Safari ya kuchosha kutoka Musoma - Arusha

Kumbe ni wengi wamekumbana na kadhia hiyo hapo mbugani!

Na mimi nielezee kiufupi kilichonisibu katika mbuga ya serengeti wakati nipo safarini kulekea arusha kwa ajili ya masomo.

Ilikuwa ni mara ya kwanza nasafiri kuelekea kwenye jiji la arusha ,nilipata tiketi yangu siku moja kabla ya safari na nililala karibu na kituo ili kuliwahi basi.

Alfajiri ilifika nikapanda gari pamoja na abiria wenzangu ,nakumbuka tulipanda basi la Serengeti liner tuliondoka majira ya asubuhi kama ulivyo utaratibu ila hali ya hewa ilikuwa ni masika kipindi hicho 2014 April, baada ya kuondoka tulisindikizwa na mvua hadi maeneo ya mugumu-serengeti kabla ya kukatika na sisi tuaendelea na safari ile hali kuna ubaridi na tope barabarani.

Tulifanikiwa kuingia kwenye mbuga ya serengeti salama na tulikaguliwa kwenye geti la kwanza na tukaruhusiwa ila maafisa jeshi waliokuwa eneo lile walimpa onyo dereva wetu kuwa kuna daraja kimefurika kama maji yatakuwa bado mengi tusivuke mpaka yapungue ,maana kingo za daraja zilikuwa hazionekani na pia daraja ni jembamba.

Nakumbuka vizuri daraja hilo lipo karibu na kituo cha pili (seronera hotel) tulika pale majira ya saa nne au saa tano kasoro,namkumbuka dereva yule walikuwa ni shemeji yangu na ilikuwa ni miezi michache imepita tangu aoe mdogo wangu (binti wa baba mdogo) Mungu amlaze panapositahili ,basi baada ya kufika darajani hapo kweli tulikuta daraja limefurika na kingo hazionekani na katika mto ule kulikuwa na tahadhali kwani pale ni maskani ya viboko,dereva alisimama na akasogea kwa tahadhari karibu na daraja wakati huo sisi tukiwa ndani basi,alikagua na alirudi na kusema maji ni mengi hatuwezi kuvuka.

Pale pale nilianza kuichukia safari na ikiwa ni mara ya kwanza naingia arusha na ilitakiwa nipokelewe na mwenyeji wangu nikawa ninawaza tukifika usiku nitalala wapi na maswali mengi lukuki.

Wakati tunaendelea kusuburi maji yapungue tulipewa taarifa kuwa mvua ni kubwa maeneo ya juu (yaani yatokapo maji) hivyo inaweza kuchukua muda mrefu hadi maji yapungue, tulikaa pale tukisubiri maji yapungue huku tuking'alisha macho yetu kwa kuwaona viboko wakipita eneo lile na wengine wakisombwa na maji maana maji yalikuwa na nguvu kubwa sana.

Punde walikuja askari wa wanyamapori na kutoa tena tahadhari ya kusuburi hadi kingo zionekane ndipo tupite kwani jana yake kuna gari moja ya seronera hotel iliyokuwa na watu wawili ikiwa na vinywaji ilisombwa na maji na watu wale kuokolewa.

Habari zile ziliniogofya sana nikawa naona safari ishaingia doa ,tulikaa hadi majira ya saa nane kama sikosei likafika gari lililokuwa linatoka arusha likikuwa ni basi la AM Dreamliner ,likiwa ng'ambo nyingine na sisi tukiwa ng'ambo nyingine tukiwa na subira ili maji yale yapungue ili tupite.

Maji yalizidi kuongezeka (abiria mmoja alimwomba dereva mpigie boss wake simu ili tubadilishane magari na tuendelee na safari kwani watu walikuwa wamechoka kwa kusubiri njaa nayo ikawa karibu nasi isivyo kawaida ,nakumbuka kuna jamaa alikuwa na samaki wa kukaanga kwenye buti aliwatoa na kuanza biashara pale (kufa kufaana ) aliwauza kwa bei ya aina yake japo wadogo wadogo ila aliza mmoja kwa shilingi 3000/=.

