diana chumbikino
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 428
- 368
NCHI za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zimepinga Mkataba wa Kudhibiti Biashara ya Kimataifa ya Kuhifadhi Mimea na Wanyamapori walio hatarini kutoweka (CITES), unaowataka kuongeza idadi ya wanyama wanaozuiwa kufanyiwa biashara wakiwemo tembo, twiga na faru. Akizungumza katika maazimio ya mkutano wa mawaziri wa mazingira, maliasili na utalii wa nchi za SADC uliokuwa ukifanyika jijini Arusha, Dk Hamisi Kigwangalla alisema moja ya mambo yaliyojitokeza ni pamoja na nchi zilizoendelea kutaka kuongeza idadi ya wanyama watakaozuiliwa kufanyiwa biashara wakiwemo tembo, twiga na faru jambo ambalo haliwezekani.
Waziri Kigwangalla ambaye alikuwa mwenyekiti wa mawaziri wa SADC katika mkutano huo alisema masharti hayo ni magumu kwa ustawi wa bara la Afrika ukizingatia kwamba asilimia 80 ya nchi za Afrika zinamiliki na kusimamia maliasili hizo kama urithi pekee uliopo.
Tanzania na nchi nyingine za SADC zimekubaliana kwa maandishi kutounga mkono maamuzi hayo kwa sababu wanyama hao ndio tegemeo pekee kibiashara katika ustawi wa nchi za Afrika na wanaenda wawe na mamlaka kamili katika kusimamia maliasili zao. “Wanapozidi kuweka masharti magunu zaidi katika kusimamia maliasili zetu maana yake wanatukosesha mapato ambayo yanapatikana katika kufanyabiashara za wanyama pori,” alisema.
Naye Ofisa Wanyamapori Mkuu kutoka Mamlaka ya Wasimamizi wa Wanyamapori Tanzania, John Kaaya alisema maazimio mengine ni pamoja na kuwa na mashirikiano katika kulinda rasilimali zinazovuka mipaka. Mkakati mwingine waliokubaliana ni kupambana na ujangili kwa ajili ya wanyamapori ambao wapo hatarini kutoweka na suala la mabadiliko ya tabia ya nchi katika nchi za kusini mwa Afrika.
Alisema jambo lingine waliloafikiana ni kupinga mapendekezo ya mkataba CITES unaopinga matumizi ya wanyama pori kutumika kibiashara. Suala lingine ni kuridhia kwa itifaki ya mazingira, maliasili na utalii kwani hadi sasa ni nchi tatu ndio zilikuwa zimeridhia itifaki hiyo huku nchi zingine zikiwa bado.
Mpango huo utakuwa na manufaa makubwa kwa kuwa na sauti moja na mkakati wa pamoja katika kuridhia itifaki ambayo itakuwa na manufaa mbalimbali ikiwemo kuongeza idadi ya utalii kwa nchi wanachama wa SADC.