Saikolojia: Namna ya kutambua tabia ya mtu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Saikolojia: Namna ya kutambua tabia ya mtu

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by MziziMkavu, Sep 18, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Hakuna anayependa kusahihishwa, kugombana au kukemewa mbele za watu, hii ndiyo tabia ya watu wajeuri na walio na tabia za kitukutu. Mara nyingine hudhani wanapata sifa. Wako watu wa jinsi hii ambao hawawezi kukugombeza au (kukupa vidonge vyako) mkiwa wawili peke yenu, watangoja watu wengine wawepo ndiyo waanze kubwabwaja, cha kufanya jiepushe nao.

  Kwa kule kukimbiwa na marafiki, na kuwa mpweke, huongeza tabia za kitukutu na kijeuri na hii huwafanya watu hawa kutambulika haraka na kiurahisi zaidi.

  Zifuatazo ni alama zitakazokutambulisha mtu jeuri na mtukutu:

  a) Alama za kimaneno
  Mara kwa mara hupendelea kusema maneno haya vinywani mwao.
  Nakwambia bora unge"
  Wewe sichochote, silolote"
  Nakwambia, lazima u..."
  Fanya vile ninavyokuambia mimi"
  Nataka u..."
  Wewe endelea tu tutaona..."

  b) Alama za kimwili
  Hupendelea kusimama wima
  Huwa wenye pozi kavu, ngumu (still and rigid pause)
  Hupenda kukunja mikono
  Hupenda kupayuka au kupigia wengine kelele
  Hupenda kuwanyooshea wengine vidole.
  Hupenda kuwazodoa wengine na vidole (hawezi kukuelekeza hadi kidole chake kikusukume)
  Hupenda kupiga au kugonga meza na viti akizungumza

  2. Watu wapole, waliotayari kukubali kushuka (Submissive)
  Hawa ni watu wanaopenda kujitoa sadaka kwa ajili ya manufaa ya wengine. Kwa hali hii ni rahisi watu hawa kujikuta wanatumiwa vibaya na watu wengine hasa wale wajeuri na watukutu tulio waangalia awali.

  Mara nyingi watu walio wapole na wanaokubali kushuka hupenda kuwatia moyo wengine wawe kama wao. Katika vizazi vilivyopita, wanawake walitegemewa zaidi kuwa watu wa kundi hili. Ni mabadiliko ya maisha na ya jamii ya leo ambayo yamemfanya hata mwanamke kuwa mjeuri na mshindani tofauti na jamii za awali.

  Kwa upande mwingine mfumo wa maisha wa vizazi vya nyuma ulimweka chini mwanamke na kuzuia maendeleo yake hasa katika kujiendelezea vipawa alivyonavyo kwa vigezo tu kwamba yeye ni wakukubali chochote na wakati wowote sasa tunayaona mabadiliko kwa kiasi fulani.

  Mara kwa mara watu wapole, na waliotayari kushuka wamekuwa wenye hisia za kinyonge na kutengwa, wakijihisi kutokuwa salama wakati mwingi. Kujijali, kujipenda na kujithamini kwa watu hawa siyo kwa kudumu, bali kunakuwa na nyakati za kuyumbayumba kutokana na mazingira. Hawa siyo watu wenye ujasiri ndani yao wenyewe na hata katika vile wavifanyavyo.

  Mara mtu wa kundi hili anapokutana na mtu mjeuri na mtukutu, hofu na ujasiri wake hupungua sana, na anaweza kukubali kupingwa hata kama alikuwa ana haki. Kwa sababu mara nyingi watu wa jinsi hii wanajua kuwa kwa upole wao watu wengi wamekuwa wakiwatumia na kuwachezea, hii imewafanya wawe ni watu wenye vihasira vya mara kwa mara.

  Kwa sababu wameunganishwa na hisia zao zaidi, ni rahisi wao kuzielezea hisia zao kwa mtu mwingine, hata kama hisia zao ni za kujutia kile walicho kifanya wenyewe. Mara nyingi husikia amani kwa yale wanayofanya au kuyaamua.

  Ingawa mara nyingine mambo huwaendela tofauti na walivyopanga, watu hawa hufahamu kuwa hawanabudi kukubali kosa au na kuwa tayari kujifunza kutokana na yale makosa.

  Mambo yanapowaendea vema hupenda kujisifia na kujiona walio juu. Mara nyingine misimamo yao huwashawishi na kuwavutia wengine watazame kama wao, sio watu wanaopenda kuwatumia wengine vibaya (being manipulative) kama vile kuwasema au kuwasengenya wengine, hii huwafanya kuwa na wafuasi au washabiki wengi zaidi.

  Kule kujiamini kwao na kuwa na ujasiri hupunguza sana msongo wa mawazo maishani mwao na hii huwasaidia kuelekeza nishati na nguvu zao zote katika kufikia malengo waliojiwekea.

  Mara kwa mara sio watu wenye mabadiliko ya hisia (change of attitude) na hii hufanya mahusiano yao na wengine kuwa yasiyoyumba na mawasiliano baina yao na wengine huwa wazi, sio watu wakuficha wanachokiona, uwazi walionao kuwaweka huru.

  Hujisikia vema hujipenda na kujithamini muda mwingi. Hujijengea hisia za usalama na imani kwa sababu ya mawasiliano bora walionayo na wale wanaowazunguka, hii pia husababishwa na wao kuelewa fika wajibu wao na wajibu wa wengine pia.

