeni. ‘’kwa uelewa wetu mdogo kuhusu maswala haya, kauli ya Rais huwa ndio kauli ya mwisho na ni sawa na hukumu, na tayari Rais (Rais Mstaafu Kikwete) alishasema kuwa suala hilo haliwezekani ‘’. Ilisisitiza taarifa hiyo ya Makandege.

‘’katika hali ya kiubinaadamu, si vema kwenda bungeni kushusha lawana na tuhuma kuwatuhumu watu na ama kampuni ambazo zenyewe haziwezi kuingia bungeni kujitetea’’. Ilisema sehemu ya taarifa hiyo

‘’hata mheshimiwa Zitto alifanya makosa kujihusisha na suala la IPTL/PAP wkati akijua kuwa ameshtakiwa mahakamani na kwamba moja kwa moja anakuwa na mgogoro wa kimaslahi, japo hajatamka mahala popote kuwa ana mgogoro wa kimaslahi na sakata husika’’. Iliongeza sehemu ya taarifa hiyo

ZITTO AWAJIBU

Naye mbunge wa Kigoma mjini ACT – WAZALENDO ambaye wakati wa mjadala wa sakata hilo la ESCROW alikuwa mwenyekiti wa kamati ya Bunge inayosimamia hesabu za serikali, amejibu taarifa hiyo kwa kusema ni ya uongo inayoambatana na uoga wa kuwajibishwa na bunge baada ya kugundua maovu yao na kwamba IPTL /PAP hawana mamlaka ya kisheria kumzuia mbunge kujadili swala lolote ndani ya bunge akiwa anatimiza wajibu wake wa kikatiba.

‘’Sikuwa na soma ripoti yangu wala kuwasilisha maoni yangu, nilikuwa nawasilisha ripoti ya kamati ya kudumu ya bunge kwa hiyo si sahihi kulihusisha swala lile na mambo binafsi’’ inasema taarifa ya Zitto Kabwe.

‘’Mpaka wakati nawasilisha taarifa ya kamati bungeni, sikuwa nimewahi kupokea hicho wanachosema ni shitaka lao kwangu, kwa kuwa tumesoma ripoti mwezi November mwaka 2014 na nimeletewa shitaka lao mwezi mei mwaka 2015, kwa hiyo sikuwa na mgogoro wowote wa kimaslahi kama wanavyotaka kuuaminisha umma’’. Iliongeza taarifa ya mbunge huyo.

Zitto aliongeza zaidi kwa kusema kwamba mpaka sasa hajapokea taarifa ya kimahakama ikimzuia kutokujadili hoja inayohusiana na yeyeb kujadili jambo linahusiana na IPTL/PAP na badala yake amepokea taarifa ya kesi ya madai ya fedha na hivyo haki zake za kutumia katiba kujadili maswala ya kitaifa ndani ya bunge zipo pale pale na kwamba ataendelea kuwawakilisha watanzania kwa kusimamia rasilimali za taifa.

Sakata la IPTL na akaunti ya ESCROW lilibua hisia mbali mbali wakati wa mjadala wake uliodumu kwa zaidi ya miezi saba mwaka juzi na kuhitimishwa mapema January mwaka jana baada ya Waziri Muhongo kujiuzulu

Chanzo: Gazeti la Jamvi La Habari
 
Attachments

  • IMG-20160125-WA0009.jpg
    IMG-20160125-WA0009.jpg
    202.3 KB · Views: 76
  • IMG-20160125-WA0009.jpg
    IMG-20160125-WA0009.jpg
    202.3 KB · Views: 55
SAKATA LA ESCROW LAIBUKA UPYA

MAGUFULI MKAMATE SETHI WA IPTL

Wasomi wataka wabunge wamalizane na kiporo cha SETHI

IPTL/PAP yawazuia wabunge kuliibua upya suala hilo

‘’Sikuwa na soma ripoti yangu wala kuwasilisha maoni yangu, nilikuwa nawasilisha ripoti ya kamati ya kudumu ya bunge kwa hiyo si sahihi kulihusisha swala lile na mambo binafsi’’inasema taarifa ya Zitto Kabwe

‘’Mpaka wakati nawasilisha taarifa ya kamati bungeni, sikuwa nimewahi kupokea hicho wanachosema ni shitaka lao kwangu, kwa kuwa tumesoma ripoti mwezi November mwaka 2014 na nimeletewa shitaka lao mwezi mei mwaka 2015, kwa hiyo sikuwa na mgogoro wowote wa kimaslahi kama wanavyotaka kuuaminisha umma’’. Iliongeza taarifa ya mbunge huyo.

