Ujamaa ni laana mkuu.Hizo ndizo akili za CCM kila level.Huyu anaweza kuwa mtu mkubwa sana ccm,sasa anafanya propaganda ili wakimwomba wasema kanywea. Si unakumbuka Magu akiwa ktk ujenzi,watu walikataa kuendelea na kazi akaowamba wachina na wazawa,aliporudi bungeni akapaza sauti sana.Kwamba wamelipwa wote na asiyetaka anapigwa chini.Mwezi tuu baadae akarudi ktk mkutano na wakandarasi wa ndani akawaomba na kulipa kiduchu huku watu wakilia. Hawa ndio wajamaa wanapenda kufa na suti shingoni bila sababu.Mtoa Mada Kwa Swali Hili.
Kweli Watanzania wengi ni Villaza.
Biashara siku zote kama Haikulipi Unafunga na yeye Dangote ndiyo Mwenyewe Kiwanda Akiamua Kufunga Hakuna wa Kumzuia.
Hakika kiwanda cha Dangote ni jipu kubwa kama IPTL au ESCROW account. Mkulu asipokaza buti hataweza kulitumbua. Kelele kubwa tunazozisikia ni za wapambe wa wenye maslahi ambao wana mikono kama ya pweza kwani wapo kwenye shughuli zote kubwa za kiuchumi za nchi hii. Kwenye vitalu vya gesi wapo, vitalu vya urani wapo, IPTL wapo, Bandarini wapo. Kwa kifupi wanamwonya mkulu asitake kukata mkono unaomlisha. Yetu sisi nyasi ni maumivu au kwa lugha ya kisasa ni kuisoma namba.Tumpe ushirikiano JPM,mchwa ni wengi sana
Hilo ni kovu kubwa na baka lisilo tazamwa mara mbili!! kutaifisha ni WIZI na unyanganyi Mtupu.. !! Hadi leo halijasahauliwa... na halitosahauliwa !!!Busara inatakiwa itumike maana Tajiri bilionea tena wa kimataifa kama Dangote akifunga biashara zake ina maana wawekezaji karibu wote duniani watatishika sana na hali ya uwekezaji nchini.Tena wakikumbuka na utaifishwaji uliotokea baada ya Azimio la Arusha,taswira ya Tanzania inaweza kuchafuka vibaya sana kimataifa.
Kwan atafunga milele...anafunga kwa miaka 9 akija rais mwingune anayeelewa mambo ya uwekezaji wataongea terms upya atafungua
Mkuu Tunakuelewa ila tumia neno la upole. Duh! "Kichaa"Kwa taarifa yako Dunia inaongozwa na biashara siyo viwanda.
Ndio maana mnalipa capacity charges kwa IPTL bila kupata hata unit moja ya umeme hiyo inaitwa biashara.
Serikali imepatwa ugonjwa wa kichaa
Tatizo kubwa ni kuwa bei ya gesi kwa Tanzania ni kubwa sana ukilinganisha na sehemu nyingine na hii inatokana na labda na mikataba ya uchimbaji pamoja na usafishaji wa gesi na hapo ndiyo tatizo lilipo
Dangote was also joining two other newcomers so this industry ipo vzur aende tuUtashangaa Kiwanda kikipakiwa kwenye Kontaina kwenda Angola.
Sina hakika kama umefatilia hili sakata vzuri au na ww ni moja Ya wanadhi wa wale wanasiasa wanaotumika na Dangote kutaifisha ile dhana ya Dangote kutumia rasilimali zetu Dangote anaagiza makaa Ya mawe kwa kisingizio kuwa Ya kwetu hayana ubora (ash content yake ni kubwa) hatukatai ila lipa kodi..last year aliagiza gypsum na hakulipa kodi this year TRA walizua meli Yake pale bandar ilikuwa na gypsum pia from Oman wakati lindi ipo na anadeni kama la 1billion la VAT (sina hakika kama kalipa)...sasa unawekeza kwenye cement hununui limestone from lindi wala makaa ya mawe from Ngaka wakat Tayar ana contract na Tancoal waproduce coal almost 13500 Tonnes a year unataka bado kuwekeza kwetu wa nn ? unamsaada gani ?Mbona unawaza kitoto sana yaani unafurahia dangote kufungwa?