Saed Kubenea: Ndumilakuwili mbobezi

Saed Kubenea: Ndumilakuwili mbobezi

Bahati nzuri kila uliloliandika nalifahamu na kuna mengi pengine huyajui au umeamua kutoyaweka wazi. Utabezwa, utapondwa sana humu, lakini huo ndo ukweli wenyewe. It's just a matter of time. Ukiwa na mahaba na kitu/mtu hatauambiwe vipi utaona ni uongo na uzandiki, lakini hakuna kitu kizuri kama muda.
Kweli kabisa mkubwa
 
kubenea ni msakatonge ambaye hajitambui anasimamia nini, makala zake nyingi zimekita kuwashambulia watu binafsi kwa maslahi binafsi.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Yule n sawa na demu aliekosa bwana.....

Anatangatanga tu kwa sasa taarabu zake
 
Mlolongo wa porojo lakini ushahidi hakuna , wewe ndio wa kupambana na kubenea ? Halafu ulisubiri usome makala ya kusaga msaliti ndio upate idea !

Kama nilichokisoma nimekielewa. Basi kubenea hapaswi hata kuwa mjumbe wa nyumba Kumi. Maana ni Tatizo
 
Ndugu wanaJF,

Kulingana na maneno ya misemo ya kiswahili kila mwosha naye huoshwa, ni dhahiri Saed Kubenea mbunge wa jimbo la Ubungo CHADEMA ameosha wengi na imefika wakati kaongeza CV ya ubunge mbali na uandishi wa habari za kikachero. Ninapopita kwenye vyombo vya habari anavyomiliki ninakuta muda mwingi ZITTO, ZITTO sijui huyu Ztto ni nani anayetrend kwenye vyombo vyake vya habari vya Mawio na mwanahalisi tu, kwa stori ambazo vyombo vingine havizioni kama ni habari na haviziandiki kwa kuwa ni uzushi na uongo wa kutungwa.

Ukiona Zitto ametajwa BBC, DW, Mwananchi,etc ni habari njema kwa Taifa akimwagiwa sifa kama mwanasiasa kijana wa mfano wa kuingwa, lakini ukisoma habari za Zitto mwanahalisi au mawio utashangaa hawa jamaa wao wanatoa wapi hizi habari au ndio ugonjwa wa chuki unaosemekana anaugua Kubenea? Kubenea inasemekana hauna vyeti vya shule kulingana na ulivyokuwa unajinadi wakati wa kampeni october 2015, nenda kwenye magazeti yako ya Mawio na Mwanahalisi uchapishe CV na utuoneshe vyeti vyako au tuma mtu hapa JF tujiridhishe tuhame mada.

Mwisho kabisha, nakushauri japo najua hauwezi acha tabia yako inayosemekana ni ya undumilakuwili leo Lowassa ni Fisadi mchafu asiyesafishika hata kwa dodoki na unasema una ushahidi lundo, kesho Lowasa sio fisadi ni msafi hahitaji hata kunawa kwa sabuni. Dr Slaa Rais mtarajiwa aliyeko mioyoni mwa watanzania kwa ubora wake kesho Dr Slaa ni hovyo msaliti wa mabadiliko. Ikiwa unashindwa kutumia akili ya vyuo vyako vya hapa na pale ulivyoongeza elimu ya juu India na kwingineko huko na kule, basi tumia hata ya Elimu ya chekechea tulikojifunza " Is it possible to hold three things in one hand?"

Inaaminika na kusemwa sana mwanamke hawezi tumikia mabwana watatu asiitwe kahaba. Uandishi wewe, Upelelezi wewe, uwakilishi wa wananchi wewe, uongozi wa propaganda za chadema wewe. Acha, acha kabisa kutaka kuongeza umaarufu kwa kukashfu watu weka CV zako Mawio na Mwanahalisi. Acha kabisa kuwadanganya watanzania kwa kivuli cha mwandishi wa habari uliobobea. Umetoka kwenye mstari umekiuka misingi ya uandishi katubu haraka iwezekanavyo.
 
Jana ulitolewa ushauri kwamba zitto aje mwenyewe..maana nyie anaowatuma hamjui kumtetea..
 
Kambi rasmi ya mkuu wa Wilaya na kiongozi wa chama kazini!!!
 
Mwami hii in ID ya ngapi? Ukiangalia trend ya uchangiaji wako kwa ID hii inaonyesha uliisahau
 
Jana ulitolewa ushauri kwamba zitto aje mwenyewe..maana nyie anaowatuma hamjui kumtetea..
Nani kakuambia sio mwenyewe? Unacheza na dogo wewe! Hii ndio style take ila safari hii kaingia choose cha kike
 
Kubenea naye katumwa kuwakilisha watu wake pale mjengoni. Mbona anawawasha sana.

Elimu ya Tanzania inayotambuliwa ni ya msingi. Si anajuwa kusoma na kuandika.

Wanaume wambeya mnaudhi sana.
 
Kubenea kubenea kubenea
Ikiwa hana shule anawanyima usingizi je angeingia darasa!!!!!!
Kubenea kumbe ni kichwa
 
Hii ni sawa na kumpiga chura teke teh teh teh ila umejitahidi kuweka mtiririko mzuri wa matukio kwanini usiwe mtunzi tu wa liwaya kuliko kujisumbua na watu maalufu kama Kubenea ?
Kwanini usiandika makala inayohusu maisha yako tukainjoy flava ?

Kwanini usiandike uozo wa serikali kama kubenea na kupata sifa lukuki kwa kulisaidia taifa ?

Kwanini usiandike Escrow kwa undani wake tukaelimika?

Kwanini usizungumzie umeme ambao umekuwa tatizo kubwa saana hapa nchini?


Kwanini usiandike maswala ya makontena angalau tukafahamu undani wake?

Kwanini usiandike matumizi mabovu ya vyombo vya habari kwa ujumla ili tukuone kweli unajua?


Yote hayo yapo na unayajua ila unafiki na ubinafsi na chuki zimekufanya umchafue kubenea

Kama tindikali ilishindwa sembuse wewe mchumia juani ?
 
Huyu kubenea ndio yupi jamani wekeni japo picha yake tumuone
 
Ila watu wa JF vigeu geu kama nini hao hao wanaopinga CV ya kubenea kuwekwa hadharani ndio walikuwa mstari wa mbele kuitaka CV ya Stella Manyanya mpaka wakawekewa ndio wakaridhika sasa sioni tatizo wekeni na ya kubenea hata kama ameishia la NNE kwani kuna ubaya gani? Na kila kitu kikiwa hadharani ndio itaondoa utata wa jina Halfan na so saed
 
Hizi ni kampeni za kuchafuana kuhusu uenyekiti wa PAC
 
ACT mnahangaika sana na Kubenea

sasa hiyo habari kama sio udaku ni nini?

hahahahahahaah....Upuuzi huu
 
Back
Top Bottom