Zitto aliongeza zaidi kwa kusema kwamba mpaka sasa hajapokea taarifa ya kimahakama ikimzuia kutokujadili hoja inayohusiana na yeyeb kujadili jambo linahusiana na IPTL/PAP na badala yake amepokea taarifa ya kesi ya madai ya fedha na hivyo haki zake za kutumia katiba kujadili maswala ya kitaifa ndani ya bunge zipo pale pale na kwamba ataendelea kuwawakilisha watanzania kwa kusimamia rasilimali za taifa.

Sakata la IPTL na akaunti ya ESCROW lilibua hisia mbali mbali wakati wa mjadala wake uliodumu kwa zaidi ya miezi saba mwaka juzi na kuhitimishwa mapema January mwaka jana baada ya Waziri Muhongo kujiuzulu

Source :- GAZETI JAMVI LA HABARI
Thubuutuuuu
 
Thubutuuuuu! Nani amkamate Seth. Singa singa huyo ni jipu uchungu limekaa pabaya. Si rahisi kutumbuliwa na hivyo linahitaji mtu jasiri anayeweza kufanya eperation (kulipasua jiupu hilo) ambayo inahusisha kukata kata baadhi ya vioungo. Sidhani kama mtu wa kufanya upasuaji huo ni JPJM.

Tusubiri tuone!
 
Tusubiri tuone![/QUOTE
Seth ni jipu la sikioni linahitaji oparation na mtumbuaji awe ni specialist siyo Jpm mkurupukaji?
 
Simuoni mkulu JPM kama ana jeuri hiyo ya kumchimba na kumharibia aliyempisha ofisi. Akigusa tu, ajue na Richmond, meremeta, epa na nyinginezo zitaamshwa zilikolala. Na hapo ndipo USO wa utawala wake utajidhihirisha wazi kuwa ni wa kulipa kisasi.
Hata hivyo aliishafungwa mdomo na mikono na huenda akavalishwa miwani ya mbao asiuone ufisadi mwingine.
 
Huu mfumo wa SSM ndo unaopelekea waliotuhumiwa na kuhukumiwa na bungu juu ya sakata Tegeta Escrow kuendelea kuteuliwa kwenye nyazifa kadhaa serikalini.

Hii inamaabisha kwamba maamuzi ya Bunge si chochote dhidi ya Escrow. Na hili litaendelea mpaka kampuni hiyo itakapofilisika yenyewe, kuondoka nchini ama mmiliki kupoteza viashiria vya uhai.

By the way, wabunge watarudi kuimbisha tena huu wimbo wa ESCROW, wananchi tutaendelea kisikiliza kwa makini huku tukiona the featured artist "sirikali" akiendelea kuimba kwa sauti ya chinix2 kama dharau kwa hadhira ya watz.

Tupo!
 
Thubutu yake!!! Sio tu kumkamata, hata kumsogelea hawezi. Anachoweza ni kubomoa nyumba za walalahoi...
 
Thubutuuuuu! Nani amkamate Seth. Singa singa huyo ni jipu uchungu limekaa pabaya. Si rahisi kutumbuliwa na hivyo linahitaji mtu jasiri anayeweza kufanya eperation (kulipasua jiupu hilo) ambayo inahusisha kukata kata baadhi ya vioungo. Sidhani kama mtu wa kufanya upasuaji huo ni JPJM.

Tusubiri tuone!
Kusema kweli hata ajigambe vipi kuna majibu hawezi kuyatumbua. Soon tutamsikia akilia lia bila kufanya lolote.
 
Jpm kasema atayatumbua yote mpaka yaishe yote hayo yamekaa foleni
Naamini foleni yake ikifika atalitumbua tu.
 
Wasomi wataka wabunge wamalizane na kiporo cha SETHI

IPTL/PAP yawazuia wabunge kuliibua upya suala hilo.

Yadaiwa kutumia Mahakama kujikinga dhidi ya maamuzi ya Bunge

Yamtumia Rais Mstaafu Kikwete kujitetea wasifilisiwe

Yamshitaki Zitto Kabwe Mahakama Kuu

Zitto Mwenyewe ajibu mapigo

Waziri Muhongo atakiwa kukaa upande wa Umma sio SETHI

Na Mwandishi Wetu.

JUMUIA ya Wanazuoni Watetezi wa Rasilimali nchini (JUWARA), imewataka wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania linalotarajia kuanza rasmi vikao vyake vya kujadili hotuba ya Rais aliyoitoa wakati wa kulizindua bunge hilo hapo kesho, kumuomba na kumkumbusha Rais DK. John Pombe Magufuli kutoa agizo la kukamatwa mara moja kwa mfanyabiashara Harbinder Sing Sethi ambaye ni mmiliki wa kampuni ya IPTL/PAP inayoendesha mtambo wa kufua umeme wa dharura uliopo tegeta Salasala kama sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge lililopita .

