Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 57,913
- 133,926
Tofauti ya Mbowe na Yuda ni ndogo sana
Na Saed Kubenea
FREEMAN Mbowe, aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa miaka 21, hawezi tena kuaminika.
Taswira aliyojijengea tokea Januari mwaka huu, aliposhindwa kutetea wadhifa wake wa uenyekiti, inamuonyesha kuwa ni mbinafsi, amesheheni visasi, chuki, msaliti na msahaulifu.
Hapa aweza kuzungumza hili, pale akazungumza lile. Amekuwa wa kubadilisha kauli na kuzalisha migogoro.
Hana tofauti na Yuda Iskariote, aliyetumia alama ya busu – ishara ya amani – kuwaonyesha maadui mahali aliko Yesu ili wamkamate.
Katika uchaguzi huo, uliokuwa huru na haki, Lissu alipata kura 513 (sawa na asilimia 51.5) dhidi ya kura 482 (asilimia 48.3), alizopata Mbowe.
Akizungumza baada ya kushindwa uchaguzi, tarehe 22 Januari 2025, Mbowe alisema, mchakato huo, umekiacha Chadema na majeraha.
Alisema, “ijapokuwa uchaguzi umefanyika katika misingi ya uhuru, haki na uwazi” lakini mchakato wa kampeni umeacha majeraha na kuwataka waliochaguliwa kuyatibu kwa kuleta maridhiano.
Aliongeza, "Mimi niliahidi kama ningeshinda, ningeunda kamati ya ukweli na maridhiano, ili watu wazungumze na kutibu majeraha yaliyoletwa na kampeni.”
Alisema, “… sasa kama mnaniheshimu kama baba, basi nawaagiza Lissu na viongozi wenzako wapya, mlete maridhiano baada ya majeraha yaliyoletwa na kampeni."
Lakini muda mfupi baadaye, Mbowe akaonekana kutenda tofauti. Akabariki kwa njia ya kunyamazia, migawanyiko inayoweza kudhoofisha Chadema, kwa njia ya kutengeneza propaganda za Tanganyika na Zanzibar; ukabila, ukanda na udini, hadi kuzomoka na matamko na maandishi kwenye mitandao.
Karibu wote waliokuwa kwenye mradi wa kudhoofisha Chadema kwa njia ya kushambulia viongozi wapya, ili kuleta migawanyiko, wamekuwa wakijitambulisha au kujitanabaisha kuwa “vijana wa Mbowe.”
Baadhi yao, ndio waliotangaza kujiondoa Chadema na kujiunga na Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA).
Miongoni mwao, ni pamoja na Salum Mwalimu, Benson Kigaila, John Mrema na Catherine Ruge, viongozi wa sasa waandamizi wa chama hicho.
Kisa: Ni madai ya kutengwa na uongozi mpya wa Lissu, kufuatia kile wanachokiita, “kumuunga mkono Mbowe.”
Wakaendelea kutuhumu viongozi wakuu wa Chadema, kukataa kusaini kanuni za maadili na hivyo “kusababisha kuondolewa kwenye uchaguzi mkuu unaokuja na kuzima ndoto zao.”
Hakuishia hapo. Yeye na iliyokuwa sekretarieti yake ya Kamati Kuu – wakakacha vikao vya maridhiano - kilichoitishwa mjini Bagamoyo na viongozi wapya.
Hii ni baada ya Lissu na wenzake kuridhia ushauri wake, wa kufanyika vikao vya maridhiano. Wakadai wanahitaji muda wa kupumzika. Mpaka sasa yeye bado yuko fungate.
Kuna madai amegoma hata kupokea simu za viongozi wenzake, hasa Lissu, John Heche, makamu mwenyekiti na Godbless Lema, mjumbe wa Kamati Kuu.
Kamati iliyoundwa na mwenyekiti wake, kutafuta maridhiano ndani ya chama, ameinyima ushirikiano.
Hatua yake hii, imesababisha mpasuko zaidi, kuliko ilivyokuwa kabla ya kampeni za uchaguzi.
Waliokuwa wanajiita “timu Mbowe,” wakapata mwanya wa kutumika na watawala. Wakaanzisha genge ndani ya chama na kulipachika jina la G55.
Baada ya genge hilo kushindwa kuvuruga chama, wakatumika kufufua Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), kwa njia ya kukiteka na kujipachika uongozi.
Wakaendeleza madai yao kuwa Mbowe ametengwa na warithi wake. Hajawakana hadharani wanaotumia jina lake, kujitafutia uhalali.
Hajajitokeza kutetea msimamo wa No Reforms, No Election, kutetea chama na viongozi wake kwa ujumla, kwenye madhira wanayopitia.
Aidha, Mbowe aliwataka viongozi wapya kusimama na katiba na kujizuia kuwa na kiburi. Lakini anafanya tofauti na alivyowaeleza wajumbe wa mkutano mkuu.
Kuhusu mustakabali wake kisiasa, Mbowe alisema, anachukua likizo na ataendelea kujikita katika kufanya biashara zake na kuendelea kukishauri chama.
