chazachaza
JF-Expert Member
- Feb 21, 2018
- 2,824
- 3,846
Habari za wasaa wana JF.
Asubuhi ya leo nimedamka mapema sana tayari kwenda bus terminal kwa safari ya kutoka jiji la mbeya kwenda jiji la Dodoma.
Nilifika stend mapema sana saa 0600 asubuhi ya leo, basi nimekuta lina abiria kama 8 tu. Basi safari ikaanza saa 1230 asbh, kufika kituo fulani sitakitaja hapa, bus likapiga Kona kuuingia mtaani lakini katibu na mainroad. Eee bwana ee tumepack pale mpaka saa 3 kumbe jamaa walikuwa wanawasubiri abiria wengine lakini hawa abiria ni Wamalawi wameijaza bus nyomi, hadi hewa nikaanza kuona imekuwa nzito.
Tukaondoka na kuanza safari yetu, dereva hakusinzia akaanza kukanyaga pedo ya accelerater, bus ikakubali, ndani ya bus kinachosikika ni Kimalawi tu maana wako wengi kuliko sisi abiria wa kibongo. Pembeni yangu akaja abiria akaniongelesha akiwa anataka kunisalimia nikatikisa kichwa tu, akagundua mm si Mmalawi ikabidi abadili lugha, how are you friend? Nikamuitikia, am fine and u? Akajibu, fine.
Ghafla akaanza kukohoa mara kwa mara. Kikohozi cha huyu Mmalawi niliekaa nae siti moja, kikanikumbusha nimonia kali inayosumbua mpaka sasa. Kumuangalia hajavaa barakoa, nikawaangalia na wengine hasa hawa wamalawi pia hawana barakoa.
Tukafika kituo fulani baada ya mwendo mrefu, hapo kulikuwa na gate, askari akaingia akakagua abiria wote na kuwakagua hawa Wamalawi passport zao, akajiridhisha akashuka. Bus likaruhusiwa tukaendelea na safari.
Nikajiuliza inamaana huyu askari mbona hakagui suala la kuvaa barakoa, na humu tuna abiria wamejaa wamalawi tupu humu ndani.
Kiukweli hili bus sijui lilikodiwa na hawa wamalawi, hapo ndo sijui, ila kinachotia shaka ni hii nimonia kali na nasikia huko Malawi imechanganya sana kuliko hata hapa tz, na hawana hata barakoa.
kiukweli kipindi hiki tunaosafiri tunasafiri katika mashaka kibao, hasa bus zinazotoka mipakani.
Hapa nilipo sitaki stori na huyu jirani yangu Mmalawi kuhofia nimonia kali. Sio kwamba namtenga Ila sasa nyomi hii na hawa wamalawi, ndo inanipa shaka.
Baadhi ya picha nilizpiga: