Safari yangu ya kielimu kunde ekeke

Safari yangu ya kielimu kunde ekeke

Safi sana Kunde, kuna mdogo wangu kamaliza Six matokeo ndo ya juzi ila sio mazuri.... analilia degree ‘yoyote’ tu mradi apate mkopo.
Nikimshauri kuhusu fani inabidi niahidi kumlipia ada, hebu tupeane mawazo.... nimsukumize VETA au Diploma kozi gani..?
Mpeleke veta akipata level 2 atajikuamua kimaisha
 
mm nilifeli darasa la nne, nikafeli veta, nikafeli mafundisho ya dini asaiv nimefeli maisha, nasubr pengne naweza feli hata kufa.
Mtu aliye feli maisha ni yule aliyekufa
Uhai ndio maisha
Kifo mwisho wa maisha au kufeli maisha
 
Mimi kama ikibidi kuishi moshi ni marangu tu hali ya hewa safi ila huko kwingine ukitoa machame kibosho na moshi mjini Hali ni ngumu sana
Uchagani yote Hakuna eneo lililo nyuma kote maendeleo ni 90% kwanzia rombo,mwika, marangu,kilema,himo,vunjo,kirua,machame,uru, kibosho,old Moshi ,siha nk
Nadhanj huijui uchagani mkuu
Vijin ndan ndan kabisa Ni kijani Cha kahawa na migomba huku majumba ya kifahari yakitamalaki
TEMBEA UCHAGAN YOTE ULETE USHUHUDAView attachment 1154591
IMG_20190626_125940.jpeg
IMG_20190611_114834.jpeg
 
Muhandisi anaweza akajua vipimo na masomo ya darasani lakini asijue kushika kono bao na mwiko kujenga.
Fundi ujenzi anaweza asijue hesabu za darasani lakini akajua kujenga Bila shida yoyote.
Wapo mafundi wengi hawajui hizo hesabu. Lakini ndo wanaojenga.
Na wapo wahandisi wengi wanajua hesabu lakini kujenga hawajui
Dah... tofauti yao ni nini?
 
Muhandisi anaweza akajua vipimo na masomo ya darasani lakini asijue kushika kono bao na mwiko kujenga.
Fundi ujenzi anaweza asijue hesabu za darasani lakini akajua kujenga Bila shida yoyote.
Wapo mafundi wengi hawajui hizo hesabu. Lakini ndo wanaojenga.
Na wapo wahandisi wengi wanajua hesabu lakini kujenga hawajui
Kuna vijana wanakuja field ata mwiko unampiga chenga kushika lakini wenye degree kutoka India anajua kila kitu elimu yetu bado
 
Habari zenu ndugu zangu nina imani mko poa.Hii ni historia yangu fupi ya kielimu.

Baada ya kumaliza darasa la saba Bukoba nilienda Uganda sehemu moja inaitwa Kakuuto kusoma english course huu ni utaratibu uliokuwepo kwa vijana walio maliza la saba kwenda Uganda sijui siku hizi sijui kama utaratibu bado hupo kulikuwa na mawakala hii ilikuwa 2007.

Matokeo yalipo toka nilifaulu nilichaguliwa kujiunga kidato cha 1 nikiwa katika jitihada za kujiunga january mzee wangu akahamishiwa Dar 2008 ikabidi niongozane nae.

Nikaangaika nikapata shule Wilaya ya Temeke nikaanza shule 2011 nikamaliza form four matokeo yangu hayakuwa mazuri sana nilipata History C English B na English in literature B Civics D yaliyobakia nilipata F.

Nilimpelekea mzee result akasema hapa uchague urudie hama ukasome Uganda kidato cha tano nikaona isiwe shida nikachagua kwenda Uganda kupiga advance 2012 mwezi March nikafunga safari mpaka nyumbani Bukoba nikaanza kuulizia shule za bei nafuu mzee alisema isizidi laki 7 kwa mwaka.

Nikafanya mchakato wa passpprt nikapata ya mwaka 1 nikapanda gari mpaka Kampala kipindi hicho nauli ilikuwa elfu 15 Bukoba to Kampala nikasaka shule nikapata ya walokole ada ilikuwa laki 5 kwa mwaka nikarudi home Bukoba nikamcall mzee nikampa data.

Huku nikisubiri mzee aje twende Uganda nikajiunge na shule nikapata kibarua cha kusaidia mafundi kujenga yalikuwa majengo ya zahanati kwa siku nilikuwa nalipwa elfu 6 nikaona mafundi wanapiga hela nakaachana na mawazo ya kusoma advance nikaona bora niingie Veta.

Nikamueleza b mkubwa akakubali shingo upande ila mzee alinielewa akanipeleka shirika la elimu Kisarawe 2013 nikapiga Mason mpaka level 1nilimaliza. Sikuendelea na le level 2 nikaanza kufanya kazi hela zinakuja tu jengo la mfuko wa jamii lilinipa uzoefu mkubwa hapo station posta ya zamani sikujuta kusoma ufundi.

2015 niliamua kurudia baadhi ya masomo nikaagiziwa kwa Aziz kuna ticha anafundisha fresh anaitwa Ginga nikachua masomo 3 Kiswahili, Civcs na Math bahati nzuri nilipata kazi kupitia kampuni ya Estim kujenga ubalozi wa India nikapata muda wa kuingia job nikawa naudhuria darasa la jioni nikafanya mtihani civics D Math F Kiswahili C, nikaunganisha matokeo 2016 nikaanza kusoma Advance 2017 nikafaulu.

Nikatulia kwa sasa naendelea na shughuli zangu za ujenzi hapa Bukoba kuna project nafanya mwezi kesho nitakuwa Zanzibar sehemu moja inaitwa Fumba naenda hii ndio raha ya ufundi ulali njaa.

Kwa kuwa nina malengo ya kuwa engineer narudi Veta kusoma level 2 pale Kibaha Kongowe mwakani January ili nipate sifa ya kusoma ngazi ya juu.

Ushauri wangu nyote mliosoma masomo ya art kwenda kusoma chuo kikuu kupata ajira ni mtihani ni bora ukasoma fani kuepuka kuwa mzigo baadae.
Kiongozi,hiyo kunde ekeke ndo kitu gani?
 
Back
Top Bottom