Saed Kubenea - Mapendekezo ya Katiba Mpya

Saed Kubenea - Mapendekezo ya Katiba Mpya

Katika muda tutakao kuja kuujutia ndio huu..Inabidi tujitokeze au tukae chini toka ngazi za kifamilia kijamaa au hata majirani tuzungumze kwa pamoja nini cha kwenda kutoa maoni ya katiba
Niliwahi kushiriki semina ya kutaka mabadiriko ya katiba iliyofanyika Morogoro miaka kadhaa iliyopita leo hii nasoma na kujionea baadhi ya Watanzania wenzangu nusu wanajitokeza kuchangia mabadiriko ya katiba wengine hata mpango hawana
Jamani naomba tukipata wasaa twendeni tukatoe maoni yetu...
Tukumbuke hii nchi haikupata rais mwendawazimu laiti ingepata na ile hii katiba ya zamani tungelia na kusaga meno
 
bila mwanahalisi hatuwezi kuyajua maovu ya watawala.tupe updates mitandaoni tujue hatima ya mwanahalisi,sijaona muundo wa bunge na nguvu ya kura ya wapinzani hata wakiwa wachache.jamaa watalitumia bunge vibaya kama litapewa mamlaka makubwa bila kuhojiwa.
 
maoni ni mazuri lakini je hawa wakuu watakupitisha kweli mambo yanayowaba wao
 
Katika bunge kusiwepo viti vya upendeleo kwa wanawake bali utaratibu uandaliwe utakao ondoa sababu zinazowafanya wanawake waogope/washindwe kugombea kwenye majimbo kwa mfano; tuhakikishe kuwa wakati wa kampeni hawafanyiwi unyanyasaji wa kijinsia!!
 
Back
Top Bottom