Safari ya miaka 2 kusoma Diploma ya ICT imeanza Leo ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Safari ya miaka 2 kusoma Diploma ya ICT imeanza Leo !

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Rutunga M, Sep 15, 2011.

 1. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2011
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Wakubwa,

  Leo nimeanza safari ya miaka 2 ya kusoma Diploma ya ICT katika chuo fulani nchini Tanzania.
  Kwa kuwa hii fani ni pana,ningeomba wajuzi wa hii kitu wanijuze ni mambo yapi natakiwa Niyajue baada ya kuhitimu.hivyo naomba wataalam mnisaidie kwa hilo.

  Iwapo mungu ataniweka hai nitarejea katika hii post baada ya miaka hiyo miwili.

  Note:Nasoma ili nipate ujuzi siyo karatasi(cheti)
  Nasubiri
   
 2. HT

  HT JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kumbe sio mdogo wako?
  Tafuta mtaala wa chuo husika, utajua yakupasayo kujifunza. Pia field of interest ni muhimu kama SE, Networking, DBMS Admin et al
   
 3. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #3
  Sep 15, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 908
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
 4. F

  FUSO JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  Diploma ya ICT unakuwa bado una mambo mengi ya kujifunza na inategemea Diploma hiyo ina contents zipi ila cha msingi katika masomo yako jaribu kufuata mkondo kati ya hii ifuatayao maana ICT ni pana sana.
  1. Computer Programming - uwezo wa kuandika application softwares kwa kutumia lugha za kumputa, unatakiwa uwe mwerevu hasa kwenye logics, hesabu kwa ujumla ( Hii haina siko may be uwe mwalimu)
  2. Data Base Programming - uwezo wa kuandika Database kwa kutumia lugha za nne za komputer ( Hii ina soko sana kwa sasa) hapa unakutana na programs kama Oracle, Visual Basic, SQL nk
  3. Network Systems - Hapa utajifunza ujuzi wa ku install servers, routers, switches na mawasiliano kwa komputer kwa ujumla,
  kuna mitihani ya Microsoft na Cisco unaweza kufanya ili kujipima ujuzi wako. ( Hii ina soko sana hasa kwa makampuni ya kugawa internet (Internet Service Providers), Kwenye mabenki vitengo cha ICT hasa security systems, Makampuni ya Simu kama VODA, TIGO, ZAIN nk
  Kifupi ukifuata mkondo huu unatakiwa uwe mwerevu, mdadisi na unayependa kujifunza hasa logics. ( Hii ina market kubwa sana)
  4. Web Designing -- hii ni kutengeneza web pages, blogs na vitu kaa hizo -- kwa mafano unapofungua hii JF basi kumbuka kuna designing imefanyika ya hali ya juu. ( Hii ina market kubwa sana)

  Diploma Level hiyo ya miaka miwili watakufundisha kidogo kidogo kwenye mambo hayo 4 si detailed, kinachotakiwa wewe ndiyo uchague mkondo utakaoupenda na kujisomea zaidi na zaidi bila kuchoka ili ukimaliza Diploma yako basi unaweza either kujiajiri au kufanya kazi fupi kwa malipo. Kuajiriwa kwa kudumu ukiwa na Diploma level si rahisi kwa sasa.

  Nakutakia maisha mema na hongera sana kuchagua ICT ingawa kozi hii ni pana sana kuliko vile watu wengi wanafikiria.

   
 5. chiko

  chiko JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2011
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hapo Kweli kabisa, cha kuongezea; Hali ya masoko, isiwe issue sana kwako, kwani ICT waweza kujiajiri mwenyewe, ukijitahidi hata hio diploma inaweza kukupa upeo mkubwa. Watanzania tusiwe na mawazo ya kizamani kuwa " kusoma ndio kupata kazi!" karne ya sasa, uchumi unajengwa na wanaoji ajiri!!!, Mwisho usiseme kuwa tutaonana baada ya kumaliza hio kozi, jaribu sana ukipata nafasi uwe uki "Browse Internet" na kutembelea hili Jukwaa kwani ICT ina kasi kubwa sana kila kukicha!!!
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa vizuri utaje mtaaala wa hiyo diploma ili wadau wakueleze wapi pa kukomaa la sivyo utaamabiwa mambo amabyo hayapo covered kwenye mtaala wako.
   
 7. C

  Chief Lugina JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 290
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mungu akujalie ufike salaama......................................!
   
 8. IHOLOMELA

  IHOLOMELA JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 834
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 80
  Kuna mdogo wangu yupo Nzega anataka kusoma Diploma ya ICT lakini ana HKL na o-level alikuwa na F ya Basic Maths na Physics. Je anaweza pata chuo? Naomba nijuzwe wadau, maana dogo kanikomalia kinoma ila nakuwa cna mzuka kutokana na performance yake ya masomo ya sayansi. Msaada plizzz!
   
 9. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,015
  Likes Received: 2,661
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Mkuu nimependa sana ulivyo ielezea ICT japo kwa kifupi tu.
   
 10. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2011
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,854
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  ungesema ni chuo gani itusadie na sisi wengine tulio na intrest ya kusoma ICT lkn hatujapata mwanga wa kutosha.
   
 11. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  tehe nilipiga Java 2001 - 2002. niliandika Codes mpaka vidole viliuma. SQL database adminstration. ICT bomba sana kijana kaza uzi
   
 12. Robati

  Robati JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 292
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  wewe ni mdau mzuri, tanzania bado sana kwenye ict, changamkieni fursa hiyo vijana
   
 13. B

  Bokohalamu Member

  #13
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 13, 2012
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mimi nina D ya hesabu o-level na kupata Division 2,nikachukua HGE A-level nikapata S ya hesabu na Division 3,ingawaje nilichukua uhasibu chuo na sijapata kazi ila ninapenda sana kujua ICT computer kwa ujumla!Je nikiomba vyuo vikuu naweza kuanzia na level ipi kwa maana ya certificate ama degree?
   
 14. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #14
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Kabla sijakushauri nin cha kufanya ningependa kupata course outline ya hiyo DIploma
   
Loading...