Safari yangu ya leo, nimebahatika kukaa na Mrembo mwenye mshepu wake

Story inaanzia hapa..
Nimeingia kwenye basi nina begi langu la mgongoni nimeshikilia risiti mkononi natafuta seat yangu,
Nakutana na seat mbili zipo wazi moja ni yangu nikakaa seat ya dirishani kusubr safar kuanza.

Baada ya dakika kma 2 hiv naona anakuja binti ambae basi kama lilitaka kumuacha hivi, kafika na kajitupa kwenye seat iliyobaki pembeni yangu huku akihema juu juu kiasi..
Namtizama tu mimi sina usemi kama kawaida yangu lakini macho yangu huwa hayatulii yanaangaza huku na huku..
Mala akanipa Simu yake pamoja na Earphone nimshikie ili akachukue begi lake lilikua mbali kidogo..
Aliporudi kukaa nikamrudishia simu yake..
Akanisalimu, Safar ikaanza..
Akaanza kujieleza yeye mwenyewe, ohh nimetokea hospitali, na pili nilikua na mizunguko sana yani nimechoka..
Mie namsikiliza tu..
Kwenda kidogo, Basi likasimama binti akaona mahindi ya kuchemsha, kusogea kuchua Muhindi dirishani, maziwa yake yote yakaishia kifuani kwangu, akatoa elfu tano chenchi ikakosekana.. na basi linataka kuondoka ..

Ikabidi nilipe mimi maana nilikua na pesa ya chenchi, nikapewa asante kama zote, akanikatia muhindi nikataka kugoma kuchukua, akanilazimsha nikawa sina jinsi, nikapokea.

Sikua na safar ndefu, nikafika ninapo kwenda, binti akaniaga kwa kunishukuru sana.

HIVYO NDIVYO SAFAR YANGU YA LEO ILIVYOKUWA.
Sikuchukua namba hata, nikamwambia dada ubarikiwe sana, Mungu akipenda tutaonana tena.
Katika siku ambazo hujawahi jitendea haki basi ni pamoja na leo
Umekwama wapi?
 
Jana nilikaribishwa kwa jirani, nikakuta wamepika ugali maharage ya nazi...

Je, niandike uzi kwa kukaribishwa ugali maharage?
jukwaa limepoa sana mimi nilitaka nichangamshe tu jukwaa, japo story yangu haikua na maajabu yoyote mwishoni 🤣😅😅
 
Hii stori yako inabidi uitengenezee uzi wa Kuwa bwege kimasihara , ungekua mzima ungechukua hata mawasiliano ela yako ya muhindi isipotee bure.
 
Back
Top Bottom