Daktari wa Meno
JF-Expert Member
- Sep 5, 2019
- 509
- 1,617
Safari ya kipekee iliyoteka hisia zangu..
Safari ilianza saa 10 usiku kutoka nyumbani hadi eneo la kupandia gari, niliamka na kujiandaa tayari kwa safari na nikachukua baiskeli ambayo nililipa shilingi 400 kutoka nyumbani. Usiku wa saa kumi naaga familia yangu Mama na wadogo zangu naenda Dar kusaka maisha na wote wananipa baraka zote, nawatazama mbuzi na kondoo bandani wananipa sana simanzi machozi yananilenga kwa namna ambavyo ufugaji ulivyo unaendelea pale nyumbani bila msaada.
Natazama nyumba ambayo wanafamilia wanakaa nashindwa kuzuia hisia zangu machozi yanapita, kwa vile ilikuwa usiku hakuna aliyegundua kuwa nalia ila sauti ilibadilika na nikaanza kuguguma na kuaga wanafamilia wangu, Mama ananishika bega ananiambia kijana wangu maisha ni sarafu yenye pande mbili irushe kadri uwezavyo itakupa matokeo unayoyataka.
Wanaingia ndani nikiwa natafakari maneno ya mama na mlango wa debe unafungwa na hatimaye nuru ya kibatari inapotea mle ndani nikajua tayari wamelala katika vitanda visivyokidhi mahitaji kutafuta usingizi wa asubuhi. Napanda baiskeli nikiwa na kumwambia jamaa aliyekuwa anaendesha tuanze safari yenye takribani kilometa 20. Baridi la asubuhi linatua katika kifua changu ambacho kilikuwa kibovu na mara naanza kutetemeka isivyo kawaida huku kukizidi kupambazuka na sauti za ndege na wadudu zinaingia katika ngoma ya masikio yangu huzuni inajaa moyo nakuwa na majonzi yasioelezeka yamesababishwa na kipi.
Saa 12 kamili nafika eneo mahususi na kusubiri gari na dakika chini ya 10 linafika likiwa na abiria wenye hali mbalimbali, walikuwepo wazee, watoto, wanawake na vijana ila kila mmoja sura yake ilieleza kilichopo moyoni mwake.
Begi langu mkononi likiwa na nguo zisizo na maana kwa wengine ila kwangu ni nguo muhimu zaidi nikalishika na kutoa kipande cha mhindi wa kuchoma katika begi na taratibu nikaanza kutafuna huku gari likizidi kwenda. Miti ikarudi nyuma nami nikarudisha mawazo nyuma na kuanza kukumbuka familia yangu, mifugo na mazingira yasiridhisha nafsi ya mwanadamu yeyote yule hapa duniani. Njiani naona makazi na watoto wenye kupungia mkono basi huku wakiwa vifua wazi na mkono mmoja wakishikilia kaptula zao ili zisishuke chini.
Jua linachomoza na miale inapiga paji la uso wangu kidogo napata ahueni na kifua kinakuwa sawa, ndani ya nafsi naimba nyimbo za kilugha.
"Kat'a ka ongegoo, Nyasae biro konya.
Kat'a ka ginyiera abiro yudo ambe kendo mang'eny.
Nyasae telinha, telinha, telinha, jowa.
Abiro dok dala, dala waa kendo dala maber"
Wimbo ulikuwa unaendelea katikati nafsi yangu nikiwa naendelea kutafakari Dar es Salaam nitakuwa nani na nitaisaidia vipi familia yangu iwe katika kiwango japo cha kati kama si kiwango kizuri.
Mchana ukafika na ulikuwa muda wa kula nikitazama saa ni saa 8 mchana nikamuuliza jirani yangu bado sana kufika Dar akasema ni mara yake ya kwanza kwenda Dar hivyo hajui, nikamuuliza baba mmoja niliyeona huwenda akawa ni mwenyeji wa safari za Dar akasema tutafika usiku sana na hata robo ya safari bado. Nikashusha pumzi na kukumbatia begi langu na kuinamisha kichwa pale huku mwili ukianza kuhisi uchovu wa safari.
