Safari za ndege zaanza tena Ulaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Safari za ndege zaanza tena Ulaya

Discussion in 'International Forum' started by MziziMkavu, Apr 20, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280


  Siku sita baada ya vikwazo vya usafiri wa ndege kuwekwa kaskazini mwa bara ulaya, kufuatia jivu linalotokana na mlipuko wa volcano nchini Iceland, ndege kadhaa zimerejelea safari zake.

  Ndege tatu ziliruka kutoka uwanja wa Schiphol mjini Amsterdam na kuelekea miji ya New York, Shanghai na Dubai. Shirika la ndege la Ujerumani, Lufthansa limesema, baadhi ya ndege zake zilirejelea safari zake kutoka uwanja wa Frankfurt jana jioni.

  Awali mawaziri wa uchukuzi wa nchi wanachama wa muungano wa ulaya waliafikiana kulegeza vikwazo vya usafiri wa ndege kufuatia majadiliano yaliyofanyika kwa njia ya video.

  Eneo hilo sasa limegawanywa mara tatu, moja eneo ambalo usafiri wa ndege umepigwa marufuku, pili eneo ambalo usafiri wa ndege utaruhusiwa endapo kutatokea haja na nyingine ambalo mashirika ya ndege yako huru kutumia wakati wowote.

  http://www.msnbc.msn.com/id/36664233/ns/us_news-crime_and_courts/
   

  Attached Files:

Loading...