Mawasiliano kati ya dereva na bosi wake yalianza na kukukuwepo ugumu wa kubadilishana magari kwani basi la lililitoka arusha liliomba liongezewe pesa ili lirudi arusha maana safari ya kurudi arusha ilikuwa ni ndefu sana zaidi ya hili ambalo lilikuwa limetokea musoma.

Hatimaye mawasiliano yalifanyika kwa maboss wa makampuni yote mawili na kwa makubaliano yao walikubali tubadilishane magari (abiria waliokuwa wanaenda arusha wapande gari lililopo ng'ambo ya pili na abiria waliokuwa wanatoka arusha wapande basi lililokuwa linatoka musoma),najua utajiuliza tungepandaje magari hayo ile hali daraja limefurika maji (pembeni ya daraja lile kulikuwepo na daraja dogo kwa ajiri ya magari ya watalii ambalo ni jembamba na haliwezi kuruhusu basi kupita kwa wembamba wake,basi tulichukua mizigo yetu na tukavuka daraja lile kwa uoga na tahadhari maana tulikuwa kwenye maskani ya wanyamapori ,baada ya kupishana na abiria wenzetu waliokuwa na shauku ya kuingia musoma na sisi tukiwa na shauku ya kufika kule watakapo tulitakiana safari njema na tukapanda basi la Am dreamliner.

Mabasi haya yalikuwa na tofauti maana hili basi la pili lilikuwa sio zuri kama lile la kwanza kwani mwendo wake haukuwa kama ule wa basi tuliloacha ng'ambo ile ,baada ya abiria kuenea kwenye seat gari iligeuza na kurudi arusha na lile lingine likigeuza kurudi musoma huku dereva wa basi la Serengeti liner akigeuka moja kwa moja kwani toka hapo sikumwona tena hadi leo (alifariki baada ya kuugua kwa muda mrefu) tuliingia seronera na kula huku jua likiwa limening'inia nawakati huo sijui umbali uliobaki hadi kufika arusha,kwa njaa niliyokuwa nayo siku ile ilikuwa ya hatari maana usiku sikula na nilikuwa na mechi na mpenzi wangu hivyo nilijikuta nakutana na dhahama ya ajabu sana mbugani.

Baada ya gari kusimama na kuruhusu watu kula huku wakitaka watu kuharakisha sababu ya muda ,mimi niliingia dukani na kuagiza mkate mmoja na soda mbili za kopo,mkate ule ulikuwa wa 2000 na niliuchukua kama tutalala njiani basi nile hadi kesho yake, Tuliondoka nikiwa na mkate wangu huku simu ikilalamika betri haina moto na wakati huo mwenyeji kaniuliza nimefika wapi hadi kachoka.

Nilikula ule mkate na soda zile mbili na robo iliyobaki nikampa jirani niliyekaa nae ili nae aendelee na safari huku tumbo likiwa vizuri.

Jua lilizama tukiwa bado mbugani na kabla hata hatujafika kwenye geti la mwisho lililopo ngorongoro ,na kwa mujibu wa Maelezo ya konda wa basi alisema ni ngumu kuruhusiwa kupita baada ya jua kuzama ,majira ya saa tatu hivi tunafanikiwa kufika pale na baada ya ukaguzi na maelezo marefu tunapewa kibari cha kuendelea na safari kutoka pale mbugani na awamu hii tunashika barabara ya lami ila kutokana na mwendo wa gari bado tu hakukuwa na mabadiliko yoyote.

