Safari ya Ban Ki-moon nchini Zambia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Safari ya Ban Ki-moon nchini Zambia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yericko Nyerere, Feb 26, 2012.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,206
  Likes Received: 3,771
  Trophy Points: 280
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewasili katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka kwa ajili ya mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo.
  Katika safari hii Ban Ki-moon alipangiwa kukutana na Rais Michael Chilufya Sata wa Zambia na kuhutubia Bunge la nchi hiyo. Vilevile Katibu Mkuu wa UN atahudhuria katika kikao cha ustawi wa sekta ya utalii ya Zambia.
  Baada ya kuwasili Zambia jana, Ban Ki-moon alipongeza mwenendo wa demokrasia nchini humo na kuelezea matumaini kwamba nchi hiyo itapiga hatua kubwa zaidi za kuelekea kwenye maenedeleo na ustawi.
  Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Zambia Kani Wignaraja ametoa taarifa akisema kuwa serikali ya Lusaka imefanikiwa kwa kiwango fulani katika kuboresha hali ya kimaisha ya raia wake. Amesema miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na ustawi wa kiuchumi, kuitisha uchaguzi huru na wa amani na kutimiza baadhi ya malengo ya milenia.
  Rais Michael Sata wa Zambia ambaye ni kiongozi wa chama cha Patriotic Front (PF) alimshinda mpinzani wake Rupia Banda katika uchaguzi wa rais uliofanyika Septemba mwaka jana. Kaulimbiu kuu ya Sata maarufu kwa jina na "King Cobra" katika kampeni za uchaguzi ilikuwa ni koboresha hali ya uchumi na kupambana na uhaba wa chakula na nishati. Vilevile aliahidi kusaidia raia maskini na kutazama upya shughuli za makampuni ya kigeni nchini Zambia ambayo mengi ni ya Kichina.
  Licha ya kwamba katika kipindi cha utawala wa Rupia Banda uchumi wa Zambia ulikuwa na kustawi kwa kasi ya kuridhisha, lakini kiongozi huyo hakufanikiwa kupata kura za kutosha kumshinda mpinzani wake katika uchaguzi uliopita. Hata hiivyo hatua ya rais huyo wa zamani wa Zambia ya kuitisha uchaguzi huru na kukubali kukabidhi madaraka kwa njia ya amani ilipongezwa mno na jamii ya kimataifa.
  Ripoti zinaonyesha kuwa uchumi wa Zambia unastawi kwa kasi ya kuridhisha katika miaka ya hivi karibuni. Pato jumla la Zambia katika mwaka 2010 lilistawi kwa asilimia 6.6 na inatazamiwa kuwa kiwango hicho kitaongezeka katika mwaka huu wa 2012. Serikali ya Zmbia pia imeanzisha mchakato wa marekebisho ya kimsingi na hatua za kujaribu kuwavutia wawekezaji zaidi wa kigeni. Hata hivyo utekelezaji wa hatua hizo za serikali ya Sata unakabiliwa na matatizo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa rasilimali za kutosha, riba kubwa ya mikopo ya taasisi za kimataifa, urasimu na sheria zisizokuwa na uwiano katika sekta mbalimbali za nchi hiyo na kadhalika.
   
 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Cha muhimu hapo ni Cobra kuwa makini na hao wapambe wa US
   
 3. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,541
  Likes Received: 2,237
  Trophy Points: 280
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Mbona hakuja Bongo au kwavile kamtema Asha Rose?
   
Loading...