Miguu ikazidi kuwaka moto na kuamua kuvua kiatu changu cha Cossovo ambacho nilikuwa nimevaa na kuvifunga kamba kwa kuvishikanisha ili visipotee, miguu ikapata hewa na safari ikaendelea katika nyika isiyo na ukomo katika mboni za macho yangu. Viatu vile ndivyo nilikuwa natumia katika shughuli za kilimo pale nyumbani hivyo hazikuwa na usafi wa kutosha na ndani ya basi wakaanza kuvuta hewa isiyo ya kawaida, kwa mbali nikiwa katika usingizi nikasikia sauti ikisema vaa viatu vinanuka. Vaa viatu vinanuka sauti ikajirudia na nikaamshwa na mkono uliotikisa bega langu la kulia. Nikafungua kamba na kuvivaa vile viatu ambavyo vilionekana haviko katika usafi wa kukidhi.
Nilitoa kipande cha mhindi wa kupika ambao mama aliniandalia katika safari na kuula japo ulikuwa umeanza kupata utelezi ila kilikuwa ni chakula bora sana kwangu kwani kilipikwa na mwanamke ambaye alikuwa anahangaika juu yangu, hivyo sikuona ajabu kula mhindi ule. Safari ikaendelea na jua likaanza kuning'inia sauti za ndege zikarudi kutawala jioni ile na mara milio ya bundi na fisi ikazidi kusindikiza safari yetu. Ndani ya basi ulitawala ukimya ila sauti za minong'ono zilisikika kwa wale ambao walikuwa wakiendelea kuteta mambo yao..
Saa 2 usiku kondakta akaanza kutangaza vituo vya kushuka abiria nikajua tayari nitakuwa nakaribia kufika Dar, hivyo nikajiandaa kumpigia simu mjomba kutumia simu ya abiria mmoja niliyekuwa nimeongea naye na akakubali kunisaidia simu hapo baadae. Nilipaza sauti nikasema konda nashuka Ubungo, dah!! Umati uliokuwa mle uliibua kicheko na sikujua kwa nini ila baadae nikagundua tulikuwa mbali sana na Dar es Salaam na ingechukua masaa manne kufika.
Nikaendelea na safari na majira ya saa 6 usiku nikaanza kuona taa zikiwaka na majumba mazuri yaliyojengwa pembeni mwa barabara nikajua Dar es Salaam ni hii na sasa nikakaa mkao wa kuchunguza vizuri mazingira yake. Magari yalikuwa mengi isivyo kawaida sikuwahi kuona katika maisha yangu, kelele za watu zilizidi nje ya gari wakiongea kwa lugha nzuri ya Kiswahili tofauti nilivyozoea na muziki ukasikika nje ya basi. Hatimaye gari linaacha njia na kuingia stendi ya Ubungo ambapo pia niliona magari mengi mithili ya mifugo ambayo huwa naona katika mboni zangu niwapo nyumbani.
Nilichukia simu na kumpigia mjomba wangu "Jomba yooo asegik kaa tim piyo kik gikwalina" nilimaanisha mjomba nimeshafika fanya haraka nisije nikaibiwa. Akachukua simu yake nikaendelea kushangaa uzuri wa Dar ambao ulikuwa zaidi ya London niliyoona katika sinema kule kijiji miaka ya nyuma.
Itaendelea...
Safari ya Dar es Salaam II.
Baada ya kufika Ubungo na kumpigia simu mjomba aje kunichukua nilikaa kusubiri mwitikio wake nikiwa nimeshikilia kwa umakini mfuko wa nguo niliobeba ambao bado haukupungua thamani kila nilipokuwa nautazama. Pilikapilika zikawa zinaendelea pale stendi magari yakiendelea kuingia kutoka maeneo mbalimbali.