“Nimepewa likizo ya lazima, na nitaenda kwenye biashara zangu na nitaendelea kutoa ushauri kwa chama…Nashukuru nimepewa likizo hii kidemokrasia na katika mfumo ambao nimeujenga mwenyewe,” alijigamba.
Kauli ya Mbowe kuwa uchaguzi ulikuwa wa kidemokrasia, iliungwa mkono na Lissu baada ya kusema kuwa chama hicho kimeweka kiwango cha dhahabu cha demokrasia ya ndani na kuvitaka vyama vingine kuiga mfano huo.
Lissu alisema, uchaguzi ulikuwa wa wazi, huru na haki bila mizengwe, ingawa alikiri kulikuwa na misuguano ya hapa na pale.
“Tumefanya jambo ambalo halijawahi kufanywa toka chama chetu kianzishwe… tumeweka kiwango cha dhahabu – tunawaambia vyama vingine kama vinaweza viige," alieleza.
Lissu alitumia hotuba yake hiyo ya kwanza kama mwenyekiti, kumshukuru mtangulizi wake.
Alisema, Mbowe alichukua kjiti cha uongozi wa Chadema, kikiwa na wabunge watano na katika uongozi wake, amekifanya kuwa chama kikuu cha upinzani nchini.
Akaongeza, “Mbowe ndiye aliyefanikisha uchaguzi kuwa huru na haki na anastahili pongezi. Historia ya chama chetu itakapoandikwa, watatambua mchango wako huu mkubwa uliotoa.”
Mwenyekiti huyo mpya alisema, Mbowe hajastaafu na ataendelea kuwa mjumbe wa kudumu wa kamati kuu kama ambavyo katiba ya Chadema inavyoainisha.
Bali Mbowe hajasimama na kauli hiyo. Hajakishauri chama chake. Hajakitetea. Hajaonekana kokote kukisaidia kukabiliana na madhira inayokikuta. Hajakisaidia kukabiliana na maadui zake. Hata pale alipotafutwa na wenzake, inadaiwa amekuwa akiwakacha.
Hajahudhuria kikao chochote cha Kamati Kuu, miezi mitano tangu kushindwa kinyang’anyiro cha uenyekiti. Hata anapoulizwa juu ya ukimya wake, ameishia kusema, “…unataka niseme nini, wakati mimi siyo kiongozi.”
Mjumbe wa Kamati Kuu na mwenyekiti mstaafu, anashindwa kusema katika kipindi ambacho chama anachohubiri kuwa amekiasisi, kinashambuliwa kila kona?
Hata kama angekuwa mwanachama wa kawaida, hakupaswa kunyamaza. Kama ambavyo wengine hawajanyamaza.
Kwa mujibu wa Katiba ya Chadema, mwenyekiti mstaafu, ni mjumbe wa kudumu wa vikao vya Kamati Kuu, Baraza Kuu (BKT) na mkutano mkuu.
Vilevile, Mbowe hakuonekana kwenye operesheni muhimu iliyobeba ajenda ya No Reforms, No Election” – Bila Mabadiliko, Hakuna Uchaguzi.
Mvumo wa mabadiliko kwenye mifumo ya uchaguzi, ilianza kusikika baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024, wakati Mbowe akiwa kiongozi mkuu wa Chadema.
Maamuzi ya No Reforms, No Election, yalipitishwa kwenye vikao vilivyokuwa chini yake. lakini ameshindwa kuonyesha uongozi, hasa baada ya kutokea baadhi ya watu kupotosha ukweli.
Katika maeneo mengine, Freeman Mbowe alisema, “… kuna watu waliniambia nijitoe kwenye uchaguzi nitaadhirika, nikawaambia nitafia demokrasia."
Lakini demokrasia ipi anayoifia? Demokrasia ipi anayoihubiri, wakati anaruhusu chama chake kuhujumiwa na wanaojitambulisha kuwa watu wake?
Huwezi kujiita mwanademokrasia, wakati unaendeleza manung’uniko ya chini kwa chini; unabariki mifarakano na uchochea migawanyiko ya ndani kwa ndani. Haiwezekani.
Kama angekuwa anachokinena ndicho anachokiishi, asingenyamazia yanayoendelea. Angeshirikiana na viongozi wenzake kuihami na kuijenga upya Chadema. Kurejesha umoja na mshikamano; undugu na upendo.
Lakini kwa kuwa alilewa madaraka kwa muda mrefu, bado anajiona yeye ndiye chama na chama ndiye yeye (mtindo wa Augustine Mrema); na au yeye ni zaidi ya chama.
Kilevi hicho ndicho kinampa kiburi cha “kupinga maamuzi halali ya chama chake, tena nje ya vikao.”
Mbowe anajua taratibu za chama chake; kanuni na katiba. Anajua kuwa hata kama angekuwa hamaanishi kwamba No Reforms, No Election, siyo kuzuia uchaguzi – kama washirika wake wanavyodai – alipaswa kurudi kwenye Kamati Kuu, kufafanua alichokilenga.
