Said Mhando afariki dunia

Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,286
4,493
MCHEZAJI wa soka wa zamani nchini, Said Mhando (38), amefariki dunia jijini Dar es Salaam. Mwanasoka huyo mahiri wa zamani aliugua kwa muda mfupi.

Baba wa marehemu, Salum Mhando, amesema, mwanawe amefariki dunia leo asubuhi kwenye Hospitali ya Wilaya ya Ilala, Amana.

Amesema, alipelekwa jana usiku kutibiwa baada ya kuugua ghafla homa ya mapafu.

Kwa mujibu wa baba wa mchezaji huyo wa zamani, Mhando alianza kuumwa Jumatano iliyopita, lakini ilikuwa homa ya kawaida, hivyo aliendelea na shughuli zake kama kawaida.

“Lakini hali ilibadilika jana tukampeleka Hospitali ya Amana na leo mauti yakamfika,” amesema.

Amesema,msiba uko nyumbani kwa baba huyo, Magomeni Kota jirani na ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), atazikwa kesho alasiri Kisarawe mkoani Pwani.

Mhando alichezea timu mbalimbali ikiwemo Yanga, Mtibwa Sugar, Prisons ya Mbeya, African Sports na Coastal Union za jijini Tanga, na Vijana ya Handeni, pia mkoani Tanga.

Atakumbukwa kwa mchango mkubwa alioutoa kwa Yanga katika michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (sasa Kombe la Kagame), iliyofanyika Uganda mwaka 1999 na Yanga kutwaa kombe hilo.

Marehemu ameacha mjane na watoto wawili, Husna aliyezaliwa mwaka 1991, na Mustapha aliyezaliwa mwaka 1997.

RIP Said Mhando, poleni wapenzi wa Yanga na wapenda soka wa Tanzania.

Habari Leo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom