Safari yangu CTC

Safari yangu CTC

Braza Kede

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
5,165
Reaction score
8,959
Kwa msiojua CTC ni kituo cha kuchukulia dawa za kudhibiti virusi vya HIV (UKIMWI).

Anayechukua dawa hizo anaweza kuwa ni mtumiaji wa muda mrefu au yeyote yule anayejiona ameingia kwenye hali hatarishi ya kupata maambukizi.

Sasa juzikati harakati za maisha zilinifikisha kwenye moja kati ya vituo hivi.

Pale nilishuhudia yafuatayo.

Ukarimu wa wahudumu. Kati ya vitu vilivyonishangaza ni ukarimu wa watoa huduma. Hapo watoahuduma wanawasiliana na wateja kwa staha na utulivu.

Hii ni tofauti sana na vitengo vingine ya hospitali ambako makelele huwa mengi.

Pale ni fulu customer care, kwanza pale mgonjwa anaitwa 'mteja' na wala sio mgonjwa.

Ukiondoa hayo nilijifunza UKIMWI UPO. Kulikuwapo misururu ya makumi ya watu waume kwa wake, lakini hasa wanawake wa rika zote kuanzia watoto, vijana balehe na watu wazima wakiingia na kutoka pale kituoni.

Makutano makuu yakiwa dirisha la kuchukulia dawa. Pale palikutanisha wakongwe wa muda mrefu, wanaoanza dawa na wanaochukua kwa dharura.

Kwa ujumla niliona kuna utulivu mkubwa huku sauti pekee zinazosikika zaidi ni za wale manesi watoa huduma wakiwasiliana kufanikisha kazi zao.

Huduma inatolewa kwa spidi ya upepo. Hakuna muda wa kupoteza. Ukiona mtu amekaa tu basi ujue anangoja kufanyiwa kipimo flani au majibu ya vipimo, nje ya hapo mwendo ni bandika bandua.

Kwa upande wa wateja, niliona wachache hasa wale unakuta wamekuja pamoja au inaelekea wamefahamiana kitambo ndo unakuta wanapiga stori kwa sauti ya chini ila nje ya hapo hakuna na stori zaidi ya kukodoleana macho.

Nachotaka kuwaambia leo humu UKIMWI UPO, ndio narudia tena UKIMWI UPO na wanaoupata sio wengine, ni mimi, wewe na yule.

Sasa basi, kama wewe hujui hali yako pima ujue hali yako.

Kama wewe ni negative basi jilinde na ujiepushe na njia za kukupa maambukizi.

Lakini kama tayari umejikuta positive sio kesi pia, jikubali tu maana hata ufanye nini hauwezi kubadilisha hali hiyo. Ila jua kuna wengine wengi tu wa hali hiyo, zingatia kujilinda usijiongezee maambukizi mapya, usisambazie wengine na cha muhimu zaidi pata dawa zako kwa usahihi ili maisha mengine yasonge kama kawaida.

Kheri ya maandalizi ya Eid.

Kheri ya maandalizi ya Pasaka.
 
Nilidhani unataka kuelezea hali ya KABLA na BAADA ya Trump kusitisha kufadhili huduma hizo
 
Back
Top Bottom