Safari za daladala toka Kigamboni kwenda maeneo ya jiji kupitia darajani

bobdizo

Senior Member
Jun 28, 2014
137
50
Wadau hebu toeni maoni yenu hapa kuhusu hizi trip mpya za daladala
3ba1430f8f44f11ad8c0cdd294552bf6.jpg
 
Hebu ngoja!! Ukitoka Kigamboni kwenda "Kariakoo" ni kwamba daladala zitatumia Barabara ya Kurasini na kutokeza Chuo cha Diplomasia/JKT? Au ile barabara ishapanuliwa?!

In addition, ukifika Bandari kituo kinachofuata ni Keep Left kisha nduki hadi Machinga Complex! Keep Left hiyo ni ipi? Au KAMATA? Na kama ni KAMATA, hivi kuna eneo pale la ku-accomodate watu wa kutoka Kariakoo kwenda Kigamboni?!

Hizo nauli zipo sawa tu!
 
yaani ndio tutaona wakianza hizo trip kama kuna mapungufu watarekebisha nadhani
 
nitaziweka tena fresh kama haionekani vizuri hiyo list ya rout
 
Hawajatoa route ya Kigamboni kuja maeneo ya ndani ya Kigamboni kama Mjimwema, Geza, Kibada n.k???
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imeanzisha njia mpya ya usafiri wa daladala kati ya Kigamboni na maeneo mengine jijini Dar es Salaam. Ilianza juzi kutoa leseni kwa mabasi ya daladala yanayobeba abiria kati ya Kigamboni - Machinga Complex iliyoko Ilala, Temeke na Mbagala Rangi Tatu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Mawasiliano ya Umma ya Sumatra, njia hizo zimeanzishwa kutokana na kufunguliwa kwa Daraja la Mwalimu Nyerere linalounganisha Kigamboni na maeneo mengine ya jiji hilo kwa barabara.

Sumatra imewataka wamiliki wa mabasi yanayofanya safari hizo na wawekezaji katika sekta hiyo kuwasilisha maombi ya leseni katika ofisi zao mkoa wa Dar es Salaam. Imewataka kuwa na madereva na makondakta watakaozingatia masharti ya leseni.
 
Back
Top Bottom