Sikusogea mbali na basi nililopanda nilikaa jirani na mwendo kama wa saa moja nilikuwa bado sijaona mjomba, nikaendelea kuvuta subira nikiwa kimya, kiu ya maji katika koo langu na hakuna kitu chochote kwenye mfuko ambacho kingetuliza njaa niliyokuwa nayo usiku ule, baada ya muda nikaona kondakta wa ile basi akija mbio na kuniuliza majina yangu nikamwambia naitwa fulani kwa uoga ila sikuogopa sana kwa sababu nilikuwa naye tangu safari inaanza. Akaniambia kuna mtu anakutafuta yupo kwenye jengo la wageni, nilimwambia sijui hilo jengo lilipo akanionesha na taratibu nikawa naelekea kule huku nikichechemea hii ni kwa sababu nilivaa viatu kwa muda mrefu.
Nilifika katika lile jengo nikiangaza ghafla nikasikia naitwa jina la kilugha nikageuka na kukutana na mjomba wangu, nilifurahi sana kupita maelezo. Miaka zaidi ya 3 sikuwahi kuonana naye tangu atoke kijijini na sasa tunaonana Dar akiwa amenawiri zaidi ya kipindi kile cha mwisho naonana naye. Mjomba alikuwa vizuri kiuchumi kutokana na biashara zake za uuzaji wa vifaa vya umeme hivyo alikuwa na pesa na maisha ya kuridhisha. Nilikaa ndani ya gari lake na mfuko wangu na tukaondoka nikiwa sijui Mashariki ni wapi wala Kaskazini ni wapi.
Baada ya muda tukafika kwake nikiwa mchovu sana kuanzia mwili na akili. Makaribisho yakafanyika nikaingia ndani japo miguu ikianza kutoa harufu kali nikaona kumaliza hili niombe maji nioge, nilipewa maji nikaoga na kula chakula ambacho sikujua kama ni cha mchana ama usiku kwani safarini nilikuwa nakula mahindi aliyoniandalia mama siku moja kabla ya safari.
Baada ya kula nilioneshwa chumba cha nje ndicho kitakuwa chumba changu nikaingia kulala, kabla sijalaza mwili wangu niliomba kushukuru Mungu kwa safari salama pia nikimsihi awe pamoja na familia yangu kule kijijini kila kiutwapo leo. Japo sikuwa na shuka ya kujifunika nililazimika kujifunika ngumi na mateke usiku ule, usingizi siku hiyo ulinitafuta wenyewe na nililala nusu nikiwa marehemu nusu mzima.
Majira ya saa 1 mlango unagongwa na kufungua nakuta ni mjomba akinijulia hali na kuniaga kwenda kazini, baada ya mazungumzo kidogo nikaendelea kulala hadi saa 4 nikaoga na kunywa chai. Kijijini chai mara nyingi huwa ni uji na sio lazima unywe kuna muda unaukosa hivyo unalazimika kusubiri mchana ule chakula cha mchana.
Ugeni wa Dar ulinifanya niwe mpweke sana nikatamani ningekuwa nyumbani malishoni na mifugo yangu, sikuwa na mtu wa kuzungumza naye kwani mjomba alikuwa na dada wa kazi pale kwake mkewe aliitengana naye na watoto walikuwa wakisoma shule za bweni hivyo pale nyumbani tulikuwa watu watatu pekee.
Jioni akarudi mjomba nikaongea na mama na wadogo zangu, wakati maongezi yakiendelea nilikuwa nasikia kengele ya ng'ombe wetu zikigonga, ni huzuni sana muda mwingine ila hatuna budi kushukuru Mungu kwa uhai maana hayo mengine hutupatia kwa wakati muafaka.
Siku zinaenda sasa utafutaji wa ajira ukaanza rasmi baada ya kuzoea hali ya Dar, nikaanza kuzunguka na mjomba mjini akinionesha watu wanavyofanya kazi pia akinionesha biashara zake na miradi mingine.
Wakati ujao nitakuja kusimulia kwanini mjomba hakutaka niwe daktari, chanzo kulikuwa nini!!.
Asanteni.
Sent using Jamii Forums mobile app