  Ingawa wanaweza kuwa wabishi, lakini huheshimu misimamo ya wengine na kupenda ya kwao iheshimiwe pia na hii huwafanya kuwa na ushirika na wale wanaowazunguka. Mara nyingi ni wazuri katika kuwatia wengine moyo kujitahidi zaidi.

  Alam za kuwatambua:

  Alama za maneno
  Nahisi Najisikia kuu
  Ningependa kuu
  Wewe unaonaje hapa/mawazo yako nini
  Unadhani njia gani bora kulishuhulikia hili
  Nafikiri
  Hembu tu

  Alama za kimwili
  Hupenda kuwa wima ila wenye pozi laini (relaxed stance)
  Huangalia kijasiri na kuangalia usoni (kukodoa macho).
  Huwa na hisia za upole, kujitawala na kujimiliki wenyewe

  Kwa vyovyote vile, mara zote unapokutana na mtu mwenye tabia yeyote kati ya hizi tatu kumbuka una haki ya kufanya yafuatayo;

  Jifunze kuelezea hisia zako njema (usiogopoe au kuona aibu kwakuwa hutokuwa umejitendea haki)
  Jifunze kuzielezea hisia zako mbaya au za hasira, kamwe usifunike. Mfano; "Sipendi kabisa unavyokula"
  Jifunze kusema hapana, Mfano; "Hapana sitaweza kufika leo"

  Toa wazo la kweli, usipake watu mafuta kwa mgongo wa chupa. Mfano; "Mimi siliafiki hilo jambo hata kidogo"
  Kiri kuwa umekasirika, hasa pale ambapo haunabudi kukasirika.

  Mfano: "Kweli umeniudhi sana baada ya kusema hayo maneno". Usitoe tabasamu la mamba tu, kutabasamu wakati ndani yako unahisi kuungua moto.
   
 2. nipeukweli

  nipeukweli JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  naam...
   
 3. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #3
  Oct 6, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Nafikiri mimi ni haina ya mtu wa pili......
   
 4. majany

  majany JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2012
  Joined: Sep 30, 2008
  Messages: 1,199
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  mtu hawezi kuwa hybrid hapo kweli???
   
 5. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,672
  Trophy Points: 280
  Na hata bila hiyo saikolijia nadhani waweza tambua tabia ya mtu hata kwa mavazi yake,tembea yake n.k.
   
 6. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  mi niko kati kati ya makundi hayo ma2
   
 7. Root

  Root JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,146
  Likes Received: 12,853
  Trophy Points: 280
  Nilihama toka kundi la kwanza kwenda la pl

  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
 8. chumvichumvi

  chumvichumvi JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2012
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 1,050
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Mie nipo makundi yeyote inategemea na nyakati
   
 9. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,285
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  nitarudi baadaye kusoma,
   
 10. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,079
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  tabia ya mtu is never permanent hubadilika kutokana na mazingira na hali na watu anaoishi nao kwa wakati huo husika

  mf mtu anaweza akawa na hizi
  Alama za kimwili
  Hupendelea kusimama wima
  Huwa wenye pozi kavu, ngumu (still and rigid pause)
  Hupenda kukunja mikono

  lakini asiwe mtukutu wala mkorofi ila mchapakazi na ana mood ya serious wakati wote ila ukiongoea nae ni mtu mwenye maneno ya busara matamu na mtaratibu mno.
  human behaviour is very complex to explain n understand it.
   
 11. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,739
  Likes Received: 537
  Trophy Points: 280
  Je,utamgunduaje mtu anayepretend?
   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Hii ina apply kwa tamaduni zote kutoka stockbrokers wazungu wa NYSE, watu wa misitu ya Amazon, Congo na aborigines wa Papua NG na Australia huko?

  Tusije ku copy paste tamaduni za watu huko, ambazo kwao mtu kuongea na wewe huku anaangalia chini ni dalili ya uongo, wakati kwetu ni dalili ya heshima na haiba.
   
 13. Fyong'oxi

  Fyong'oxi JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na hii imekaaje ??, kwa wanaosema mtu mpole/asiyeongeaongea akipandwa na hasira ni mbaya kuliko mtu mkorofi
   
 14. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Mkuu kuna tofauti kubwa kati ya Mpole na Mkimya. Watu wengi wanapo mwona mtu mkimya wanamwita mpole, hao ni wau wawili tofauti.
   
 15. MSeush

  MSeush Member

  #15
  Nov 3, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Asante kwa somo lako nimejifunza kitu..
   
 16. THE BIG SHOW

  THE BIG SHOW JF-Expert Member

  #16
  Nov 14, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 13,925
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  MURUA KABISAA
  KARIBU SUPU YA SAMAKI MKUU
  SATO LAKINI
  :smile: :smile:
   
 17. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #17
  Dec 15, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,945
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  Na yote hii ni malezi utotoni.
   
 18. Patty B

  Patty B Member

  #18
  Dec 23, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Naam nimeipenda hiyo...!
   
 19. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #19
  Dec 24, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  sipendi watu kama wewe! Chit chat mtafanya nini sasa? Kwa nini ucopy habari ndefu hivyo aafu kamchango ka chit chat?
   
 20. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #20
  Dec 24, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,088
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  mi sitabiriki sipo katika makundi hayo yote labda mwana saikolojia atueleze kama kuna kundi jingine kwani mi ni kimya sana na pia sipendi kum comand mtu na pia sipendi mtu anikomand ukinizengua ntakuchenchia mpaka utajuta kunifaham, naweza kwambia maneno machace ila yakakuuma wiki nzima.
   
Loading...