Saidi Arfi: Tunahitaji viongozi wenye hekima na busara kama mfalme Sulemani

Dec 21, 2012
96
15
Akiwa ktk kuchangia hoja juu ya bajeti ya wizara ya nishati na madini,mbunge wa mpanda mjini na makamu mwenyekiti wa Chadema taifa amesisitiza viongozi wa serikali kutumia hekima zaidi pamoja na busara ktk kutatua migogoro baina ya serikali na wananchi.Hakika huu si wkt wa serikali ya ccm kutumia nguvu na mabavu ya dola ktk kuwanyamazisha wananchi,kwani huko ni kuongeza chuki kati ya serikali na wananchi
 
Ameongea mpaka nimesikia machozi yananilenga kweli uongozi ni uadilifu na hekima bila hekima ya kiongozi mkuu yaani Raisi ataivuruga nchi na yeye atakuwa Raisi aliyechukiwa kuliko maraisi wetu wote tangu uhuru,nguvu haipaswi kutumika kwa wananchi wasio na silaha
 
Kisima cha busara kinajulikana pasi na kujitangaza,wenye akili wamesikia na wamekuelewa wasindikizaji watabaki kuzomea na kupiga mabench
 
Wazee kama hawa ndo inabidi Jk akachukue busara zao sio busura za kina nchemba na Nape Mzee kaonge kwa busara sana na adabu hadi roho inauma kwa nini walio madarakani wanashindwa kuwa na busara kama hizi..
 
TAIFA LETU TANZANIA LINALAZIMISHWA KUANGAMIA KWA MTAJI WA BAADHI YA VIONGOZI KUCHAGUA KUAHIRISHA MATUMIZI YA HEKIMA NA BUSARA NA KUKUMBATIA UBINAFSI MTINDO MMOJA KWA KILA HATUA KWA KILA KILICHO CHETU SOTE

Taifa la Tanzania tumejali karibia kila aina ya mema chini ya mbingu; tunalo taifa zuri, pana na tulivu kama tulivyorithishwa na Mungu Baba Mwenyezi;

Nasema, ndani ya Tanzania tumebahatika sehemu za bahari, ma-ziwa, mito mingine kuliko taifa lolote lile barani Africa. Haya yote ni mali na rasilmali yote tuliojaliwa bure bila hata kutugharimu sumni wala penni;

Ndio, ndani ya mipaka yetu hii WaTanzania tumejaliwa rasilmali watu tele kwa kiwango kisicholinganika hata na idadi ya watu wote katika mataifa mengine yote katika Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwekwa wote kwa pamoja. Watu wetu wanajulikana kwa ukarimu wa kumwagika, vijana wachapa kazi, akina mama wenye upendo wa hali ya juu na wazee wenye hekima tele na busara kote mijini na vijijini;

Naam, Mwalimu Nyerere vile vile alibahatika kuturithisha TAIFA TANZANIA NA UTAJIRI WAKE WOTE bila kudokoa hata punje ya utajiri huo ama chini ya ardhi au ardhi yenye rutuba kwa kilimo, ni kweli Mwalimu alituacha na taifa lenye deni nyembamba mno nje ya nchi lakini heshima tele kila mahali na watu wengi sana wenye uzalendo wa kutosha wenye kupenda MASLAHI ZAIDI KWA UMMA na wala si maslahi zaidi kwa vikundi vichache au familia teule tu;

Lakini leo hii, HESHIMA NA UKUU WA UTU WA MTANZANIA kamwe haupati sauti ya kutusemea, kutulinda na kutuwekea misingi yetu wenyewe wa maendeleo ya taifa letu na miradi mbalimbali si kutokana na umoja wa sauti zetu tena katika vikundi vyetu vya wakulima na wanyakazi wa nchi hii; mambo siku hizi yamegeuka hobela hobela tu huku tukiendelea KUNINGINISHWA KATIKA NDOANO YA 'MAAMUZI TOKA JUU' yenye kutuachia fursa mbili tu sisi kusema - 'Ndiyo' ili upate kuishi au 'Hapana' ilipate ubahatike kupata pasi ya mapema kwenda ahera;

Jamani ndani ya taifa la Tanzania ya leo hii kama tatizo letu wala UTAJIRI WA NCHI wala udhaifu wa sisi watu wake sasa hili la UMASIKINI WA KUDUMU KWA KILA MTANZANIA tuliowengi sasa chanzo chake ni nini tena???????????

Bila ya woga wala kutafuna maneno adaui namba moja wa taifa letu ni UFISADI kila kona ya nchi. Na haya yote ni matokeo ya UADILIFU HAFIFU WA VIONGOZI WETU WALIO WENGI SANA hivi sasa pamoja na SERA zilizopitwa na wakati zikiendelea kung'ang'aniwa na familia teule chache ndani ya mipaka yetu.

Tanzania mama yetu leo hii inaelekea kuangamia shauri ya Ubinafsi uliokithiri kila mahali katika kusimamia rasilmali za nchi; taifa laelekea kuangamia shauri ya kuendekeza hulka za MAAMUZI KUTOKA JUU na wananchi tukipuuzwa kila kukicha.

Jamani ni uchungu ulioje kuona taifa likilazimishwa kuangamia shauri tu ya baadhi ya viongozi wetu kuchagua kuahirisha kutumia silaha zetu za jadi katika taifa hili zikiwa ni pamoja na HEKIMA NA BUSARA katika kusimamia maslahi mapana ya umma wa nchi hii.

Siku zote miradi shirikishi na zinazoibuliwa na wananchi wenyewe, mikataba kuwekwa wazi mezani na faida kwa kila mdau kujulikana peupe, uzoefu unatujulisha, uendeshwaji wake huwa ni shwari kwa kila hatua na gharama nafuu bila mawaa.

WaTanzania sote tukajiulize je kule Lindi na Mtwara mwananchi kulazimika kunyamazishwa kwa mizinga ya kijeshi, wanawake kubakwe wake kwa mabinti zao, vijana kuchinjwa na kuzikwa katika makaburi ya pamoja porini na mama wajawazito na vichanga kuuwaua kinyama kwa kuwa tu wametaka maoni yao kuzingatiwa katika mradi wa gesi,kulikoni???????????

Wakati mwingine si jambo baya sana baadhi ya viongozi wetu kuchota busara kutoka katika fungu hili dogo la maneno;
Try not to become a man of success but a man of value.

Akiwa ktk kuchangia hoja juu ya bajeti ya wizara ya nishati na madini,mbunge wa mpanda mjini na makamu mwenyekiti wa Chadema taifa amesisitiza viongozi wa serikali kutumia hekima zaidi pamoja na busara ktk kutatua migogoro baina ya serikali na wananchi.

Hakika huu si wkt wa serikali ya ccm kutumia nguvu na mabavu ya dola ktk kuwanyamazisha wananchi,kwani huko ni kuongeza chuki kati ya serikali na wananchi
 
Back
Top Bottom