Simu inazima na bado sijafika arusha ,usingizi unanipitia kutokana na ubaridi na mvua iliyokuwepo usiku ule ,nakuja kushituka tunaanza kuingia ndani ya jiji la arusha mataa na idadi ndogo sana ya watu wakiwa kwenye mizunguko kwani tayari ilikuwa ni saa saba usiku.
Baridi lotr lilinipokea kwa furaha baada ya kufika na wakati huo sina sweta wala koti kwenye nguo zangu,nilishuka na tuliambiwa ambao hatuna sehemu ya kulala tulale kwenye ofisi za serengeti liner (kiukweli ulikuwa usiku wa ajabu sana maana nilipigwa na baridi hadi nikatamani kwenda kukaa kwenye microwave).

Usiku ule nilichaji simu yangu na asubuhi niliwasiliana na mwenyeji wangu akanielekeza tukutane wapi.

Moja kati ya safari ambazo sitazisahau yaani ilikuwa ni uchovu na baridi la kutosha,umenikunbusha mbali sana
 
We Jamaa lazima utakuwa Mwalimu tu, tena wa sekondari!!
Habari WanaJamvi Leo Napenda Kushare Nanyi kisa hiki cha safari Fupi iliyochukua muda mreeefu na kuchosha Miili ya Wasafiri.

Ilikua siku ya Tarehe 13 mwezi Wa 12 mwaka 2014 Kutokea Musoma mkoani Mara kuelekea Moshi Mkoani Kilimanjaro katika basi la Kampuni ya A.M the Dream liner

Nakumbuka wakati huo ulikua ni msimu wa Sikukuu za mwisho wa mwaka Na mvua kubwa. Na kutokana na Njia inayotumika haikuwa na lami na inakatisha katika Mbuga za Serengeti na NgoroNgoro hivyo kupelekea kusiwe na luxury bus inayoweza kukatisha anga hizo Na kufanya bus zote zinazopita maeneo hayo kuwa Ni Scania na Man pekee

Safari hii ilianza asubuhi na mapema mida ya saa12alfajiri tuling'atuka kutoka mitaa ya musoma mjini na kupitia abiria kadhaa stendi kuu Bweri., Na safari kuanza Rasmi kupita vijiji kadhaa.

Mwanzoni safari ilikua nzuri Tukishangaa vijiji na Mazingira ambayo Mimi binafsi nilikua mgeni nayo hivyo nilivutiwa sana na mazingira Yale kama Bunda, Nata , Isenye yalikua mazingira flan ya kupendeza japo yako mbali.

Safari ilianza majanga tulipokaribia Mugumu Serengeti kumbuka ulikuwa ni msimu wa mvua na barabara inakatisha mbugani haina lami na magari mazito kama basi yanapitapita hivyo kusababisha mashimo ambayo wakati wa mvua yanajaa maji na kusababisha usumbufu.

Njia imezibwa.
Kwa kuwa maeneo Yale ni karibu kabisa na mbuga hivyo tulianza kuona magari ya watalii na moja ya magari hayo lilinasa kwenye Matope na kuziba njia Na hapo ndo ukawa mwanzo Wa matatizo
Kwa mara ya kwanza kuona foleni pasipo Traffic Lights, wasafiri ambao safari yetu bado changa kabisa ilitubudi Tutoe msaada kuondoa gari lililonasa njiani ili kuacha nafasi ya kupita bus tuendelee na safari kwani tulifika maeneo Yale katika majira ya saa 3 asbh na kila mtu alikua na shauku ya kufika mapema aendako.
Tulifanikiwa Hatimae na safari ikaendelea lakini tulishapoteza kama masaa 2 pale kwa sababu kawaida ya wasafiri kupendeza hvyo hakuna aliyetaka kuchafuka kwa kuingia kwenye Tope lakini ilikua haina maana Tuishie pale hivyo ilibidi tujitoe japo Tuliwakuta askari wa mbugani lakini ilibidi Tungeze nguvu kufanikisha.

