Safari bado; Mene mene tekele na peresi

Safari bado; Mene mene tekele na peresi

JM inc

Senior Member
Joined
Apr 27, 2013
Posts
114
Reaction score
54
MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI.

MENE-Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha.

TEKELI-umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka.

PERESI- ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi.

haya maandiko yanapatikana katika kitabu cha biblia AGANO LA KALE... mfalme Belshaza alijiona ni mkuu akajiona ufalme wake hakuna mwingne atakayekuja mbele yake na hakuna mwngne akasahau kuwa safari inaendelea.

Mwisho wa mfalme Belshaza ulikua mbaya, na hii ilitokana na kulewa madaraka akamkosea Mungu, Mungu alichukizwa na hili jambo akaamua kumuadhibu.

Tunao wafalme weng siku za leo ambao wanafanana na utawala wa Mfalme Belshaza, kupata nafasi wanadhani wamefika, wanaona hakuna kama wao, wanasahau walipotoka.

Wafalme wa leo wenye kufanana na Belshaza nawakumbusha tu, cheo kisikubadilishe ukaisahau jana yako na kuibaki kuikumbuka leo yako, maana utakuja kuijutia kesho yako. Cheo ni dhamana.

Mfalme Belshaza ni funzo kwetu, wako wapi watawala wa zamani waliowahi kuitikisa hii dunia?... wako wapi matajiri wa kale?... Hakuna ajuaye kesho yake, unaweza kulala kiomgozi leo kesho mambo yakabadilika, TUSIBADILISHWE NA LEO YETU.

Cheo chako kisiondoe utu wako.... tusilewe madaraka, madaraka yasitulevye, safari bado inaendelea kuna maisha baada ya uongozi...
 
Joseverest samahani lakini.


Tume huru idaiwe mapema ccm itoke vinginevyo watanzania mtapata tabu sana
 
Ukiona shetani anampinga shetani mwenzake basi jua kuwa ufalme wa kishetani unakwenda kusambaratika
 
Back
Top Bottom