Hastahili kupinga uamuzi huo mitaani kwa njia ya kunyamaza. Anapaswa kurudi katika chama. Ni kama ilivyo mahakamani; jaji au hakimu akitoa hukumu, huwezi kupinga barabarani. Unarudi kwenye mahakama ya juu kuomba ubatilishaji.
Mbowe anajua chama hiki, ndicho kilichomlea. Ndicho kilichomkuza na ndicho kilichompa jina. Ndicho kilichohamasisha wananchi nchi mzima kupinga uonevu.
Ndicho kilichompigania kwenye madhira yote yaliyomkuta, ikiwamo mashitaka ya feki ya ugaidi aliyofunguliwa na Jamhuri, kutoka tarehe 21 Julai 2021 hadi 4 Machi 2022.
Lakini kwa makusudi, ameona ni bora Chadema kisimbaratike na Cha Mapinduzi (CCM), kishinde kuliko chama hicho kushinda bila yeye. Anaonekana kuwa na nongwa.
Ndiyo sababu ya kukacha kuhudhuria vikao vya juu vya chama chake. Hata kimya chake cha sasa dhidi ya hatua ya serikali, kumfungulia mashitaka ya uhaini mwenyekiti wake na mmoja wa waliokuwa watetezi wake, imetokana na nyongo hiyo.
Alikwenda gerezani kumjulia hali, lakini hajatoa kauli yoyote inayokosoa uamuzi wa serikali wa kumfungulia mashitaka Lissu wala hajaonekana mahakamani.
Kwa wanaofahamu vema wanasema, Mbowe ni mtu wa visasi, chuki na choyo. Kwamba, wote waliowahi kushindana naye, kutofautiana naye kimawazo na misimamo ndani ya Chadema, wameishia kupewa majina mabaya.
Wengine wamefukuzwa kwenye chama. Wapo waliovuliwa uongozi na wengine kulazimika kuondoka, huku wakiwa bado wanaipenda Chadema.
Miongoni mwa waliondoka Chadema, wakiwa bado wanakipenda, ni pamoja na Zitto Kabwe, aliyekuwa naibu katibu Bara, mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya upinzani bungeni.
Wengine, ni David Silinde, aliyekuwa mbunge wa Momba na Tunduma; Anthony Komu, aliyekuwa mbunge wa Moshi Vijini na mkurugenzi wa fedha; Fredrick Sumaye, aliyekuwa waziri mkuu na mwenyekiti wa kanda ya Pwani na Wilfred Lwakatare, aliyekuwa mbunge wa Bukoba Mjini na mkurugenzi wa usalama.
Kwenye orodha hiyo, wapo pia Joseph Selasini, aliyekuwa mbunge wa Rombo, kaimu mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini na Kaimu Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni; Mwita Mwaikabe Waitara, aliyekuwa mbunge wa Ukonga na mkuu wa idara ya sera na utafiti.
Hata Prof. Abdallah Safari, aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Chadema -Bara, aliamua kujiweka kando kabla ya muda wake wa uongozi kumalizika. Orodha ni ndefu.
Yote haya yametokana na Mbowe kuendesha chama, mithili ya kampuni binafsi. Aliwaweka pembeni watu wenye uzeofu na kuanza kubeba “alioamini” kuwa watu wake.
Hata walipofanya makosa aliwanyamazia. Wakaishia kutengeneza makundi yaliyochangia anguko lake.
Mathalani, mwaka 2015, mmoja wa mshirika wake wa karibu, Halima Mdee, alimteua mlinzi wake kuwa diwani wa viti maalum, manispaa ya Kinondoni, bila kufuata taratibu. Akaondoa wanaostahili.
Mbowe akatetea na kusema, muacheni ameteua mwenyewe. Akaelezwa hiki anachokijenga, kitakuja kugharimu chama. Hakusikiliza.
Matokeo yake, miaka mitano baadaye, Mdee akajipeleka bungeni, kwa njia ileile aliyotumia kumpeleka mlinzi wake kwenye baraza la madiwani.
Alikuwa amejiaminisha kuwa yeye ni mshirika mkuu wa mwenye chama na hakuna wa kumhoji au kumfukuza.
Naye Ester Bulaya – mshirika mwingine wa Mbowe – akafanywa Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, nafasi aliyomvua Selasini.
Akazuia wabunge kwenda bungeni bila kuwashirikisha. Wabunge walipoomba kikao cha majadiliano, Mbowe akazomoka bila kusikiliza hoja zao na kusema, “maamuzi yaliyofanyika, yatekelezwe.”
Wabunge wakakatika vipande vipande. Wengine wakakaidia agizo la Bulaya la kutoingia bungeni. Wakafukuzwa uanachama bila kusikilizwa na bila kuwapo kikao halali cha kufikia maamuzi hayo.
Hatua hii ilizidisha mifarakano ndani ya chama. Kundi likaendelea kupanuka. Mwenyekiti akazidi kupoteza ushawishi. Akatuhumiwa kuendesha chama nje ya vikao.
Madai haya na mengine, yakawafikia hadi wanachama na baada ya kuona wamepata mtu sahihi wa kuwaongoza katika mapambano na kuwasimamia, wakaamua kumuweka kando.
mwisho.