GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,292
- 6,769
Zilikuja taarifa kuwa Kuna madini yamegunduliwa Mozambique na watu wengi wanakimbilia huko, Rafiki zangu kadhaa na watu wengi ninao wafahamu waliacha shuguli zao na kuingia kwenye Mkumbo huo, wengi wao walirudi kimya kimya na kujikita kwenye shuguli zao bila hata kueleza kilichojiri huko.
Hiyo ilikuwa ni miaka kadhaa nyuma, Mwaka 2012 mwishoni kijana mmoja ambaye nilikuwa namtumia sana kwenye shuguli zangu za kusafisha Mabanda ya Kuku n.k aliniomba ruhusa ya kwenda Mozambique kujaribu bahati yake, hii ilikuwa ni baada ya tetesi za kugungulika madini ya RUBI katika eneo la MTIPWEZI. Safari hii utitiri wa Vijana ambao walikuwa wanamiminika kuelekea eneo hilo ulikuwa ni mkubwa zaidi. Tofauti na Mwanzo safari hii wengi walirudi na majibu mazuri, wengi walirudi wakiwa wamepata kati ya 5,000,000 mpaka milioni 50.
Yuko Mtu mmoja ambaye alielekea huko kama kuficha fedheha yake baada ya kufumaniwa na Mke wa Mkuu wa kituo cha polisi, yeye alirudi meno nje baada ya kuambulia dola15,000 huku akisahau yale yote ambayo yalimkuta, lakini kubwa ni kwa huyu aliyekuwa mfanyakazi wangu ambaye aliweza kupata kiasi cha Shilingi milioni 80. Aliporudi alikuja kunishukuru na kuniachia shilingi milioni 2. Kitendo cha kijana huyo ambaye alikuwa choka mbaya kurudi na mafanikio makubwa kiasi hicho kilimshawishi rafiki yangu wa karibu ambaye anamiliki Mashamba, mifugo, duka la spea za pikipiki na mashine ya kusaga naye kujaribu bahati yake.
Waliondoka watu wanne, ilimchukuwa wiki mbili tu naye kurudi akiwa na kiasi cha shilingi milioni 140 baada ya mgao wa watu watatu kufuatia kifo cha mwenzao mmoja ambaye alifia hukohuko akiwa shimoni.
Ikafika zamu yangu, Niliondoka mwezi wa kwanza 2014 kuelekea MTIPWEZI nilipitia Kilambo Mtwara pale tulivushwa na boti kwa Tsh 10,000 (ukivuka na pantoni ni tsh 500 (mia tano)) Tukafika eneo maarufu la uhamiaji la msumbiji linaloitwa NAMOTO, nikiwa na pasport yangu ya ujirani mwema lakini wewe kama unataka kwenda kwa kutokea huku Tanzania ni rahisi zaidi ukipitia Chikongo (uliza tu) nilipita vijiji kadhaa kama Kiyonga hadi kutokea wilaya ya Palma, hapo nilipumzika kwa siku moja kabla ya kuendelea na safari iliyonifikisha Musimbwa.
Nilipumzika Musimbwa kwa siku mbili kabla yakuendelea na safari, Nilikuwa peke yangu sikuongozana na yeyote yule, wenyeji wangu walinieleza ugumu wa ninakoenda lakini wakanipa moyo kuwa wengi hufanikiwa huko ingawa wao hakuna aliyejaribu bahati hiyo.
.Baada ya mapumziko hayo jiooni ya siku iliyofuata nikaingia Rasmi eneo la machimbo linalojulikana kama MTIPWEZI, Miongoni mwa vitu ambavyo vilinisisimua ni kukutana na rafiki yangu ambaye tuliachana mara ya mwisho baada ya kumaliza Darasa la saba, ni miaka mingi wengi walikuwa hawajui yuko wapi lakini nimemfuma huko, yeye alikuwa wa kwanza kunitambua na kustaajabu baada ya kuniona nikiwa na kitambi (Nimeanza kukiondoa) hakujua kuwa licha ya kitambi changu nina mazoezi ya kutosha kuweza kupiga kazi za kuchimba
Siku ya pili nikaanza kazi baada ya kujiunga na watu wanne ambao nilikutana nao huko, wawili walikuwa ni wa Msumbiji, mmoja Mtanzania na yule mwingine alikuwa anatoka Zimbabwe, miongoni mwa maswali niliyoulizwa ni kama nilikuja na dawa yoyote ya kunisaidia katika mashimo, nikawajibu kuwa sina walinicheka sana wakisema kuwa nimekuja kitoto, yule mmoja wa Mozambique alinionyesha Korodani za Binadamu alizodai kuwa ni za mjombaake na amekuja nazo ili ziweze Kumsaidia. Sikuuliza kama kamuua au ilikuwaje kwani nilishaingiwa na woga na kundi hili na wala sikutaka kuuliza hao wengine wamefanya nini.
Ilipofika saa mbili usiku tukiwa tuko eneo la machimbo ilisikika milio ya Risasi, Shimo letu halikuwa kubwa sana Hivyo tuliwahi kuchomoka na kukimbia. Watu walikuwa wanakimbia ovyo kunusuru maisha yao wengine walikamatwa na tulionusurika ndio hivyo tena tulijichanganya maporini. Ndugu yangu usifanye mchezo na njaa ya siku mbili. Kitu nilichoambiwa (sijathibitisha) Ni kuwa wale wanaokamatwa huuwawa na kutupwa kwenye mashimo ya madini.
Tulikutana na mambo mengi sana, nafasi haitoshi kusimulia yote hayo, ni katika kisa ambacho nimeshuhudia mwenzetu ambaye tulikimbia naye akiiaga dunia.
Tofauti na Wenzangu mimi nilikuwa na ile TEMPORARY PASPORT hivyo sikupata shida kuingia katika eneo lolote lile. Niliachana na wenzangu katika kijiji kimoja ambako Nyoka huwa wanaliwa sana, wanaitwa CHIDUDU ukisikia chidudu kama huli nyoka acha maana inafanana sana na Samaki.
Kutoka hicho kijiji niliweza kusafiri hadi PALMA, Palma nilikutana na fursa kadhaa ambazo zilinifanya nijaribu kuwashawishi wanaJF humu ndani kuweza kuchangamkia fursa hizo lakini kama kawaida wengi walionekana kutoniamini, nilijua ilikuwa ni vigumu kuniamini lakini ulikuwa ni mpango mzuri ambao wachache ambao walichangamkia Fursa hizo wamefanikiwa sana (sio niliowashawishi mimi)
Mwisho napenda niwaeleze kuwa mafanikio yana mapito yake ambayo ni magumu kweli kweli kwa yeyote ambaye atakutana na mikasa kama hiyo basi hatakiwi kukata tamaa bali azidi kukaza Buti.
NAWATAKIA ASUBUHI NJEMA.