Wanazuoni hao wamesema kuna kila sababu ya wabunge wa bunge hili la 11 kusimama imara ili kutetea rasilimali za taifa letu zinazoonekana kutafunwa na wajanja wachache wanaotumia visingizio dhaifu vya sheria na uwekezaji kwa kumtaka Rais John Magufuli aharakishe utekelezwaji wa maazimio hayo ya Bunge hasa azimio namba moja lililoitaka serikali kumchukulia hatua kali na kumkamata mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Herbinder Sing Seth kwa makosa ya kulisababishia taifa hasara ya zaidi ya bilioni 320 kutokana na wizi uliofanyika katika akaunti ya TEGETA ESCROW.

Pia, jumuia hiyo imesema ina imani kubwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo huku ikimtaka awe mwangalifu na asiwe mtetezi wa IPTL safari hii kwa kuwa maamuzi ya bunge yalikuwa sahihi dhidi ya kampuni hiyo, ambayo imeisababishia hasara kubwa serikali kutokana na vitendo vyake vilivyofanya.

Wakizungumza na JAMVI LA HABARI, Mwenyekiti na Katibu wa Jumuia hiyo, Omary Kisambu na Mahmud Salibaba kila mmoja,w ameonyesha kusikitishwa na kitendo cha serikali kumkumbatia mfanyabiashara huyo, anayelalamikiwa na watanzania wengi kwa kulitia hasara taifa kutokana na vitendo vyake alivyovifanya kwenye sakata nzima la akaunti ya Tegeta Escrow.

"Tunashangaa mpaka sasa mapendekezo na maazimio muhimu ya Bunge kuhusu TEGETA ESCROW hayajatekelezwa na badala yake wameishia kuwatoa kafala kina William Ngeleja na Anna Tibaijuka, hii haitakiwi kuachwa ipite hivi hivi, lazima kama vijana wasomi tusimame kidete kupigania taifa letu na rasilimali zake" alisema Mwenyekiti huyo.

Naye, Katibu wa Elimu na Mawasiliano wa Jumuia hiyo, Mahmud Salibaba amelinukuu azimio namba moja na kushangaa kuona serikali imekubali kutekeleza azimio namba nane wakaliacha azimio namba moja ambalo linahitaji utekelezaji tu.

Mahmud aliongeza kuwa azimio namba moja linasema

"Bwana Harbinder Singh Seth na wengine,Bunge linaazimia kwamba, TAKUKURU, Jeshi la Polisi na Vyombo vingine husika vya Ulinzi na Usalama, vichukue hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, dhidi ya watu wote waliotajwa na Taarifa Maalumu ya Kamati, kuhusika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na Miamala ya Akaunti ya Escrow, na watu wengine watakaogundulika kufuatia uchunguzi mbalimbali unaoendelea kuhusika katika vitendo vya jinai". Aliinukuu.

Katibu huyo, alisema "Hatuna wasiwasi na Prof. muhongo, Tunaamini ana mapenzi mema na utayari wa kulitumikia taifa katika sekta hii, lakini kwenye hili tunamtaka aweke mbele maslahi ya Taifa na kamwe asigeuke kuwa mtetezi wa IPTL wala Sethi".

Wanazuoni hao wameendelea kuonyesha matumaini yao kwa Bunge hili huku wakiamini kwamba kama ilivyo kawaida ya mabunge yaliyotangulia, panapotokea masuala ya kitaifa yenye maslahi mapana kwa nchi basi wabunge wav yama vyote huungana na kuweka tofauti zao pembeni na kulisimamia taifa liokoe rasilimali zake.

IPTL/PAP YAMZUIA ZITTO KABWE KUZUNGUMZIA.

Wakati hayo yakiendelea, kampuni hiyo inayolalamikiwa kuingizia hasara ya mabilioni serikali na kupelekea kuwajibishwa kwa watumishi kadhaa wa umma, imejitokeza na kuwataka wabunge waache kulizungumzia suala hilo kwa kuwa bado lipo mahakamani.

Katika taarifa iliyosambazwa kama tangazo iliyosainiwa na Katibu na Mshauri mkuu wa sheria wa Kampuni hiyo, Joseph Makandege, imemtaka Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto kutokuendelea kulizungumzia suala hilo na kwamba aache mpango wake wa kutaka kulifufua upya suala hilo hasa bungeni kwa kuwa tayari kampuni hiyo imeshamshitaki katika kesi ya madai iliyopo mahakama kuu na kwamba haitakuwa busara kwa mbunge huyo kulizungumzia suala hilo ambalo yeye binafsi ana maslahi nalo.

