Sijui kama kati yetu kuna mtu amepata kuisikia hyo ngoma yenyewe ya "KALINYE-KALINYE"?
Hahahahaha
Humo utamtambua Sygon, ni bonge la "Pin" alilipika Majani kipindi hcho 2005 kijana wakati kisharudi bongo toka UK, baada ya wapuuzi wengi kupakaza kuwa oh Sygon teja oh Sygon kadata oh sijui nini....
Kwa bahati mbaya sana hyo ngoma haikupata kupigwa kwenye redio nyingi (hasa ya wafu) hvyo haikuwa maarufu!
Magic Fm ndio waliipiga sana hasa kwenye kile kipindi cha Dj Mar-J kulikuwa na segment ya "NGUMU ZA BONGO" haikukaa sana hii segment sijui kwanini ila pale zilikuwa zinapigwa "Bongo hardcore hiphop" zile ngumu balaa, hata KALINYE-KALINYE ilikuwa ni track ngumu sana kwanzia beat hadi style nadhani Majani hakuifanyia Mixing sababu ilikuwa kavu sana,
ila kwa mtu mpenzi wa hiphop ngumu kama mimi KALINYE-KALINYE ni nyimbo tamu sana tena sana, naweza kusema miongoni mwa nyimbo kali za Sygon basi ile naiweka kwenye tatu bora!
KALINYE-KALINYE ni msemo wa mitaa ya kimasikini ukimaanisha kizazaa au heka-heka zitokanazo na rapsha fulani hivi mfano kama kitaa limetokea pila (yaani askari wenye difenda wamevamia maskani) katika masimulizi mtu atasema tu "jana hapa ilikuwa kalinye-kalinye", yaani palikuwa hapashikiki..... (tafsiri binafsi isiyo rasmi)
Hivyo katika hyo ngoma Sygon alikuwa anajaribu kuelezea KALINYE-KALINYE zinazoikumba dunia yaani nchi mbali mbali na hapa home Tanzania,
amezungumzia siasa ya kimataifa hasa current issues (kwa kipindi hicho)
na masuala mengine ya ki-music!
Mara ya mwisho mwaka juzi nilisikia stori kuwa Sygon yupo Iringa, kaoa mtoto mmoja wa kishua.......
Sikuthibitisha hizi taarifa!
Popote alipo namtakia maisha mazuri na yenye heri!