SAIKOLOJIA: Wema wa mwanzo hufunikwa na ubaya wa mwisho. (Mfahamu Dr. Fitz Haber mshindi wa Nobel prize 1918)

OK,thanks more
 
unapenda uandishi lakini uandishi haukupendi mkuu.

sijasoma hadi mwisho.

kichwa cha habari cha kuvutia ila mpangilio mbovu.

wala haina maneno ya kumshawishi mtu kusoma hadi mwisho!
Duuh watu kama nyie ni masikini
 
Asante
 
Hapana.

Fritz Haber hakugundua gesi ya chlorine.

Gesi ya chlorine iligunduliwa kitambo sana kabla hata uyo Haber hajazaliwa.

Ila yeye alikuwa mtu wa kwanza kuitumia kama chemical weapon.
Uko sahihi
 
Ukweli ni kwamba hakuna mwema wala mbaya bali kuna mtenda na mtendwa na kila mtu anakuwa na maono yake juu ya mwengine.
Maono hayo ni Mbaya na Mwema.

Mfano tuseme mwizi anakuja nyumbani kwako kwa nia ya kukutoa uhai wewe na familia yako lakini badala yake wewe unamuwahi kwa kumuua yeye.
Je hapo nani ni mbaya na nani mwema? aliyeua au aliyeuliwa?

Wewe utamuona mwizi ni mbaya sababu alitaka kukuua na mwizi atakuona wewe ndio mbaya sababu umemuua.
Na kama ungejitia wema kwamba unayemuona leo adui kesho anaweza kukusaidia, na humjui atakae kusaidia kesho.
basi hapo ungekufa wewe mbele ya huyo adui (mwizi).

Mfano mwengine mzuri
Tuseme mimi ninapoishi nimeweka balbu nyuma ya nyumba ambapo kuna dirisha langu lakini kuna majirani wanakuja kufuata taa ile kwa ajili ya kufanyia mambo yao.
Lakini wakikaa hapo wanaanza kupiga kelele na kuweka radio zao na kupiga mziki mpaka saa 5.
Hivyo mimi nashindwa kusoma, kulala na kufanya mambo yangu mengine sababu ya kelele na fujo zao hivyo nazima ile taa.

Kinachotokea mimi wananiona mbaya mwenye roho mbaya kwa kuzima taa na mimi nawaona wao ndio wabaya sababu wanapiga kelele bila kujali kuhusu mimi?
OK so nani mbaya hapo mkuu?

Duniani na kwenye maisha hakuna guarantee kwamba ukifanya kitu fulani na kuwa fulani basi matokeo lazima yawe kitu fulani, Hakuna.
Bali wabaya watalipwa mabaya na wema watalipwa mema na huo ndio ukweli, hakuna mwanzo wala mwisho wa hayo mambo mawili.

Utalipwa kwa kile unachokifanya na utalipa kwa kile unachofanyiwa.
Ukifanya vinginevyo basi bila shaka utaishi kwa tabu na bila shaka utakuwa hauko sawa kama binadamu.
Na hicho ndicho kilichotokea hapo kwenye hiyo story yako.

Kuepusha yote hayo ni kila mtu ajitambue na ashikike nafasi yake yeye kama binadamu kamili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…