Kadharika taarifa hiyo inasema kwamba tayari serikali imejibu kupitia hotuba ya Rais mstaafu Jakaya kikwete pindi alipokuwa madarakani kuwa haipo tayari kumkamata Sethi wala kutaifisha mitambo hiyo kwa kuwa itasababisha kuanzishwa kwa mahusiano mabovu na wawekezaji, hivyo Makandege amesisitiza kwamba ni vema mbunge huyo na mbunge mwingine yoyote aachane na mpango wa kuliibua suala hilo bungeni. ‘’kwa uelewa wetu mdogo kuhusu maswala haya, kauli ya Rais huwa ndio kauli ya mwisho na ni sawa na hukumu, na tayari Rais (Rais Mstaafu Kikwete) alishasema kuwa suala hilo haliwezekani ‘’. Ilisisitiza taarifa hiyo ya Makandege.

‘’katika hali ya kiubinaadamu, si vema kwenda bungeni kushusha lawana na tuhuma kuwatuhumu watu na ama kampuni ambazo zenyewe haziwezi kuingia bungeni kujitetea’’. Ilisema sehemu ya taarifa hiyo

‘’hata mheshimiwa Zitto alifanya makosa kujihusisha na suala la IPTL/PAP wkati akijua kuwa ameshtakiwa mahakamani na kwamba moja kwa moja anakuwa na mgogoro wa kimaslahi, japo hajatamka mahala popote kuwa ana mgogoro wa kimaslahi na sakata husika’’. Iliongeza sehemu ya taarifa hiyo

ZITTO AWAJIBU

Naye mbunge wa Kigoma mjini ACT – WAZALENDO ambaye wakati wa mjadala wa sakata hilo la ESCROW alikuwa mwenyekiti wa kamati ya Bunge inayosimamia hesabu za serikali, amejibu taarifa hiyo kwa kusema ni ya uongo inayoambatana na uoga wa kuwajibishwa na bunge baada ya kugundua maovu yao na kwamba IPTL /PAP hawana mamlaka ya kisheria kumzuia mbunge kujadili swala lolote ndani ya bunge akiwa anatimiza wajibu wake wa kikatiba.

‘’Sikuwa na soma ripoti yangu wala kuwasilisha maoni yangu, nilikuwa nawasilisha ripoti ya kamati ya kudumu ya bunge kwa hiyo si sahihi kulihusisha swala lile na mambo binafsi’’ inasema taarifa ya Zitto Kabwe.

‘’Mpaka wakati nawasilisha taarifa ya kamati bungeni, sikuwa nimewahi kupokea hicho wanachosema ni shitaka lao kwangu, kwa kuwa tumesoma ripoti mwezi November mwaka 2014 na nimeletewa shitaka lao mwezi mei mwaka 2015, kwa hiyo sikuwa na mgogoro wowote wa kimaslahi kama wanavyotaka kuuaminisha umma’’. Iliongeza taarifa ya mbunge huyo.

Zitto aliongeza zaidi kwa kusema kwamba mpaka sasa hajapokea taarifa ya kimahakama ikimzuia kutokujadili hoja inayohusiana na yeyeb kujadili jambo linahusiana na IPTL/PAP na badala yake amepokea taarifa ya kesi ya madai ya fedha na hivyo haki zake za kutumia katiba kujadili maswala ya kitaifa ndani ya bunge zipo pale pale na kwamba ataendelea kuwawakilisha watanzania kwa kusimamia rasilimali za taifa.

Sakata la IPTL na akaunti ya ESCROW lilibua hisia mbali mbali wakati wa mjadala wake uliodumu kwa zaidi ya miezi saba mwaka juzi na kuhitimishwa mapema January mwaka jana baada ya Waziri Muhongo kujiuzulu

Chanzo: Gazeti la Jamvi La Habari
Waziri wa nishati na madini alilithibitishia bunge kuwa hazikua hela za umma. Sasa wamkamate huyo wa nini? Akikamatwa basi muhongo hana budi kujiuzuru tena maana atakua na kosa la kuudanganya umma
 
Hii sasa inaelekea kuwa cultural revolution ya Mwenyekiti Mao. Walete tu. Watakaojiharia ni wale wakoa manza!
 
Kuna Majipu hata afanyeje hawezi kuyagusa.Kuna Cancer ambayo akiigusa tu wote chali.Hakuna cha Escrow wala UDA.Ubavu Magu hana.
 
Hhahahah Mimi ngoja nicheke tu BT naamini mtukufu mwisho wake NI kukumata wakurugenzi tu huko hawezi kabisaaa
 
Back
Top Bottom