Safari za Dar-Moro zinahitaji jicho la ziada

Cherenganya

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2018
Posts
2,309
Reaction score
1,787
Wanabodi

Wanasheria wanakawaida ya kuyatenga au kuyagawa makosa katika makundi mfano, Makosa ya Jinai, Makosa ya Madai na au Makosa ya Kikatiba. Mimi ninao theory yangu inayo jitegemea ambayo ni Makosa dhidi ya Mtu na mtu, yaani A kampiga kofi B na pia A kamsukuma B akasababisha madhara kwa C, au A kamlazimisha B kufanya kosa na mwisho kabisa A na B wanashirikiana kwa hiari yao kutenda kosa..

Wanasomi wa sheria mtanisamehe sana kama nitakua nimeleta mvurugo kwenye KITIVO chenu, ila Taifa letu Tanzania lina watu wa hovyo labada HOVYO haitabeba uzito wa UHOVYO ninao ukusudi.

Nikiwa abiria mwenye siti namba 2 katika basi la ABOOUD BUS SERVICE namba T877 DJP toka Dar - Moro, Dereva anaitwa Yahaya, nilipata shida sana pale abiria wenzangu waliolipa nauli ya Sh 6,000 kwakua wamekosa siti na kukalishwa kwenye Godoro litalotandikwa juu ya injini. Labda hilo halikuwa tatizo sana kwakua labda walikua na sababu zao za msingi, nimesema 'labda'.

Abiria hawa tuliokuwa nao basi moja walipata usumbufu wa kushushwa mara kadhaa kwenye gari na kufaulishwa kwenye COSTA ili kuwapita askari waliopo mbele yetu, na tulipo fika Kibaha Maili moja nilishuhudia dereva akitoa Sh 5000 na kumkabidhi Muuza maji ili awapelekee Trafic, kabla gari haijaondoka dereva anapiga simu na kumwambia mpigiwa simu kwamba vijana wako wanatabia mbaya anasema mimi nimeshusha abiria watangulie mbele,...

Baada ya simu sasa dereva anasema ooh mimi nabebeshwa abiria, nasumbuana na Trafic wakati mwenye gari ndio anachukua hela yote, kwanza hata hivyo nauli inatakiwa iwe 10,500/- na sio 7,000, ooh ingekua mimi ningefanya 7,500 alafu hakuna mtu kukaa kwenye godoro alienda mbali sana na kuanza kutoa maneno ya hovyo kwamba mnang'ang'ania kupanda ABOOD kwani hizo COSTA hamzioni.

Aidha, Bwana Yahaya akaenda mbali zaidi kwamba mimi namfahamu ABOOD toka mwaka 1987 kiasi kwamba hata akiniambia kazi basi leo sina shida na kazi yake.

Sasa najiuliza ndani ya basi lile kuna namba za Trafic ambazo zinasema kama gari ikizidisha abiria piga namba hizi, kweli kweli ndio fimbo ya kumchapia mnyonge, mimi kabla sijawasiliana na Trafic naona Dereva anapiga simu kutoa mashitaka kwamba kwanini huyu msichana (Trafic) anachukua hela yake na huku analeta kidomodomo.

Ni wakati sasa kama hatuwezi kuheshimu sheria basi tutengeneze utaratibu wa kuheshimiana wenyewe.

Nawasilisha nikiwa na huzuni kubwa.
 
Unafanya nini uko ?? Rudi mlanda Tulime vitunguu swaumu .mr chelenganya
 
Mbali na hayo mambo ya kisheria, jifunze kuandika maneno machache ya kueleweka
 
Watunga sheria ndio wavunja sheria wakubwa!
 
Vipi kuhusu kusafiri masaa 6 Dar -Moro sio shida?

Aisee, katika shida hii ni samba moja. Siku moja tumetoka stendi ya Msamvu saa mbili na dakika kumi asubuhi. Tumeingia Ubungo saa saba kasoro robo mchana. Hadi toyo ilituovate... Tena basi kama tatu hivi kwa mpigo...
 
Haujaeleweka vizuri au mimi sijakuelewa vizuri,sasa madai yako hasa ni nini?
 
Aisee, katika shida hii ni samba moja. Siku moja tumetoka stendi ya Msamvu saa mbili na dakika kumi asubuhi. Tumeingia Ubungo saa saba kasoro robo mchana. Hadi toyo ilituovate... Tena basi kama tatu hivi kwa mpigo...

Hivi hakuna kampuni mbadala kwa hiyo route, kule Mwanza - Tarime kuna kampuni ya Zakaria. Mambo niliyojifunza toka kampuni ile ni;
  • Usafiri hauna abiria wa ziada wanaosababisha usumbufu kwa abiria wengine kama vile kushushwa na kupakiwa kwenye coaster kwenye check point na mizani ambako huchangia kwa kiasi kikubwa kukawia kufika
  • Malalamiko ya abiria yanafanyiwa kazi palepale yanapowasilishwa kwenye management
  • Madereva wanawaheshimu sana abiria wao hasa pale wanapowasilisha shida zao.
  • Kauli za wafanyakazi kwa wateja ni rafiki
Nashindwa kujua kwanini usiwepo uwekezaji wa namna hiyo katika route ya Moro To Dar
 
Back
Top Bottom