Sahihisho kipenga cha urais CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sahihisho kipenga cha urais CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Jun 7, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]  NA JOSEPH BURRA
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuwa, Juni 21 hadi Julai mosi, mwaka huu, itakuwa kipindi cha kuchukua na kurudisha fomu kwa wanaowania urais wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano. Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa, alisema hayo juzi katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa
  Lumumba, Dar es Salaam. Alisema wagombea kutoka bara watachukua fomu kwa Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba, katika ofisi za Makao Makuu ya Chama mjini Dodoma, kwa siku tisa kuanzia Juni 21, mwaka huu. Kwa upande wa wagombea wa urais Zanzibar, alisema watachukua fomu kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Saleh Ramadhan Ferouz, katika Ofisi Kuu ya Kisiwandui, mjini Zanzibar. Msekwa alitoa wito kwa wanachama wenye nia ya kuwania nafasi hizo kutumia haki yao ya msingi kujitokeza kuchukua fomu na kuzirudisha kwa wakati. Hata hivyo, alisema wanachama wenye nia wasiogope kuchukua fomu ya urais wa Jamhuri ya Muungano kutokana na kauli za baadhi ya viongozi kuwa Rais Jakaya Kikwete awe mgombea pekee. Alisema kauli zao zilikuwa za kumfagilia kutokana na utendaji wake wa kazi, lakini hazibadilishi kanuni za Chama, ambazo zinasimamia wanachama wote kupata haki hiyo. Kwa mujibu wa Msekwa, Julai 2 hadi Julai 8, kitakuwa kipindi cha wagombea kutafuta wadhamini wasiopungua 250 katika mikoa 10 nchini. "Kwa mgombea wa Jamhuri ya Muungano, kati ya mikoa hiyo lazima iwepo miwili ya Zanzibar, mmoja Unguja na mwingine Pemba, na wagombea urais wa Zanzibar wadhaminiwe katika mikoa mitatu mmoja kati ya hiyo uwe Pemba," alisema Msekwa. Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Julai 6, mwaka huu, Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa, itakutana kuandaa mkutano wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa utakaofanyika Julai 7, mwaka huu, kuwajadili wagombea wa urais. Alisema Julai 9, Halmashauri Kuu ya Taifa itateua jina moja la mgombea kiti cha urais wa Zanzibar na kupendekeza jina au majina ya wagombea wa kiti hicho wa Jamhuri ya Muungano. Msekwa alisema Julai 10 na 11, mwaka huu, Mkutano Mkuu maalumu utafanyika katika ukumbi wa Kizota, Dodoma, kuteua na kutangaza jina la mgombea kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano. Hata hivyo, alisema kutokana na sheria na kanuni za uchaguzi, Julai 12 hadi 18, mwaka huu, wagombea wa kiti cha urais watalazimika kutafuta wadhamini mikoani. Kwa mujibu wa Msekwa, ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inaonyesha Agosti 19, mwaka huu, itakuwa siku ya uteuzi wa wagombea. Hata hivyo, Msekwa hakutangaza ratiba ya wabunge na madiwani kuchukua fomu kutokana na kutojulikana siku litakapovunjwa Bunge. "Kuvunja Bunge ni siri ya Rais, ikijulikana tutatoa ratiba, tunataka ratiba yao iwe pamoja na madiwani, kwa uzoefu wangu taarifa atapewa Spika wa Bunge," alisema. Kuhusu kata zilizoongezwa, Msekwa alisema wenye nia ya kugombea udiwani watachukua fomu kwa Makatibu wa CCM katika kata zilizokuwepo awali, kwa kuwa uchaguzi utafanyika baada ya uchaguzi mkuu. L Imetubidi kurudia habari hii baada ya kukosewa katika toleo la jana ambapo ilielezwa kipenga cha uraos CCM ni Juni 9 badala ya Juni 21, mwaak huu.
  Sahihisho kipenga cha urais CCM
   
 2. G

  Godwine JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kiti kiko wazi kazi kwenu wanasiasa
   
Loading...