SADC kukutana ili kujadili hali ya DRC

SADC kukutana ili kujadili hali ya DRC

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) inatazamiwa kufanya kikao cha dharura kesho Alkhamisi, kujadili mgogoro wa kisiasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, uliobuka baada ya kutangazwa matokeo tata ya uchaguzi wa urais.

Mshauri wa masuala ya kidiplomasia wa rais anayeondoka mamlakani, Joseph Kabila ameliambia shirika la habaria la Reuters kuwa, mkutano huo wa dharura utafanyika katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. Hata hivyo hakutoa maelezo ya kina juu ya mkutano huo wa viongozi wa kieneo.

Awali SADC ilisema DRC inapaswa kufikiria suala la kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa baada ya nchi hiyo kukumbwa na mivutano kufuatia kutangazwa matokeo tata ya uchaguzi wa urais uliofanyika Disemba 31 mwaka uliomalizika.

[http://media]Martin Fayulu (kushoto) na Felix Tshesekedi

Hapo jana Jumatano Mahakama ya Katiba ilianza kusikiliza kesi ya Martin Fayulu, mgombea wa upinzani ambaye anapinga matokeo ya uchaguzi huo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi, akisisitiza kuwa, yeye ndiye aliyeshinda uchaguzi huo kwa zaidi ya asilimia 60 ya kura, lakini Tume ya Uchaguzi ikamtangaza mshindani wake, Felix Tshisekedi kuwa mshindi.

Alkhamisi iliyopita, Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (CENI) ilimtangaza Felix Tshisekedi wa chama cha upinzani cha UDPS kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais, kwa kujipatia asilimia 38.57 ya kura, akiwatangulia wagombea Martin Fayulu wa Lamuka na Emmanuel Ramazani Shadary aliyewakilisha muungano wa chama tawala nchini humo.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi members wa SADC wanaoweza kuikosoa Congo ni wangapi?

Wamuache huyo Tshesekedi na ushindi wake wa magumashi.

This is Africa.
Hapo ndipo unapokosea. Kumbuka hata mzazi anayevuta sigara anamkanya mtoto wake mdogo asivute.
 
Hapo ndipo unapokosea. Kumbuka hata mzazi anayevuta sigara anamkanya mtoto wake mdogo asivute.
Na awe mfano bora huyo mzazi kwa kuacha kuvuta fegi.

Ile Kauli ya "fuata maneno yangu na sio matendo yangu" isn't applicable kwny baadhi ya mambo mkuu.
 
Hivi members wa SADC wanaoweza kuikosoa Congo ni wangapi?

Wamuache huyo Tshesekedi na ushindi wake wa magumashi.

This is Africa.
Hivi unadhani SADC walikuwa hawajui Kabila atachofanya? Hapo wanamsafisha njia ya kutengeneza serikali ya umoja. Kabila na SADC ni wamoja.
 
Hivi unadhani SADC walikuwa hawajui Kabila atachofanya? Hapo wanamsafisha njia ya kutengeneza serikali ya umoja. Kabila na SADC ni wamoja.
Nalijua hilo,ndio maana nimesema SADC ni wangapi wanaoweza kuikosoa Congo?
 
Hivi members wa SADC wanaoweza kuikosoa Congo ni wangapi?

Wamuache huyo Tshesekedi na ushindi wake wa magumashi.

This is Africa.
Huenda ikaundwa serikali ya mseto wakagawana madaraka hao vigogo.
 
Waungane kama awataki warudie uchaguzi kama awataki wampe kwa mda kabila
 
Back
Top Bottom