Tanzania ya baada ya Baba wa Taifa, inayo mengi ya kuwatenganisha Watanzania kuliko kuwaunganisha. Maendeleo makubwa yanayoweza kutarajiwa kwa mfumo wa sasa ni jua kuchwa na kuzama. Mengine kama barabara nzuri, maji safi na salama, elimu bora ni yatokanayo; yanatokea kwa nasibu na hayajali ubora. Siasa zimekuwa za chuki, udini, ukanda, wenye nacho, ushirikina, n.k Wakuu wa Serikali na chama tawala wamepotea dira. Nchi inakwenda tu bila kujua inaelekea Kaskazini na je ndiko ilikopanga kwenda au inashuka kusini zaidi na kujipongeza! Hata tukifarakana, tukapigana, tukakatana mapamnga, Tanzania haitoweza kuamka na kusimama ili ianze kufuata vema njia ya maendeleo kama Rwanda. Sababu ziko nyingi lakini za haraka ni uwepo wa makundi kinzani mengi (udini, siasa, maskini na matajiri) ambayo chuki zake zimejengeka taratibu na kwa muda mrefu na sababu ya pili uwepo wa rasilimali (mafuta, uranium, gas achana na dhahabu) zilizoadimika katika ulimwengu wa mabeberu na ambazao faida yake kubwa haipatikani kama uchimbwaji wake unafanyika katika jamii yenye amani. Hivyo kiberiti kikiwaka, hawa mabeberu watakuja haraka sana kusaidia pande hasimu kuingia vitani ili wao wauze silaha, nyinyi muendelee kumwaga damu, na wao waendelee kuvuna rasilimali kwa urahisi zaidi.
Naijionea huruma siku hiyo ikinikuta ningali hai......