Safari Ikaendelea hatimae tukafika katika kituo cha kwanza Ikona Gate ambapo kwa utaratibu ni lazima wasafiri wanaotumia mabasi lazima wahesabiwe ili kuhakiki idadi yetu kabla hatujaruhusiwa kuingia Rasmi katika mbuga ya Serengeti na kujionea wanyama na mazingira ya kijani na Nyika za kuvutia
Ama kweli Tanzania ni sehemu Ya Eden jamani nilijisemea mwenyewe kimoyomoyo huku nikitabasam kwa kuona Twiga wengi tena kwa ukaribu kabisa wakijichanganya na Ngiri kadhaa.
Tulitembea kilomita kadhaa tukafika katika kituo cha pili kilichoitwa Seronela ambapo tayari ulifika mchana na hapo tulitakiwa kupata chakula cha mchana kabla ya kuendelea tena na Ngwe ya pili kumalizia safari yetu.

Tulikula na kunywa huku Tukijiselfisha na wenyeji wetu na mazingira mazuri na masafi ya mbugani Tena ilikua furaha sana kwa sababu Tulikuwa wengi mno kwenye lile bus na wengi wetu tulikua ni vijana Tulifurahia sana mazingira Yale kwani kwa nilivoona Mimi wengi wetu ilikua Mara yetu ya kwanza kupita mbugani tulitamani kama safari isiendelee tena lakini hatukujua Kama Bus lile lilisikia kilio chetu.

Baada ya kula, kunywa na kujiselfisha sana Hatimae muda Wa kuinza safari tena mchana ule ukawadia Tukajipakia tena kwa bus na mwendo ukaanza kwa furaha na kelele nyingi ndani ya bus Tukielezana sifa tofauti Tofauti za wanyama Tuliowaona. Tukiwa tumesahau yaliotupata asbh. Tukiwa bado na Tabasam la kuona wanyama na mandhari nzuri. Bado mvua ikitusindika kwa mbaali.....Bado Tukiwa tunaulizana muda na umbali uliobaki kumaliza safari yote haya yalifanya Tufarijike japo Tupo katika safari.

LaaHaulla!!!! Bus limesimama ghafla tena kwa kishindo kikubwa tena mvua ikiwa imechanganya na tumefika kwenye eneo LA nyika ambalo kwa mujibu Wa maelezo ya maafisa walituambia kuwa maeneo Yale ndio maskani kubwa ya simba tena ikifika mida ya jioni..Loooooh maafisa wanatuambia maneneo hayo ikiwa zimesalia dakika chache kufika saa 10jioni.
Kidogo mood ilikata sikutamani kuwa eneo lile tena kumbuka tena wakati huo mvua inanyesha baridi inapuliza kwelikweli.
Safari hii tena bus ilikataka difu na kusababisha kushindwa kuendelea na safari tena. na wale maafisa walitupa Yale maelezo wakidai kwamba tutafute sehemu mbadala ya kusubiri bus likitengenezwa au Tusishuke katika bus kwa kuwa tutahatarisha maisha yetu na lile eneo kumbuka ni Nyika tupu na eneo kubwa hakuna mti Wa kujificha hapo na maafisa walishaenda zao.

