Sakata la Dangote kaa la moto

Kabisa mkuu, kama jamaa ameshindwa ku sustain loss basi nchi hii siyo salama kuwekeza, utaliwa kichwa mwisho wa siku
 
Michezo hii ya kijinga kutafuta kumkomoa fulani ndiyo iliifanya Tanesco kulipa mabilioni mengi IPTL
 
Bandiko lako ungejiuliza kwanini kama anapata faida kwanini atake kufunga?...

Yaani mnajipanga mpate nyie faida mwekezaji apata hasara kweli tumeingia chaka sana .....

Serikali hata ikiambulia faida ya watanzania kuajiriwa ikapata kodi kwa wafanyakazi hiyo inatosha......

Sijui mnataka faida gani zaidi....
 

Pamoja na hayo yote.Hizi kambi mbili moja iliyoko ndani ya serikali ya Magufuli na Kambi ya Pili iliyokuwa katika serikali ya awamu ya nne WALIONUNUA HISA nyingi ndo TATIZO.

Kama wananchi hatutakubali hizi kambi ZITUHARIBIE uchumi wetu wa viwanda! Katika mtazamo wa kindani. KUNA BEHIND the scenes FORCES/ Msukumo ULIOJIFICHA unaoipa Dangote Cement KIBURI na kutaka KUi Blackmail serikali kwa kuupindisha mkono kwa nguvu ili serikali isikie MAUMIVU na iseme YAISHE.


Dangote Cement can't dictate to the government terms and conditions as per their demands. Kuna MKONO MKUBWA nyuma ya hii SAGA/Jambo na ndio huo unaoipa KIBURI kampuni hii.Hilo ndo watanzania tulijadili na tujiulize.Ni MKONO wa AKINA nani??
Magufuli ASILINYAMAZIE!!!
 
Washauri wakuu wanatakiwa walitafakari sana jambo hili. Wawe makini, ni doa kubwa, na siombei jambo hilo litokee, naamini muafaka utapatikana.
 
Lazima kuna kitu katikati ......ngoja tusubiri tuone.
 
Afunge kiwanda asifunge ni maamuzi yake mwenyewe.

Mwekezaji yoyote ni lazima afuate taratibu za nchi yetu na siyo matakwa yake.

Alipoamua kuja Tanzania kuwekeza ni kuwa alifahamu kuwa toka ujenzi mpaka uzalishaji utaratibu utakuwaje wa biashara yake.

Na akienda kinyume na makubaliano na kazi ya Serikali kulinda maslahi ya nchi na mwanainchi wake.

Hakuna mwekezaji yoyote aliyejuu ya Serikali,wawekezaji wamewekewa mazingira wezeshi ya kufanya biashara zao na Serikali itahakikisha usalama wa wawekezaji na biashara lakini kwa kufuata makubaliano na sheria na nchi.
 
Huyu muwekezaji kama angekua mzungu sidhani kama mambo yangekua hivi Ila kwa kua ni mswahili mwenzetu ndio anawekewa zengwe, nadhani anajuta kuwekeza Tz.
 
N
Dr.Kafumu nadhani amehoji maswali ya msing yanayohitaji majibu ilikupata undani wa tatizo.
Je kwa wenzetu bei ikoje?
Na anaijua vizuri dangote!! Mpaka anahisi inamikataba ya kuchukua makaa ya mawe nje! Just curious.
 
Akili za kipuuzi kwelikweli, kwani yeye si ndiyo alikijenga, iweje ashindwe kukifunga kama hakimlipi.


Kwa hiyo mna muwekea vikwazo mkidhani hatoweza kukifunga??


Wahed!
Tanzania ni tajiri kweli kweli mwache aende na sementi yake wako wengi wanakuja kuwekeza wanasubiri tu
 
yaani tunaua kiwanda kwa sababu ya kuwakomoa wanasiasa fulani?
Kama ni kweli na sio maneno ya kisiasa. Basi serikali haipo sahihi.
Kama tajiri mkubwa kama dangote akishindwa kufanya uwekezaji na kuendeleza kiwanda cha cement tu, basi wawekezaji wengine hasa wageni wataogopa zaidi. Dangote ni kioo Africa nzima inamuangalia
 
Na anaijua vizuri dangote!! Mpaka anahisi inamikataba ya kuchukua makaa ya mawe nje! Just curious.


Usiulize majibu.

Maelezo binafsi ya mgombea wa CCM jimbo la Igunga Dk. Kafumu ...
3 Sep 2011
UTUMISHI WA UMMA
*Kamishna wa Madini Tanzania (2006-2011)
*Mkuu wa Mawasiliano Wizara ya Nishati na Mdini (2004-2006)
*Mkuu wa Kitengo cha Uhamasishaji na Takwimu Wizara ya Nishati na Madini (2002-2004).
*Mtaalam Mwandamizi wa Madini (1993-2002)
*Mhadhiri Chuo cha Mdini Dodoma (1978-1992)
*Mtaalam wa Madini Wizara ya Nishati na Madini (1983-1987).
 
Siasa vs biashara
Hapa tz mfuko tungeuziwa tsh 8000 ila wanasiasa ndo wametufikisha hapa
 
Sasa jaman kuna biashara yoyote duniani inaeza kuendeshwa kwa hasara?hata kma ndio biashara yako kbwa?utafunga tu! Haijalishi kiwanda au kampuni ameona haimlipi kwa nn asifunge?
 
Tujiulize ni watanzania wangapi ajira Zao zipo shakani, Pia kwa mwezi huu tutapoteza kodi kiasi gani? Na je hao tunaohisi wana maslahi je kuna hela waliiba serekalini (Ila hii kwa sasa sio issue)
 
Mhe Rais Magufuli inabidii uwajibishe Waziri wa Nishati na madini pamoja na Waziri wa viwanda na biashara kwa kulea mgogoro huu na mwekezaji inakuwaje leo mtu amewekeza halafu unataka kumletea mizengwe. Dangote alikuwa mkombozi wa watanzania leo kanda ya ziwa cement ilishuka mpaka 15000 kutoka 20000.
Waziri wa Nishati atueleze watanzania tunafaidika nini na haya madini yanayochukuliwa kila siku badala ya kumwekea masharti mtu aliyekuja na pesa zake kuwekeza hapa Tanzania kwa manufaa ya watanzania.
Rais Magufuli chukua hatua za haraka kama unataka Tanzania iwe nchi ya viwanda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…