Saikolojia ya Rais Samia inaonesha hofu badala ya ujasiri au matambo

BICHWA KOMWE -

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2022
Posts
7,969
Reaction score
20,013
Sifahamu kama aliyoyasema leo kwenye mkutano wa wazee wa dar ameandikiwa ama ameyatoa kichwani mwake?

Kwa vyovyote vile inaonekana aliyafanyia mazoezi ya siku kadhaa kabla ya kuzungumza.

Kwa sisi wenye "jicho la tatu" ni rahisi sana kubaini hofu iliyopo katika matamshi yake.

Kwa juu inaonekana kama vile anatamba kwa ujasiri, lakini kwa ndani hakuna lolote kati ya hayo.

Mjongeo wa mwili wake, kushuka na kupanda kwa sauti yake, mgongano kidogo wa matamshi, kusita sita kwa sauti na kutoa hotuba kwa namna ya kuuliza maswali kama vile "sasa mlitaka sisi tufanyeje", hayo yote yanaakisi hofu na wasiwasi mkubwa ndani mwake.

Kule kuonekana kujitutumua na kushika kiuno kunazidi kutia mashaka kuhusu ujasiri wake.

Ujasiri una sura yake. Sijaiona kwenye hotuba ile.

Labda pengine tumuombee samia. Tusali azidi kuwa na hekima zaidi. 👁
 
Yea, sisi wataalam wa body language tumeona hili anaongea kwa hofu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…