Safari ya Kuchosha.
Hapa ndipo tulipochoka kabisa kwani Dakika 40 baade walirudi wale maafisa walikuja na polisi pamoja askari Gemu kadhaa. Na ndipo ikaamriwa Turudi katika kile kituo cha pili ambacho ni Seronela wakidai kwamba ndio sehemu salama ya sisi kusubiri bus lile likitengenezwa na kwamba pale wabakie watu wachache tu wasioozidi 4 wengine wote turudi seronela na bus litakapotengemaa litatufuata tena seronela..Daaaah hakuna alieamini kinachoendelea kwa shingo upande Ilibidi kutii Amri kulinda maisha yako zikaletwa Cruiser za kutosha na sisi tukawa kama watalii tukiangaza huku na huko kwa nafasi zaidi kwani cruiser zile nyuma ziko wazi hivyo kufanya uweze kuangaza mbaaali zaaid kuliko ukiwa kwenye bus. Tukarudishwa tena Seronela pale ambapo tulitamani tusiondoke kidogo Tulikuta mabadiliko pia Nitumie fursa hii kuwashukuru wahudumu Wa Kambi ile ya seronela kwa ukarim waliotuonesha kwani tuliporudi tena Mara ya pili tulikuta Nyama choma ya kusaza tena wakatushauru ili kudhibit baridi mnapaswa kula sana Nyama na kuchangamsha mwili na wakati tunafika tena Seronela ilikuwa ni mida ya saa11 Nawashukuru tena wahudumu Wa Serengeti kwa kujali kwao watanzania Kwa mda huo mfupi tuliwezA kushiriki michezo kama Mpira Wa miguu mazoezi ya viungo.
Kumbuka ni wasafiri lakini ilibidi tubadilike kutokana na mazingira na wale maafisa walijitahidi kutuzoesha mazingira na kwakweli Tulitulia.
Baada ya Giza kuingia unajua Kule ni mbugani haifai kutembea usiku na kupiga kelele kwani baadhi ya wanyama hawapendi kelele hivyo tulikaa kwenye jengo moja kubwa jipya humo tukapata chakula cha kumalizia siku tukiendelea na stories mpaka majira ya SAA 7 usiku Bus liliporejea tena kutufata baada ya kutengemaa.

Usiku Wa manane bus linatengemaa toka jioni ya SAA 10 lilipo haribika na hii ni baada ya kuagiza difu nyingine kutoka Mwanza,. Kwa sababu ukilala mbugani lazima ulipie na sisi tulilipa 1500 ambayo ni ada ya MTU mmoja kupita Serengeti akiwa ndani bus hivyo hatulipa ada ya kulala pale na vile walivyotufanyia ni kwasababu tulikua wengi na hatukukusudia kulala pale hivyo ikatulazimu kwa kuwa bus liko sawa sasa na Tukaruhusiwa kuendelea na safari usiku huo

Njiani Mbugani usiku
Amini usiamini kuna wanyama hawalali kama Ngiri, punda miria, Fisi, Mbogo, na wengine Tuliendelea kuwaona wakirandaranda mbugani usiku.
Tumekwama tena
Wakati tuko pale seronela mvua iliendelea kunyesha lakini kwa kuwa tulikua pale kamp hatukuona madhara yake lakini tulipokua safarini tena usiku ndio tuliona madhara ya ile mvua kwani ilijaza mito na kuifanya icheue na kusababisha kuziba baadhi ya madaraja ya chini yaliopo Serengeti.
Tulikwama tena kwa sababu njia ya kupita ambayo ni daraja LA chini ilijaa maji na kuwa njia ya maji na kufanya Kingo znazoonesha mwsho wa daraja kutoonekana ikatulazimu tusubiri tena mvua ishe ili maji yapungue pale kwenye daraja na njia ionekane.
Tulisubiri eneo lile mpaka saa11alfajiri kutoka saa9 usiku ndipo maji yakaanza kupungua na Kingo za daraja zikaonekana lakini licha ya maji kupungua bado speed yake ilionekana kubwa.
Ilibidi sasa tumtafute mtu Wa kupima ile speed ya maji kama itafaa kwa bus kupita.kulikuwa na wanawake kwa bus hawakuamini kabisa mwendo Wa Yale maji na ndio walifosi itafutwe namna ya kuyapima kama tutapita salama.
Nitumie Tena nafasi hii kuwapongeza vijana Wa kimasai waliothubutu kuhatarisha maisha yao kwa sababu ya watu wengine kwani wao ndio waliopima speed ya maji kwa kwenda wenyewe kukanyaga sehemu tulizohisi ndipo Kingo zilipo tuliwafunga kamba kiunoni na walifanikisha kazi Hatimae tukapita salama na kusaidia pia magari mengine madogo ya watalii ambayo yalitukuta eneo hillo asubuhi.

