Safari bado ni ndefu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Safari bado ni ndefu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Jul 20, 2010.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Jk alipo ingia madarakani mwaka 2005 mimi ni mmoja wa watu walio kuwa na matumaini makubwa sana na awamu ya tatu. Labda ilikua ni utoto. Labda kama wengine nili bumbuwazwa na ujio wa "raisi" kijana. Sidhani kama JK kafanya vibaya saaana ukilinganisha na waliomtangulia bali kwa matumaini watu walio kuwa nayo ilikua vigumu sana kuridhisha wapiga kura wake. Kuna nukuu ya kisiasa inasema "Promise little, deliver more." Mheshimiwa kafanya kinyume na kuahidi mengi na kufanikisha machache.

  2007 Edward Lowassa alipo jiuzulu pamoja na mawaziri wawili mimi pamoja na utoto wangu tena nikasema demokrasia Tanzania ina panuka na ipo siku ina karibia tuta kuwa na nchi yenye vyama walau viwili vinavyo pokezana madaraka. Mimi ni mshabiki wa CCM tokeo nilipo kuwa mtoto lakini kwa jinsi ninavyo kuwa naamini kabisa it is in the best interest of Tanzania to have a strong opposition. Nikasema sasa viongozi wameanza kuwa jibika na nikasema sasa vyama vya upinzani vita tumia nafasi hii kujiimarisha lakini ah wapi. Siyo siri kwama tungekua nchi iliyo komaa kidemokrasia na wananchi wanaojua wajibu wao basi CCM isingeweza kushinda uchaguzi huu lakini kwa muonekani wa mambo CCM inaelekea kwenye ushindi tena.

  Kelele zoooote za mabadiliko zilizo pigwa JF nika jiaminisha kwamba sasa Watanzania wame badilika kifikira na kimawazo. Nika sahau kwamba Tanzania ina wananchi milioni 40 wakati JF ina members takriban elfu kumi na mbili na kitu. Kumbe mawazo ya wengi JF hayaonyeshi uhalisia wa mawazo ya wananchi wa kawaida.

  Naamini safari bado ni ndefu sana na hadi siku zinavyo sogea ndivyo ninavyo amini kwamba mabadiliko Tanzania hayata letwa na kizazi kilicho zaliwa wakati wa uhuru bali sisi watoto wao. Kadri muda unavyo kwenda ndivyo nianvyo zidi amini kuwa vijana makini na wenye uwezo wana takiwa kuonyesha utashi wa uongozi si kwenye siasa tu bali kwenye vitengo mbali mbali vya serikali, mashirika ya umma na biashara binafsi. Nasikitika kusema kwamba baba zetu mme tuangusha vijana wenu tuliyo tegemea mtatuachia Tanzania iliyo bora zaidi kuliko ile mlioachiwa nyie.

  2010 ndiyo hiyo. CCM ita shinda kwa kishindo. Hamna chama cha upinzani kita kacho jitokeza kama upinzani wa kweli. Wazee wataendelea kung'ang'ania madaraka na wale vijana wachache wata kao bahatika kushika uongozi wengi wao ni wale ambao wata wekwa na wazazi wao ili kulinda maslahi ya familia zao na si taifa. Kati ya 2010-2015 tutaendelea kupiga makelele yale yale lakini tutaendelea kuwa taifa la wapiga kelele walio na utendaji sifuri.

  2005-2010 we have talked the talk but we have failed to walk the walk. Nime poteza matumaini na 2010-2015. Nimejiandaa kusikia maneno yale yale kutoka watu wale wale. Tofauti ni kwamba kati ya 2010-2010 nita toka kwenye vijana wanachuo na kuingia kwenye kundi la vijana wanaofanya kazi. Ni matumaini yangu kuifanyia kazi serikali hiyo hiyo na kuacha kuwa muongeaji na kuwa mtendaji. Nchi ni yetu, uamuzi ni wetu.
   
Loading...