Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,760
WaTanzania wengi wana hamu ya kuona CCM inaondoka katika kipindi wakiwa hai,wanataka kushuhudia tukio hili kuu likitokea.
Kwa miaka kadhaa unapofanyika uchaguzi mkuu ,wimbi la kuiondoa CCM limekuwa likiongezeka na waliowengi wakiongezeka katika kupiga kura ya kuiondoa CCM madarakani ,hilo halina ubishi ,vyama vya siasa upande usio madarakani vimekuwa vikikua kwa kasi ya ajabu na kuzidi kuongeza idadi ya Wabunge ,uchaguzi hadi uchaguzi.
Uchaguzi 2015 ni wakti ambao kwa mara nyingine jitihada za kuiangusha CCM zitafanyika ,na mara hii uchaguzi utakuwa mgumu kwa CCM na rahisi kwa vyama vya upinzani ,na CCM wanalijua hilo ndio maana tunamuona Kinana yupo kijijini kukifufua Chama ,anachokipata huko ni lawama tu ,serikali yake haijasifiwa hata sehemu moja ,huko kunamaanisha Serikali ya CCM haijamtendea kitu mwananchi katika kumuondoa na umasikini na badala yake imekuwa ikimzidishia matatizo.
Tumeona ni jinsi gani CCM wameiba kwenye kuipitisha Katiba,hakuna kura za mahujaji wala walio India ,maana ukweli ulioenea ni kuwa Ubalozi wa Tz Nchini Saud Arabia ulikataa jukumu la kuwapigisha kura mahujaji kwa sababu za kiusalama ndani ya Saudia ,Sita alidanganya Umma wa waTanzania.
UKAWA ni lazima waanze kuonyesha dira ya kuungana kuanzia sasa katika safari ya kuelekea Uchaguzi mkuu ,kama watakubaliana kuweka mgombe mmoja kwenye nafasi ya Uraisi ,nafasi za wabunge pale kwenye sehemu ambazo kuna kiti cha miccm ,zaidi zile sehemu zenye mbunge wa CCM ni lazima vyama hivi viungane kuweka mgombea mmoja dhidi ya CCM ,waunganishe nguvu zao sehemu hizi na kuhakikisha waccm haifurukuti.
Mwisho kuidhibiti tume ya Uchaguzi na kututangazia matokeo ya uwongo hayanayo kupitia hii tume ndio yanayomwangamiza mwananchi.