SAKATA LA DOWANS: Hivi Ajenda Hasa ni Nini?

SAKATA LA DOWANS: Hivi Ajenda Hasa ni Nini?

Mtu wa Mungu

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2010
Posts
444
Reaction score
19
WanaJF hivi focus ni kuzuia malipo ya Dowans, au ni pamoja na Kuondoa mzizi wa janga la taifa kuangamizwa na mafisadi?

Bila kuweka wazi dira katika masuala haya nyeti kwa maslahi ya taifa, matokeo yatakuwa ni malumbano endelevu, na kila kukicha mafisadi wanabuni mbinu mpya za kuendelea kulididimiza na hatimaye kuliteka na kulitawala taifa hili!

Hivi kweli tunaelewa nani hasa kinara, aliye nyuma ya masakata haya yote, ambayo kwa miaka sasa yamelitikisa taifa hili? Mara EPA, mara Meremeta, mara Kagoda, mara Richmond, mara SONGAS, mara Dowans, nk; na yote haya barabara zake zote zinaelekea kwenye chama tawala; na vinara wake, hata wale usioweza kuwatarajia wako kimyaaa!

Ni bora kumfahamu adui, vinginevyo itabaki wakati wote kuwa ni mchezo wa paka na panya!!!!!!!!!!!!!!!!! Taifa lisisahau kuwa siku zote majuto ni mjukuu!
 
That is made in Tanzania, they are good at speaking!!! for six years now we have been repeating same words regarding corruption. People are delusionals and fake patriot when it comes what do we need as a country, I do believe many Tanzanian s are doing dirty deals.
 
Kafulila alishaweka bayana kwamba endapo Dowans watalipwa faster-faster kabla ya mjadala wake haujafikishwa bungeni, ataomba kuwasilisha hoja binafsi ya kutokuwa na imani na serikali. Sasa swali ni je wakati hoja hiyo ikijadiliwa sisi wananchi tutakuwa tunafanya nini kuonyesha machungu yetu? Au ndo tutakuwa tukikodolea macho luninga tu basi? Tutoe mawazo yetu hapa ya namna ya ku-react. Nawasilisha!
 
halafu hii hoja ya Kafulila mi nina wasiwasi nayo. Kwa sababu kila saa spika akiuliza kuhusu hii hoja anasema kuwa kilichowasilishwa ni "nia ya kutoa hoja" na kwamba hoja yenyewe haijafika ofisini kwake.

Hiyo sentensi maana yake, jamaa anaweza kuzuiwa kuiongelea bungeni kwa sababu hajaifikisha ofisi kwa spika bado ili ipewe go ahead au la.
 
Mi ningeomba tutoe mawazo ya ni jinsi gani ya kuwafunga na kuwafilisi waliotuletea huu uozo ukiwazibia Dowans leo kesho au saa hizi huenda kuna deal nyingine wanafanya ya kutuibia
 
VAA NGUO NYEUSI AU FUNGA KITAMBAA CHEUSI 05-02-2011 kama ishara ya maombolezo ya janga linaloitwa CCM
 
Toa mawazo yako ili tuyajadili na kuona kama yanatufaa.
MwanaJF Magafu, tunahitaji vitendo, siyo maneno; taifa limepatikana!!!!!!!!!; wa kulinusuru ndiye tunamhitaji!!!!!!!!!!!!
Fisadis are very good at making up issues to keep Tanzanians busy pondering; finally nothing comes out!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Tatizo hapa si DOWANS au Kgoda AU Rostam !tatizo ni mfumo wa kijinga wa wajinga ulio tufikisha hapa .Tumekuwa Taifa la wajinga wasiohoji !tunashangilia ujinga jndio maana hata kina MAGUFULI WAKITEKELEZA mJUKUMU YAO YA kawaida tunaona kama vile wanafanya mabo ya ajabu ,tena wakiongozana na waandishi wa habari ,,,,hapo kwetu ni burudani kabisa!
 
Wakuu hawa fisadis wametushinda nguvu, simply because wanalelewa na CCM! Dawa ni kuing'oa hii kitu CCM wandugu! Sasa sijui tuanzie wapi maana wana-inji wanahangaika kutafuta mkate wa kila siku wala hawana habari kwamba siri ya matatizo yao mzizi wake ni CCM!
 
Iwapo serikali itamlipa Rostam fedha za walipa kodi tutafanya kama kile ambacho Waafrika wenzetu wa Tunisia na Egypt wamefanya. Enough is enough!
 
hawalipwi ,,,,mbona unaleta uchuro wewe!

Mbona huu siyo uchuro! Protest can be done in any way, this is the easiest way to protest against CCM's robbery of the poor. Let us send the message that we are not happy and mourning as they celebrate the birth of their corrupt party on 5 February
 
mzee mi naona hapa la kufanya ni kusaport bunge kwa kuandamana wakati hoja bungeni ikiendelea ili kuweza kulipa suala hili uzito, vinginevyo itakuwa kama Richimond tusipoonyesha hisia kwa vitendo. watanzania tuamke jamani tuwape moyo watetezi wetu
 
wakilipwa na mimi nabadili ka kuwa mhindi au mwarabu ili na mimi niwe na haki ya kuiba mali ya tanzania.
 
WanaJF hivi focus ni kuzuia malipo ya Dowans, au ni pamoja na Kuondoa mzizi wa janga la taifa kuangamizwa na mafisadi?

Bila kuweka wazi dira katika masuala haya nyeti kwa maslahi ya taifa, matokeo yatakuwa ni malumbano endelevu, na kila kukicha mafisadi wanabuni mbinu mpya za kuendelea kulididimiza na hatimaye kuliteka na kulitawala taifa hili!

Hivi kweli tunaelewa nani hasa kinara, aliye nyuma ya masakata haya yote, ambayo kwa miaka sasa yamelitikisa taifa hili? Mara EPA, mara Meremeta, mara Kagoda, mara Richmond, mara SONGAS, mara Dowans, nk; na yote haya barabara zake zote zinaelekea kwenye chama tawala; na vinara wake, hata wale usioweza kuwatarajia wako kimyaaa!

Ni bora kumfahamu adui, vinginevyo itabaki wakati wote kuwa ni mchezo wa paka na panya!!!!!!!!!!!!!!!!! Taifa lisisahau kuwa siku zote majuto ni mjukuu!

Umeuliza swali nyeti sana,"hivi kweli tunamfahamu adui?"Katika ujinga wetu tunadhani adui ni mafisadi,CCM au hata serikali ya CCM.No, that is far from the truth.The enemy yuko pembeni kabisa ametulia.And since we do not take any effort to identify the enemy,he is finishing us off queitely!
 
Kwa tafakari ya kawaida kabisa, huu ni mpango wa kuwasafisha wale ambao walichafuka katika sakata la ununuzi wa mitambo ya richmond ambayo dowans walirithi. Kilichopo sasa nikutafuta namna ambayo hiyo mitambo itachukuliwa na serikali kwa blanketi la kupunguza makari ya umeme ambayo wametangaza kuwa yatadumu kwa mwaka mzima sasa. Kunawatu wanapaswa kuwajibishwa
 
Back
Top Bottom