GE2025 SACP Mtatiro Kitinkwi: Makosa ya kiuchochezi Mitandaoni hayavumiliki, ukihusika unashughulikiwa kisheria

GE2025 SACP Mtatiro Kitinkwi: Makosa ya kiuchochezi Mitandaoni hayavumiliki, ukihusika unashughulikiwa kisheria

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Akizungumza katika mahojiano ya kipindi cha Clouds 360, Kamanda wa Polisi Kinondoni, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Mtatiro Kitinkwi ameeleza kuwa yeyote atakayevunja sheria Jeshi la Polisi litahakikisha anashugulikiwa kwa mujibu wa sheria

Aidha ameonya kuwa sheria ifuatwe na wale wanaofanya makosa ya kiuchochezi kwenye mitandao ya kijamii hayavumiliki hivyo nao watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria


"Tunaendelea kutoa elimu mbalimbali kwa wananchi waendelee kuheshimu na kufahamu kwamba makosa hayo ya kiuchochezi kwenye Mitandao ya kijamii hayavumiliki na sisi kwa sababu tunafanya misako ya doria maeneo mbalimbali ikiwemo mitandaoni basi wale wote ambao wamejikuta kukinzana na sheria basi tunawashugulikia kwa mujibu wa sheria"- Amesema Kamanda wa Polisi Kinondoni SACP, Mtatiro Kitinkwi.

 
Back
Top Bottom