Bado Mvua ilituandama na hatimae tukafika katika mpaka kati ya Serengeti na ngorongoro na hapo pia kupita ilituchuku mda kidogo kwani hapo Daraja liliondolewa kabisa na maji hivyo kufanya shimo ambalo hakuna gari ingeweza kupita lakini hapa tayari taarifa ziliwafika wakuu masaa machache baadae lililetwa daraja lingine na kupachikwa pale hatimae napo pia tukavuka salama japo muda ulishatutupa mkono kwani ilikuwa inaelekea saa tano asbuhi Siku ya pili.

Faraja yarejea.
Baada ya kuvuka mpaka na kuingia ngorongoro sasa kidogo tukaneemeka.kwa Mara ya kwanza namuona tembo katika mabonde ya ngorongoro tena kwa mbali nashangazwa na ukungu uliofunika creta kidogo tena natabasam natoa simu yangu nachukua kumbukumbu bus inasimama kidogo kupisha gari nyingine.
Barabara za ngorongoro ni za hatari kidogo umakini zaid unahitaji kupita zipo nyembamba zimetanda ukungu na zimezunguka mlima.
Tukiwa bado tunaishaa ngorongoro ghafla tena tunasikia sauti za watoto wa kimasai wamejichora usoni wakitutakia safari njema.

Hatimae.
Hatimae tunaitoka salama ngorongoro yenye creta na tunafika getini tunapewa nafasi tena ya kusafisha viatu vilivyo na tope kuosha mwili kwa wenye waToto na kujiweka tena sawa kwani sasa Tunaingia kwenye lami.
Watu wanashusha pumzi na kuangalia tulipotoka tunajiliwaza na Rosholoo kwani hatukutaka kusimama tena mpaka tufike tuendapo.

Yamungu mengi jioni ya tarehe 14mwezi Wa 12 mwaka 2014 Hatimae tunafanikiwa kuingia Arusha mjini salama kabisa lakini tukiwa wachovu wa mwili.
Asili ya watanzania ni ukarimu kama kawaida Tunashuka kwenye basi tunapeana pole kila mtu anachukua njia yake na Mimi kwa umakini Wa hali ya juu nakamata chombo nyingine sasa ni luxury kuelekea moshi mkoani Kilimanjaro katika ujenzi w taifa hili Tanzania.

Wito: kwa vijana wenzangu wasafiri ni vyema Kujiandaa kisaikoloji kwa lolote hii itasidia kurelax pale litakapotokea tatizo na kuweza kuwa msaada kama kijana .

Msafiri93

hiyo story yako inafanana na yangu ilikuwa ni 2007 January ila sisi gari liliaribikia maeneo hayo hayo mida ya saa sita na kifaa walisema arusha ndio karibu bahati nzuri kuna Kia ya wachina wakijenga hotel tulipata lift kwa 5000 hadi karatu nililala karatu asubuhi niliendelea na safari
 
Pole sana mkuu
 
Ikona gate = ikoma gate
 
Hongera kwa adventure hiyo broo, halafu kuna Mapimbi wengine Serikali inataka kuweka LAMI hiyo barabara ili kukuza Utalii na kurahisisha Usafiri kati ya Musoma na Arusha wanakuja na Vi NGO vyao kuzuia hiyo barabara. Tuache kutumika na WAKENYA jaman! Wakenya wanaogopa hiyo barabara ikipigwa Lami watalii watawakimbia msimu mzima wa mwaka, badala ya kuzuiwa kipindi cha mvua kama ilivyo sasa. Serikali yetu acheni kuhangaika na Wasalti wanaofadhiliwa na Kenya ili kupinga hiyo barabara kuwekwa lami.
 
Back
Top Bottom